WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, January 26, 2016

USIVUNJWE MOYO MTAZAME MUNGU



January 26
Tafakari ya leo tuangalie tatizo la kuvunjwa Moyo katika maisha yetu; Tabia hii hutendwa sana pale ambapo unaonekana kuwa unafanya kitu sahihi lakini unapata matokeo hafifu. Wakati mwingine unajiona kuwa unafanya kazi kwa bidii lakini mafanikio hayaonekani na wale wanaokusaidia wanafurahia kushindwa kwako; upinzani uko hasa kwa wale wanaofanya vizuri.
Na ukiangalia sana hali hii ya kuvunjwa moyo inaumiza sana nafsi na moyo wa muhusika, wakati mwingine unaweza kufikiria hata kuacha kile ambacho umepanga kukifanya hata kama unafanya kwa maendeleo ya jamii yenye huhitaji; hata Yeramia alipatwa na khali kama hii;
Lakini tukumbuke kuwa pamoja na majaribu mbele yetu bado tunatakiwa kuwa watiifu na kutathimini wito wa wajibu wetu kwa Mungu na Jamii; Tunatakiwa tu kujiuliza  je ulifanyalo na unajikuta katia wakati mgumu wa upinzani umeitwa na Mungu ulifanye?
Kama ndio hata kama utavunjwa moyo kiasi gani hutakiwi kuacha kutenda kwani wakati ukifika Mwenyezi Mungu atakuinua tu kama alivyo mwinua Yeramia alipokuwa akipambana na matendo dhalimu ya Pashhur. Fundisho kutoka kwa Yeraamia ni kuwa aliitwa na Mungu kwa kazi yake, pamoja kuwa hata yeremia alimkasirikia Mungu lakini hakuweza kudharau wito na kazi ambayo mungu alimpa kuifanya na aliifanya.
Tunatakiwa kuwa makini na waangalifu na kutambua kuwa Mungu yuko nasi na tuendelee kujiombea na kuombeana; Yeramia  20:11 anavyotukumbusha kuwa Bwana yu Pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili watona aibu ya milele ambayo haitasauliwa kamwe. Hivyo tafakari ya leo inatulumbush kuwa bwana akiwa upande wako hakuna yeyote wa kukushinda au wakushindana nawe; mungu atawashughulikia iipasavyo wakati ukifika. Hivyo hatutakiwa kuwa na wasiwasi.
Najua kama binadamu wakati kama huu ambapo tunapovunjwa moyo tunajiangalia na kujiuliza maswali mengi kwa nini iwe hivi, mimi ninatatizo gani? Na kwanini naandamwa hivi kulikoni? Tunaishia kupata mfadhaiko ambao unaturudisha nyuma katika jambo njema ambalo ulikuwa unatakiwa kulifanya. Yeramia anatukumbusha kuwa tukiwa katika khali kama hii tunatakiwa tumwangalie zaidi Mungu na kujua kuwa kamwe Mungu hawezi kutuacha katika wakati kama huu yeye anasimama kama jemedari mkuu wakati wote wa majaribu. Jukumu ketu kubwa ni moja tu kumwomba yeye na kumtumaini yeye kwa imani thabiti.
Leo tunapotafakati kukumbuke kitu kimoja katika kila hali tutambuwe kuwa Mungu yu pamoja nasi anatembea sambamba nasi, anatuongoza na kutuepusha na kila hatari ambayo inakuja mbele yetu yeye hutukingia kifua cha ushindi.

Lakini hayo yote yatawezekana kama tutakuwa watu wa kusali, kumshukuru Mungu, kama Yeramiha alivyomsifu Mungu baada ya ushindi; Yer.20.13 mwimbieni Bwana  msifuni Bwana kwa maana ameiponya roho ya mhitaji katika mikono ya watu watendao maovu.

 

Tukumbuke kuwa tunapomsifu Mungu tunadhihirisha kuwa yeye ni kiongozi  na anaweza kufanya chochote anachotaka kufanya, lakini  tukumbuke kuwa mungu hutenda kila kitu kwa haki na upendo mkuu sana.

 

Tunapomsifu mungu tukumbuke kuwa tunatekeleza mambo  Haya makuu;

Kwanza tunamtambua kuwa yeye ni kiongozi wetu na hakuna mtu wa kutuvunja moyo kwani ametuita kufanya jambo njema ndani yetu na kwa jamii inayotuzunguka; hivyo kama yesu alivyo waambia makutano wasipomshangilia hata mawe anaweza akayafanya yamshangilie;

Pili tunatambua kuwa yeye ndiye mwenye mipango yote tukisoma Yer; 29:11 maana nayajua mawazo ninayowawazia  ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Tatizo ambalo linatusumbua tunatamani kuona kuwa tunaweza kufanikiwa bila nguvu ya Mungu. Lakini mungu anatupa nafasi ya kuchagua kkuhusu au kushindana na mwito wa Mungu au kukubali mwito wa Mungu na kamwe hata vunjika moyo.


Tatu tutambue kuwa tunamsifu Mungu sio kwa kufikiria nini anatufanyia  au nini kitatokea mbele ya maisha yetu bali tunatakiwa tumsifu Mungu kwa vile alivyo kwani yeye ni mwanzo na mwisho. Kama zaburi ya 22:3 inavyosema na wewe ni mtakatifu uketiye juu ya Israeli. Tukumbuke kuwa sala zinafungua milango ya matumaini zaidi ya kweli ndani ya maisha yetu. Kwa hiyo nguvu ya Mungu iko karibu yetu tukiwa tunamwabudu. tujifunze kuwa kama watoto wadogo wao wanafuraha daima na hata wanapovunjwa moyo husamehe na kusimama tena imara katika kucheza.

Hii ni tafakari yetu ya leo Mwenyezi Mungu apewe sifa ya utukufu uliotukuka Amina


No comments:

Post a Comment