Kama Kitabu cha (Yakobo 1:17) kinavyo chambua kuhusu Kila kilicho chema, kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye Kwake hakuna kubadilika: Swali ambalo mimi najiuliza leo ni hili je zawadi ya maisha ni zawadi iliyo bora hutoka kwa Mungu? Au kuna zawadi zaidi ya hii?
Leo hii mimi nainua mikono yangu juu nikimwambia Mungu asante sana kwa zawadi ya maisha yangu, kwa kweli ni zawadi bora ambayo Mungu amenijalia. Siku ya kuzaliwa ni siku muhimu sana katika maisha ya kila mmoja wetu, Leo mimi nasherekea miaka 46 ya uhai wa maisha yangu. Namshukuru Mungu kwani yeye amekuwa na anaendelea kuwa nohodha wa maisha yangu.
Nawashukuru wazazi wangu(Mzee Alois Na Mama Anna) na wazazi wa Mke wangu (Mzee Peter na Mama Trifonia) kwa kukubali kutuleta dunia na kututunza: ni wangapi ambao hawajepata nafasi hii ambayo sisi na (wewe) tumepata? Kuna wale ambao hawajefanikiwa kuona dunia hii au wale ambao waliiona dunia hii lakini maisha yao yalikatishwa kwa sababu yeyote ile. Bibilia inatufundisha kuwa watoto inatupasa tuwaheshimu wazazi wetu, hili ni jambo linalo mpendeza Mungu tukisoma (Wakorinto 3:20). Mwenyezi mungu ametuagiza kuwa inatupasa kuwaheshima Baba na Mama ili tuweze kupata heri na maisha marefu kwani wazazi wetu ndio waliochukua nafasi ya uumbaji, uwajibikaji wa mahitaji, ugawaji wa sheria mbadala na walinzi wa maisha yetu.
Bwana Na Bibi Alois Turuka
(James: 4:6) anatuabarisha kuwa tunapompa Mungu asante, tuna mshukuru yeye kama ndiye pekee mtoaji ya vyote tunavyovifurahia hapa dunia, tunasherekea ukuu wake na wema wake; na kwa kumshukuru yeye tunaonyesha unyenyekevu wetu kwake yeye; hii ni shukrani pekee ambayo tunastahili kumrudishia bwana kwa wema na Baraka zake.
Bwana Na Bibi Peter Myamba
Katka kusherekea siku yangu ya kuzaliwa Nawashukuru Mungu kwa kunijalia Mke Mzuri, Mwema, Mwenye huruma Mcha Mungu, mpenda watu hasa wale wanaohitaji msaada. Mungu Asante sana kwa kunipa Mke wangu Mpendwa Grace Peter Myamba Leo hii ninavyosherekea siku yangu ya kuzaliwa yeye amekuwa chachu ya mafanikio na mabadiliko ndani ya maisha yangu, yeye amekuwa mke bora kwangu, Amewezesha kunisaidia katika kufanikisha kazi zangu kama mfanyakazi, kama mzazi, daima amekuwa akitumia zaidi busara ya kutoa ushauri hata pale nilipokuwa nimeteleza kwa kusema ukweli kulingana na mafundisho ya bibilia, kushauriana na kukosoana kwa kutumia faragha ambayo tunastahili kuitumia kwa faida ya kulinda famila bora na kuimarisha misingi mizuri ya ndoa; ni mke ambaye anafahamu nini maana ya kusamehe na kusameheana kama ilivyoelezwa kwenye (Waefeso: 4:31-32).
Mrs Grace Peter Myamba
Daima amekuwa akizingatia msemo huu “ it is not so much what you say but how you say it” tunafahamu kuwa kuongea ni kipaji unaweza kuwa na hoja nzuri tu ukaharimu kwa namna ambayo utaongea; Ujumbe unaufikisha vipi kwa mwenzako na katika hali na mazingira gani? Namshukuru Mungu Grace (Mama Rose) amejaliwa kipaji cha kuufikisha ujumbe kwa namna ya ajabu, katika mantiki ya amani na upendo.
Grace ni mke anayemtegemea sana Mwenyezi Mungu, anamwomba bila kuchoka; kwake Mungu amekuwa kimbiliao lake kitika maisha yake na maisha yetu kama familia kila siku, Kama kitabu cha Mithali 31:10:, 31: 11-31, inavyosema ; Mke mwenye sifa nzuri, ni nani awezaye kumpata? Yeye ni wa thamani sana kuliko marijani. Mume wake anamwamini kikamilifu wala hakosi kitu cho chote cha thamani. Humtendea mumewe mema, wala si mabaya, siku zote za maisha yake. Naye hufanya kazi kwa mikono yenye bidii. Hufanya kazi zake kwa nguvu, mikono yake ina nguvu kwa ajili ya kazi zake. Huona kwamba biashara yake ina faida, Huwanyoshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake. Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake. huangalia mambo ya nyumbani mwake wala hali chakula cha uvivu. watoto wake huamka na kumwita mbarikiwa na mumewe pia, naye humsifu.
Mhubiri 9:9 Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua.
Ni ukweli mtupu kuwa ni vigumu sana kwa mwanaume kufanikiwa bila nyuma yake kuwapo na mwanamke. Mke ni Baraka na hasa mke mwaminifu na mwenye upendo ni lulu ya ndoa na familia yake.
katika kumbukumbu yangu ya siku yangu ya kuzaliwa Namshukuru Mungu kwa familia ambayo ametujalia, ninashukuru kwa binti ambaye ameleta furaha ndani ya familia yetu Rose Turuka ambaye ni zawadi ya upendo na amani. Binti huyu kwetu nifuraha, upendo na amani ya maisha yetu. Sisi tunajisikia kuwa na heshima kuwa ni wazazi wa binyi huyu; lakini kama bibilia inavyotufundisha kupitia kitabu chake cha Waefeso 6:4
Rose and Grace
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana. inatupasa kama wazazi tunatakiwa kuto waamshia watoto wetu hasira bali tuwafunze adabu kwa utaratibu wa Mungu.
Kama kitabu cha Mithali kinavyosema 22:6 wafundishe watoto katika njia wapasayo kwenda na hata atakapozeeka hatageuka kwenda kwenye njia isiyo haki. Akina baba, ‘simamieni nyumba zenu kwa njia nzuri.’ (1 Timotheo 3:4, 5; 5:8) Nanyi watoto, watiini wazazi wenu. (Wakolosai 3:20) Hakuna yeyote katika familia aliye mkamilifu kwa kuwa wote hufanya makosa. Kwa hiyo, nyenyekeeni na kuombana msamaha. Kwa hiyo Kila mmoja katika familia anaweza kuchangia furaha ya familia kwa kumwiga Mungu katika kuonyesha upendo. (Waefeso 5:1, 2)
Kwa kweli katika kusherekea siku hii muhimu ya kuzaliwa kwangu kwa unyenyekevu naomba nirudie tena kwa niaba ya familia yangu Grace; Rose ; Emmanuel tunashukuru na tunasema asante sana kwa Mwenyezi Mungu, kwa wazazi wetu, ndugu zetu na marafiki wote, kwa jinsi ambavyo mmechangia furaha na mafanikio ya maisha yetu; ni zawadi ambayo ni vyema sisi kama wana wa adamu tukaikubali kuwa ni zawadi ambayo haiwezi linganishwa na kitu chochote kile, na ni jukumu letu tu kumshukuru Mungu:
Grace and Emmanuel
Kwa kuhitimisha namaliza kwa kusema “Asante sana Mwenyezi Mungu kwa maisha yangu na familia yangu, wazazi wetu, pamoja na marafiki ambao umetujalia Baraka na upendo wa pekee, tunaomba uzidi kutubarika kadiri unavyotujalia maisha utaangazie neema zaidi, upendo, msamaha na uwe taa inayomulika katika haya maisha ambayo hayana uhakika kwetu, ni wewe tu ambaye unajua nini hatima ya maisha ambayo yako mbele yetu amina”.
No comments:
Post a Comment