WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, December 30, 2010

MWAKA MPYA 2011



Salamu za Mwaka 2011  kwa Uongozi na  wafanyakazi wa Marine Sciences Zanzibar.


Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuukaribia na hatimaye kwa uwezo na upendo wake kuufikia mwaka mpya 2011;

Kwa niaba yangu (Emmanuel Turuka) na familia yangu ( Mrs Grace na Rose) kwanza kabisa, naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujaalia uhai na kutuwezesha kukaribia na hatimaye kuiona siku hii muhimu tukiwa bado salama.  Ni vyema na haki  kumshukuru Mwenyezi  Mungu wetu kwani wapo wenzetu ambao tulikuwa nao pamoja kazini au katika familia zetu, hawakujaaliwa kuiona siku ya leo kwa vile wametangulia mbele ya haki.  

Tunamwomba Mwenyezi Mungu awape marehemu wetu wote mapumziko mema: Tunamwomba pia awape nafuu na kuwaponya wenzetu wote wanaougua maradhi mbalimbali ili wajumuike nasi katika  familia zetu na katika Taasisi yetu katika  kuleta mafanikio mafanikio ndani ya Taasisi yetu na katika familia zetu.

Napenda kukupongeza kwa namna ya pekee Mkurugenzi wa Taasisi yetu Dr. Margareth S. Kyewalyanga kwa kuweza kuiongoza kwa ustadi  Taasisi yetu (IMS) kwani  Taasisi bila uongozi bora ni vigumu kufikia malengo: katka mwaka unaomalizika ameweza kuiendeleza miradi mbalimbali na kuleta miradi mingine ambayo imekuwa na Tija kwa wafanyakazi na Taifa kwa ujumla. Mwenyezi Mungu azidi kukujalia upendo, busara na umadhubuti katika kutekeleza wajibu wako. Ikumbukwe kuwa watawala huwekwa na Mwenyezi Mungu kwa sababu Maalum na kwa wakati wake: swali ambalo unapaswa kujiuliza kwa nini nimekuwa kiongozi wakati huu? Ni mambo gani ambayo yanahitaji umakini zaidi katika kuwapa haki wale ambao wanahitaji msaada wangu katika kipindi cha mwaka unaokuja? Hasa wale wanyonge wanaotamani kujikwamua kimaisha ndani ya Taasisi yetu: Lakini hawana njia ya kutumiza ndoto zao: 


Dr. M.S.Kyewalyanga

Vile vile napenda kuipongeza timu nzima ya Manajimenyi ya Taasisi ikoongozwa  na Dr. Ntahondi B. Nyandwi ambaye daima amekuwa akifanya kazi kwa uadilifu na kuwajali wanyonge; nakufahamu vizuri na jinsi ambavyo umekuwa ukipigania haki za wafanyakazi hasa wale ambao sauti zao hasisikiki ; nakumbuka miaka yote ambayo tumekuwa tikifanya kazi pamoja Bravo, Mwenyezi Mungu azidi kukupa nguvu  katika mwaka wa 2011 katika kutimiza wajibu huo bila kuchoka;

                               Dr. N. Nyandwi

Mwisho ni kwa wafanyakazi wote na wanafunzi nawatakieni kila la kheri katika mwaka 2011, daima tukumbuke kutimiza wajibu wetu; Mwenyezi Mungu katika mwaka mpya atushushue  rehema zake ambazo zimejaa afya njema, na uadilifu ili tuweze kutimiza ndoto zetu za maisha na za kazi; tukumbuke kuwa Kumaliza mwaka ni mwanzo wa mwaka mwingine, na unapoanza mwaka ni lazima tuanze na mikakati mipya. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu atujalie mwaka wenye furaha na mafanikio.

Asanteni sana na Mungu atubariki sote tuupokee Mwaka mpya na kuushangilia kwa Moyo mkunyufu na upendo.

 Ni mimi Mfanyakazi Mwenzenu Emmanuel Turuka pamoja na familia yangu Mrs. Grace na Rose Turuka

1 comment: