JE YATUPASA KULIPIZA KISASI DHIDI YA WENZETU KATIKA MAISHA YETU?
Kwa hakika mwanandamu anahitaji upeo mkubwa wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia zote za kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la msamaha. Kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau, kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii.
Kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini pasipo imani haiwezekani (Waebrania 11:6). Inatufundisha kuwa mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na Mungu katika Imani.
Kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14 inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."
Wale walio wanyonge moyo wako mbele ya Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa Mungu ni; katika imani jambo ni rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hebu jitafakari kwa nini umekuwa na kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule?
No comments:
Post a Comment