WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Saturday, April 30, 2016

MUNGU WETU ANATAKA TUBADILI TABIA ZETU

April 30


Tafakari yetu ya leo Mungu wetu anaendelea, kutuelekeza kuwa tunatakiwa tubadilisha, tabia zetu ili tuweze kulingana na maandiko ya biblia na utukufu wake;

Friday, April 29, 2016

JE WOKOVU NI HAKI YETU?



April 29

Isaya 55:8-9

Tafakari ya tunaangalia dhana nzima ya wokovu kama ni haki yetu. Ukiisoma na kuielewa Bibilia vizuri inatufundisha kuwa wokovu sio haki yetu bali ni neema ya Mungu tu; tukiangalia katika nyakati tofauti na kwa matukio tofauti Mwenyezi Mungu alitutengenezea njia rahisi ya uokovu kwa kuweka misingi mizuri  ambayo alitutaka sisi tuifuate; lakini katika mazingira haya yote kwa ujinga wetu; kwa kiburi chetu na kwa kukosa maarifa ya kimungu tuliishia kupoteza neema hii ya Kimungu. Tumekuwa watu ambao hatuishi kwatika kiwango ambacho Mungu anaweka sisi tuishi. Angali nini Kilitokea katika Bustani ya Aden;

Tafakari yetu inatukumbusha leo maneno ya  Nabii Isaya 55:8-9 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.  Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maneno haya mazito yanatoka na jinsi ambavyo sisi tumeshindwa kutembea katika njia za bwana. Tulitayarishiwa makao mazuri ili tutembee na bwana tumeshindwa kwa sababu ya Kiburi chetu.

Tafakari yetu leo inatakiwa itukumbushe kuwa tunatakiwa kushukuru kuwa wokovu ni neema ya peeke ambayo tumeipata na nguvu ambayo Mungu ameiweka ndani yake kwa wokovu wetu; ni wajibu wetu kuendelea kufanya maungamo ya dhambi zetu katika kuimarisha hii neema ya wakovu. Ni kweli kuwa sisi sote tumefanya dhambi na kupungukiwa utukufu wa Mungu. Ndio maana kwa upendo wake Mungu bado ameendelea kutuokoa kwa neema yake ili tusiingie katika moto wa milele. Huruma na neema ya Mungu haina mfano sisi ni kama majani yanayopuputika katika mti lakini Mungu kwa upendo wake anatuokota na kutupa sisi huruma ya ya kimungu ya wokovu. Pamoja na dhambi zetu bado tumekaribishwa katika uzima wa milele;

Wakovu wetu u mikononi mwa Bwana kwa upendo wake na huruma yake hataki hata mmoja wetu apotee wajibu wetu ni kuomba msamaha na kuishi kulingana na njia zake; Je wewe na mimi tunatumiaje neema hiiya wakovu. Hii ndio tafakari yetu ya Leo


Emmanuel Turuka

Thursday, April 28, 2016

IPO NJIA - NAYO NI YESU

April 27


Tafakari ya leo katika kila jambo tulifanyalo na ugumu wowote ambao utajitokeza tukumbuke kuwa iko njia na kuweka mambo sawa; na jibu la hilo ni Yesu pekee ambaye ndiye njia.

Tuesday, April 26, 2016

MWILI WAKO NI BUSTANI YA KWELI YAMUNGU?



April 26

Tafakari ya leo tujipime   kama mwili wako  ni  bustani ya kweli ya Mungu?  Tukumbuke kuwa Adam na Hawa baada ya kuumbwa walikabidhiwa bustani ya Aden ambayo ilikuwa na kila kitu.

Mungu aliwaambia kufurahi kila kitu katika bustani ile na walikuwa na mamlaka ya vitu vyote ambavyo vilikuwa katika bustani ile.

Tafakari yetu inatukumbusha jinsi Mungu alivyowaambia vyote tumieni lakini mti huu msiuguse. Hivyo hivyo Mungu anaongea nasi leo akitoa maelekezo kuwa : mwili wako ni bustani Takatifu niliyokukabidhi yafurahie maisha na  vitu vyote ambavyo viko ndani ya mwili wako na  hatutakiwi kuvunja amri za Mungu ambazo ni mwongozo wa maisha yetu bora.

Tafakari yetu inaonya kuwa pamoja na  Yesu kutufia msalabani lakini bado tunatakiwa kutumia mwili wetu ambao  ni bustani ya Mungu kwa hekima kubwa.  Kama tutavunja amri za  Mungu nasi tutakuwa kama Adam  na  Hawa tutalaaniwa na kuondolewa katika bustani ya  uzima wa milele.

Tafakari yetu leo inatupa mwamko Mpya kuwa tunatakiwa kuitunza bustani hii ya ajabu ambayo Mwenyezi Mungu ametutunukia kwa kuimwagilia, kuitilia mbolea, na kuifyeka vizuri kila siku kwa kusali bila kuchoka.

Mungu wetu ni mwingi wa huruma, amejaa upendo na anataka kuona kuwa bustani ambayo ametukabidhi ikiwa inastawi; lakini haiwezi kustawi bila msaada wake na  utayari wetu wa  kufuata amri zake.  Hivyo  ni wajibu wetu kuendelea kuomba na kushukuru wakati wote wa  uhai wetu. 

Hii ndio tafakari yetu ya  leo. Amina

Emmanuel Turuka

Monday, April 25, 2016

ZAO LA CHUKI KATIKA MAISHA YETU;


April 25

WAEFESO 4:31,32

Tafakari yetu ya leo tunaangalia ni zao la chuki na hasara yake katika maisha yetu ya kiroho; tukumbuke kuwa zao la chuki huzaa hasira na ghadhabu. Tukisoma Waefeso 4:31,32 inatukumbusha kuwa Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheana  kama na Mungu katika Kristo alivyosamehe ninyi. Lakini tukumbuke kuwa sisi sote  tumesulibiwa pamoja na Kristo, hivyo hatutakiwi kukaribisha chuki ndani ya maisha yetu;

Tafakari yetu inaweka sawa kuwa zao la chuki husababisha hasira ambayo huleta uchungu hivyo Mara nyingi UCHUNGU husababisha akili kushindwa kufanya kazi ipasavyo.        Ni hali ya kutokuwa na furaha, kujawa hasira zilizotokana na kutendewa mabaya.  Ni hali ya kuhisi huzuni nzito ambayo wakati mwingine inaweza kuchangamana na maumivu makali katika fahamu za mtu, ambayo yaweza kusababisha mwili kunyong'onyea na kusababisha akili kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri. Bibilia inatukumbusha kuwa ili kuweza kuondokana na zao hili la chuki basi Wakolosai 3:1-3 basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu, yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu


Tafakari yetu pia inatueleza kuwa zao la chuki pia huleta ghadhabu ambayo nia  hali ya mtu kuwa na maamuzi ya pupa pasipo kujali madhara yake. Hali hiyo yaweza kumfanya mtu kuwa na majibu ya mkato mkato, kutopenda kuulizwa ulizwa; humfanya mtu kuwa mgomvi na  kutopenda kuwa na subira;  Chuki husababisha kuvunja amri za Mungu kwani bila kutarajia hujikuta mtu kufanya matendo ambayo hayampendezi Mungu kama vile kuwa chanzo cha matusi; hasira; kukosa upendo ndio maana tukisoama Mithali 22:24-25 inatukumbushja kuwa Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.

Tafakari yetu pia inatukumbusha kuwa zao la chuki husababisha sadaka yako isipokelewe mbele ya madhabau ya Mungu; mathayo 5:23,24  Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Tukumbuke kuwa Mungu huchukizwa na sadaka za mwenye dhambi. Sadaka za mtu mwenye dhambi hazipokelewi mbele za Mungu.  Chuki ni ubaya ambao Mungu haupendi; tukumbuke kuwa  ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na wema - kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Tafakari yetu msisitizo mkubwa ni Chuki huleta ubaya, na huleta kisasi kwa sababu ya ghadhabu hivyo tunakumbushwa kuwa hatutakiwi kulipiza kisasi, bali tujiepushe na ghadhabu ambayo ni zao la chuki; Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili ya mambo mabaya uliyofanyiwa. Huwezi kulipa kisasi bila ya kumchukia huyo unayejilipizia kisasi kwake. Na Biblia inasema hivi: 1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajuaya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. Ni kweli Chuki huzaa kisasi, na huzaa dhambi ya kuua!  Isaya 59:2b inasema; dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.



Tafakari yetu inatutaka kujikosoa wenyewe na kutubu kwa kujiepusha na dhambi ya chuki tunatakiwa tujenge upendo kwani Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu; 1Wakorintho 13:4 – 8 upendo hautakabari; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli huvumilia yote; huamini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote. Tukumbuke kuwa upendo huu umo ndani yako, na ndio unaokufanya uwe kiumbe kipya.
Tukumbuke maneno ya Yesu aliposema Mathayo 4:11, 12  Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia;kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Hii ni tafakari yetu ya leo ni  zao la chuki ni hasira, ghadhabu; na kadhalika tujiepushe kusongwa na maudhi pamoja na makwazo mbali mbali yatokanayo na chuki. Amina

Emmanuel Turuka




Sunday, April 24, 2016

WAJIBU WETU KUWA NA UPENDO

April 24


Tafakari ya leo tuendelea kudumisha upendo wa kweli ili tuweze timiza ile amri kuu ya Upendo kwa vitendo na sio kuwa wanafiki wa upendo kwa maneno matupu. Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe amina

Saturday, April 23, 2016

NI WAJIBU WETU KUOMBA

April 23


Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa katika lolote ambalo liko mbele yetu ni wajibu wetu sisi kuomba kwani tumefundisha na Bwana wetu katika kila kitu wajibu wetu ni kuomba na kushukuru. Hakuna ugumu wowote katika hili kufanikiwa kama kweli tunaomba. Tatizo letu hatuombi na kama tunaomba hatuombi katika namna ile inayotakiwa.

Friday, April 22, 2016

MAMBO YA YESU - NI BOMBA

April 22


Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa mambo yte yanapatikana kwa yesu; Nini unachotaka ambacho hutapata ndani ya yesu? jibu ni hakuna kila kitu kipo ndani ya Yesu; ni wajibu wetu kukitafuta na kufuata maelekezo jinsi ya kupata. hivyo Yesu ni jibu la Matatizo na shida zetu; Yesu ni jibu la furaha yetu; Yesu ni kielelezo kizuri cha maisha yetu. Hivyo tusisahau kuwa mabo yote ni wka Yesu.

Thursday, April 21, 2016

WEMA WA MUNGU UMENIZUNGUKA

April 21

Tafakari ya leo tumshukuru Mungu kwa wema wake ambao umetuzunguka kila iitwayo leo; Tunaamka kwa neema ya Mungu na tunafanikiwa kwa neema yake pia. tunakila sababu ya kushukuru wema wa Mungu.

Tuesday, April 19, 2016

TAZAMA WEWE NI MUNGU



April 19

Zaburi 150:6




Tafakari ya leo tuungane na zaburi ya 150: ambapo tunatakiwa kumwana Mungu kuwa yeye ni jibu la matatizo na maombi yetu. Mungu hashindwi na wala hatashindwa na kitu chochote; Tatizo letu binadamu ni uhaba wa imani ambao ndio unatukosesha ushindi mkubwa wa matatizo yetu.

Monday, April 18, 2016

WEMA NA UZURI WA MUNGU


April 18


Zaburi  27:4.  

Tafakari ya leo tuangalie je ni kitu gani sisi kama binadamu tunakihitaji zaidi kutoka na uzuri wake. Kitu kimoja mimi, wewe na dunia tunahitaji ni kuishi ndani ya Mungu. Kuishi katika uwepo wa mungu katika siku zote zote na kuona uzuri wa mungu kila siku za maisha yetu; kugusa uzuri wa Mungu, kunusa uzuri wa Mungu, kuonya uzuri wa Mungu. Katika ulimwengu wa leo tuko mbio sana na vitu ambavyo mwisho wa siku havina faida kubwa kwetu. Ulimwengu wetu haujetawaliwa na uzuri wa Mungu kwani vita na mapigano ndio vinaendelea kuchuakua uzito na kupoteza uzuri wa Mungu; kwa kweli katika ulimwengu wa leo tunahitaji uzuri wa Mungu ambao ni amani na upendo.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kama tunavyohitaji chakula kwa ajili ya miili yetu, hivyo hivyo tunahitaji uzuri wa Mungu katika kurutubisha roho zetu; Mungu daima anatupa sisi uzuri wake ili kuimarisha roho zetu, lakini ni wajibu wetu sisi wenyewe kupokea na kutunza uzuru huo; kwani tukipokea uzuri huu ndio unaoleta nguvu, Baraka na mafanikio ndani yetu. Kupokea ua kuto pokea ni kitu kimoja. Lakini kufurahia na kushukuru ni kitu kingine; hatuwezi kuelezea uzuri wa Mungu sisi wote kwa namna moja ila kila mtu ataelezea kwa namna tofauti kulingana na jinsi alivyogusa, alivyonusa na alivyo onya; kama Zaburi ya 27:4 inavyosema Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake. 

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mungu ni ukamilifu wa vyote na mmiliki wa vitu vyote vizuri na sio vibaya . vitu vibaya ni matokeo ya kazi ya mikono yetu sisi binadamu na sio mikono ya Mungu. Vitu vyote vizuri, iwe tabia, utendaji wa kazi, maadili mema, uwajibikaji malezi ya vijana yenye maadili mema, ndoa zilizo bora ni kazi ya matunda ya uzuri wa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mungu hayuko ili awe sehemu ya kichwa chako kama hiyo ingekuwa hivyo basi kulikuwa hakuna sababu ya yeye kukujua wewe; kwa sababu wewe pia ungemjua Mungu zaidi na mipango yake yote; Mungu ni mkubwa zidi yetu na ufahamu wetu, yeye ndiye mwanzo na mwisho, mjengaji na mbomoaji wa jambo lolote line ambalo analiona linakwenda kinyume na taratibu zetu; mungu lazima awe hivyo ili tuweze kuona na kufurahia uzuri wake; jukumu letu ni kuendelea kujifunza kuhusu Mungu na kuendelea kumpenda kwa akili zetu zote ambazo ni zao la wema wake kwetu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa wema na uzuri wa Mungu ni zao la Limungu. Sio kila kitu tukifanyacho hapa dunia ni kizuri na kinaakisi wema wa mungu bali lazima kipate kionyo cha kimungu; maadili ya kimungu; tukizingatia kuwa Mungu yeye mwenyewe ni mkamilifu katika nyanya zote; la msingi tumepewa nafasi pamoja na mapungufu yetu ambayo yanaharibu wema na uzuri wa mungu katika maisha yetu; yatupasa bado kumpelekea Mungu Masanduku yetu ya ubaya wetu ili tuombe msamaha kwa ni yeye kwa wema na uziri wake bado amejawa na huruma na atatusamehe ili yuweze furahia uzuri wake; mungu daima anataka kutufanya sisi kuwa sehemu ya uzuri wake kwa kutusafisha na kutusamehe dhambi zetu.

Hii ndio tafkari yetu ya leo Amina


Emmanuel Turuka

Sunday, April 17, 2016

MAOMBI MAZITO AMBAYO YESU ALIFANYA JUU YETU KWA BABA


APRIL 17

zaburi ya 37: 4

Tafakari ya leo tuangalie na tuzingatie maombi mazito ambayo Yesu alituombea kwa Mungu ili nasi tuweze kuwa na uzima wa milele; utumishi wake hapa dunia ulikuwa kwa ajili ya ukombozi wetu japo hatutaka kukombolewa naye; Alipingwa kila kona hasa na wale ambao walijiona kuwa wao wanafahamu zaidi kuhusu sheria na kanunu kulingana na mafundisha ya mapokeo; pamaja na kukataliwa bado alitupenda na hata kutusamehe kwa mara nyingine alipokuwa anakufa msalabani;

Kwa pamoja tuitafakari hii sala ya Yesu kutoka katika kitabu cha Yohana 17-1-26 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; 
kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. 
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. 
Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. 
Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 
Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. 
Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. 
Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 
Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; 
10 na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. 
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. 
12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie. 
13 Na sasa naja kwako; na maneno haya nayasema ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao. 
14 Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 
15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 
16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. 
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. 
18 Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma hao ulimwenguni. 
19 Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao watakaswe katika kweli. 
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi. 
24 Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. 
25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. 
26 Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Hivyo Tafakari tukisoma pia Waebrania 12:2 inatukumbusha kuwa tunatakiwa kumtaza Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. kwa hiyo ni wajibu wetu ili kuweza kupata na kufurahia haja za mioyo yetu. Hii ni Tafakari ya leo Amina

Emmanuel Turuka


Saturday, April 16, 2016

NIONGOZE EE BWANA

April 16


IMANI YAKE ILIMPONYA ALIPOGUSA PINDO LA VAZI LA YESU

April 15

Tafakari yetu leo tunatakiwa kuishi kwa imani na matumaini ya mafanikio mbele ya Mwokozi wetu; Tuwe kama yuek mama aliyekuwa akisumbuliwa na kutoka damu kwa miaka 18 lakini baada ya kumwona Yesu alijiambia Moyoni mwake kwa ukuu wake na kwa nguvu yake nikigusa hata pindo tu la vazi lake nitapona; na ikawa hivyo; je wewe na mini tunaishi kwa imani hiyo katika maisha yetu ya kila siku tunapokabiliwa na magonjwa na tabu mbalimbali?

Thursday, April 14, 2016

WATU WANGU WANAPOTEA KWA KUKOSA MAARIFA



APRIL 14

 Hosea 4:6

Tafakari ya leo tunaangalia jinsi gani tunavoangamia kwa kukosa maarifa. Je ni maarifa gani hayo ambayo yanatusababisha sisi tuangamie Hosea natukumbusha kuwa Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Hii ndio elimu na Maarifa ambayo tunakumbushwa kuwa tumeshindwa kushika na kufuatilia. La msingi tunatakiwa kugundua kuwa tumekuwa tukikosa kujua elimu ya Mungu. Kama vile Mungu kupitia Hosea 4:1,2 aliwambia Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi.  Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kuna uhusiano wa karibu sana kati ya matendo yetu ya na matendo ya kiroho; matendo yetu daima yanatutuma na kutufanya uwajibikaji wetu katika maisha ya kiroho yakiwa yanapungua sana; tunaishia kuwa wabinafsi; tunajiangalia sana wenyewe na tunasahau kabisa nafasi yetu ya kumtumikia Mungu na kukosa kabisa maarifa katika utumishi wa Mungu wetu. Bila kujijua watu wengi tunaishi katika giza na kuvunja amri ambazo Mungu alitaka sisi kuzifuata na kuishi kulingana na amri hizo.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa maarifa ya Mungu ni ukweli, mara nyingi hatusikilizi ukweli wa maagizo au mafundisho ya Mungu kupitia Bwana wetu Yesu kristo au kupitia mitume au wafuasi wake; matokeo yake ndio kiama chetu au maangamizo yetu kwa kukosa maarifa ya kweli ya ufalme wa Mungu; Matthew 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya. 

Tafakari yetu ni kweli watu wengi wanajidai kumtumikia Mungu lakini katika uhalisia hawafanyi hivyo; utawezaje kumtumikia mungu kwa maneno na sio matendo? Utawezaje kumtumikia Mungu wakati hufuati amri zake? Huu ndio ukosekano wa maarifa ambayo yanpelekea watu kufanya matendo ambayo yanapingana na maneno yao, kuua , kuiba, kudhulumu yatima na hata kosa la uzinzi. Kwa vile hatuna maarifa yaliyosahii hatuwezi kutatua shida au matatizo yaliyo mbele yetu matoke yae tunaendelea kuangamia bila wenyewe kujijua. Mungu ametupa sisi maarifa ya kuwa wakweli ili tuweze kutimiza amri au sheria nyingine zote bila kushindwa; lakini kwa vile tumekataa maarifa ya kuwa wakweli sasa tutawezaje  kutatua changamoto za kiroho ambazo ziko mbele yetu.  Matahali 3: 19- 23 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;  Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza mande.  Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara.  Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako.  Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa. Hiiyote tunatakiwa kuwa na maarifa ya kimungu.

Tafakari yetu bado inatukumbusha kuwa  Mithali 24: 3-4 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza. Ukweli ambao ndio msingi wa maarifa ya Kimungu ni chanzo cha mafanikio yote, ukweli utakufany uwe mnyenyekevu, ukweli utakupa busara; lakini moyo wako ukijaa choyo, wivu, majivuno na unafiki ni wazi kuwa hii ni kithibitisho cha maangamizi. Hivyo ni wajibu wetu kujitathimini kuhusu tafakari hii na kumrudia Mungu na kuomba neema ya maarifa yatokanayo na mungu ambayo ni msingi wote wa upendo, amani, uwajibikaji, huruma kwa wajane na wazee, na tukumbuke kuwa Busara na Hekima hutolewa na Mungu na katika Mdomo wake ndipo maarifa na ufahamu hutolewa; Hekima ya Mungu daima inaingia ndani ya Mioyo yetu na kukaa nasi. Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina

Emmanuel Turuka






BWANA NAKUINUA UMENITOA MBALI

April 11

Tafakari yetu tukumbuke maisha yetu mpaka hapa tulipofikia tumepitia majaribu na shida kwa namna gani? ni jambo ambalo binadamu wengi tunapambana nalo japo tukifanikiwa kamwe hatukumbuki mkono wa Mungu juu ya ushindi wetu; wimbo huu ni mzuri ambao unatukumbusha kuwa daima tuendelee kukumbuka ukuu wa Mungu katika maisha yetu Amen 

Wednesday, April 13, 2016

UKOSEFU WA UADILIFU NA UWAJIBIKAJI


April 13

2 Petro 2:19

Tafakari ya leo tuangalie kwa namna gani ukosekano wa uadilifu na uwajibikaji husababisha watu kutokutekeleza majukumu yao ya kiroho katika namna ambayo inampendeza Mungu;Tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Kwani inatupasa kutambua kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu. Lakini ridhaa hiyo haitolewi hivi hivi tu, inaambatana na amana, kwamba waongozi watatekeleza dhamana  na wajibu  wao kwa makubaliano na maelewano ya kufuata barabara na kuheshimu ipasavyo kanuni na maadili fulani yanayoitambulisha na kuiongoza jamii husika. 

Tafakari yetu inalenga kumwonyesha kiongozi muadilifu jukumu lake ni kufanya kila bidii kuhakikisha amani na utulivu wa kweli katika nchi vinapatikana. Amani na utulivu ni chachu ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao kujiletea maendeleo. Maendeleo hayaji mahala penye magomvi na hasama. Lakini na amani na utulivu pia haviji mahala pasipo na haki na uadilifu. Uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi hupelekea hasara ya maisha na mali ya watu na hayo hayawi malengo ya uongozi muadilifu katika nchi
Maamuzi ya kiongozi wa kisiasa huathiri taifa zima pamoja na ukuaji wa kiroho, busara na hekima huzaa maamuzi yanayotokana na tafakuri ya kina, yanayozingatia hali halisi ya mambo na maslahi na manufaa ya muda mrefu. Kiongozi muadilifu anatakiwa ayaone haya na ayazigatie kwa kila hatua anayochukua. Tukubali tu kuwa njia ya kusonga mbele ni kukubali kutofautiana katika fikra lakini tubaki kuwa wamoja.

Tafakari yetu inasisitiza kuwa kikwazo kukubwa sana cha uadilifu na uwajibikaji ni matumizi mabaya ya ofisi kwa masilahi ambayo hayagusi maisha ya wananchi, rushwa na matumizi mabaya ya pesa ni miongoni mwa malalamiko makubwa katika hoja hii. Rushwa ni miongoni mwa matatizo yanayoikabili dunia nzima kwa ujumla.

Kipimo kimoja kikubwa cha uongozi bora ni uwezo wa kusimamia rasilimali za wananchi, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo na kumcha Mungu; kiongozi akiwa na vitu hivi huzaa hekima ua uwajibikaji wa kweli na uzalendo wa kupenda nchi yako na kusimamia rasilimali zake kwa faida ya Taifa.

Tafakari yetu ya leo inatuonyesha kuwa  baadhi ya viongozi wetu kutumia nguvu zao  sio kuondoa umasikini bali kuongeza umasikini kwa mtanzania wa kawaida. Hivyo hata kumletea maisha yake ya Kiroho kuyumba na kuingia katika vitendo ambavyo havimpendezi Mungu. Ni wajibu wa viongozi wetu kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwa misingi ya haki na sheria wakikumbuka kuwa hata wao wamechaguliwa na Mungu ili kutimiza adhima ya Mungu Dunia.

Hii ndio tafakari yetu ya leo;

Emmanuel Turuka


Tuesday, April 12, 2016

HATUTAKIWI KUKATA TAMAA

April 10


Tafakari ya leo tuungane na Mwimbaji Solomon katika wimbo wake ambao anatuasa kuto kata tamaa; maisha yetu yamejaa kila aina tabu ni rahisi sana kukata tamaa. ni rahisi kukata tamaa kama hatutamtanguliza Mungu mbele; Tumweke Mungu Mbele tutashinda bila tabu.

PETRO: ONDOKA KWANGU SHETANI WEWE




April 9

Yohana 1: 42

Tafakari ya leo tunaangalia maisha ya Yesu na wafuasi wake hasa mkasa wetu siku ya leo utakuwa kwa Mtume Petro, ambaye pamoja na udhaifu wake kama Binadamu yeye ndiye alikuwa msingi wa kanisa la Kristo; tukisoma Yohana 1: 42 Petro alikuwa  mfuasi wa kwanza wa Yesu; Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe). Petro alikuwa na sifa nyingi moja alikuwa msemaji, au mropokaji, alikuwa rafiki wa karibu sana wa yesu; petro alikuwa mtu mwenye hari kubwa; nguvu za kuwateka wengine; mwenye msukumo; jambo nzuri yesu aliendelea kumnyosha taratibu ili kuwa kiongozi mzuri wa Kanisa wa baada yake;

Tafakari ya leo tunaona kuwa Petro alikuwa ni mtu wa kwanza kukiri kuwa Yesu alikuwa ni mwana wa Mungu. Petro alikuwa kati ya wale mitume watatu ambao Yesu alikuwa nao karibu sana, na aliokuwa anafanya nao majukumu mazito ambayo yaliwadhihirishia kuwa yeye sio wa kawaida. Ni hao watatu ambao walikuwapo Yesu alipomfufua Yule binti wa Jairus tukisoma Marko 5:37; ni hao watatu walikuwa Yesu alipogeuka sura  Mathayo 17: 1 na ni hao watatu walipewa Jukumu la kuandaa karamu ya Mwisho Luka 22:8
Katika nyakati tofauti Petro ameonekana mwenye ari ya kufanya jambo kubwa lakini punde anakuwa hana imani tena na matokeo yake kupoteza lengo; Mathayo 14: 28-29 alipojaribu kutembea juu ya maji kisha  akaanza kuzama; 

Alikuwa petro ambaye alitamani wajenge vibanda vitatu baada ya tukio la kugeuka Sura Yesu lakini aliposikia sauti toka mbinguni aliogopa na kuanguka chini kujificha. Mathayo 17:4; Ni huyu huyu Petro ambaye alimwita pembeni na kumkataza yesu  asizungumzie Kifo chake Mathayo 16:22 lakini akasahihishwa na Yesu;  Alikuwa Petro ambaye alimkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu na kasha akaambiwa arudishe upanga wake Alani Yoana 18:10; na alikuwa Petro ambaye alimwambia Yesu kamwe hatamwancha au kumsaliti Yesu wakti wote wa Mateso yake. Mathayo 26:33

Tafakari yetu pamoja na mapungufu ya Petro  bado Yesu alimpa cheo cha kuwa ndiye mwamba na juu yake atalijenga kanisa lake; Mathayo 16: 18-19; tunachojifunza katika maisha ya Yesu, na Petro  alipata nguvu kutoka kwa Yesu pale alipomwambia kuwa anaweza tembea juu ya maji na udhaifu wake wa imani ndio ulimfanya aanze kuzama; 1 Yohana 4: 18 katika mifano yote hii Yesu anaelewa udhaifu wetu ambao unatokana na akili zetu na miili yetu ya kibinadamu; tunakosa nguvu na uwezo wa kufanya au kushawishi nini yatupasa kufanya kwa haki; yesu alitambua kuwa mitume wake pamoja na Petro walikuwa hawana nguvu hiyo bado; na hivyo walikuwa hawawezi kuona hata mapungufu yao katika kutimiza kazi ya kitume pamoja naye;

Katika tafakari ya maisha ya Petro tunaona kuwa alikuwa jasiri wa kuweza kujaribu mambo mengi magumu ambayo wafuasi wenzake walikuwa hawawezi kuyafanya; alimwambia Bwana wetu yesu Kristo kuwa bwana mimi nitakuwa nawe wakati wote wa mateso yako; ni Petro Peke yake ambaye aliweza kutoa ahadi hiyo; Pamoja na kuwa hakuweza kuitimiza lakini aliweza kumfuata Yesu katika safari yake ya mateso; Bahati mbaya tendo la Kumkataa Yesu kuwa hamtambui ni sababu ya udhaifu wa ubinadamu wetu; hata kama mimi na wewe tungekuwa katika viatu vya peter pengine tusingeonekana tena mara baadaya kuulizwa mara ya Kwanza. Peter alilia sana mara baada ya jogoo kuwika kwa sababu alijua kuwa amemsaliti Bwana wake na Rafiki yake

Je hadithi hii ya Petro inatufundisha nini sisi; Pamoja na kumwona Petro kuwa na imani haba lakini aliweza kuthubutu alipomwomba Yesu naye atemebee juu ya Maji aliweza kushuka kutoka katika Boti na kuanza kutembea lakini hakuweza kuendelea kuamini kuwa amepewa nguvu na mamlaka ya kutembea juu ya Maji, alipopoteza tu imani hiyo aliaanza kuzama na yesu akamwokoa. Katika maisha yetu ya kawaida sisi tumekuwa ni sehemu ya Petro kwani hatusimami kwenye ukweli wa imani juu ya matendo yetu dhidi ya wenzetu; tu rahisi sana kuacha njia bora ya Mungu kwa kuangalia makando kando ya mapito ya dunia hii; hivyo bado tunaneema ya kusaidiwa na mwokozi wetu pale tunapoelekea kuzama.
Je leo hii katika nafasi ambazo tumezipata za kuweza kuwasaidia wenzetu katika kumjua Kristo na kuishi maisha ya Upendo tunamtumainije Mungu? Je tunafanya jitihada gani za kueneza wokovu wa Mungu kwa wenzetu? Je tumekuwa watu wa kuogopa kulitaja jina la Yesu mbele ya wenzetu? Petro alionyesha mfano mzuri kwani aliweza kuleta wokovu wa kweli kwa Mataifa hasa yale ambayo yalikuwa hayamjui kabisa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa hadithi hii ya Petro inatukumbusha kuhusu maanguko yetu ya wakati tofauti tofauti; kama ilivyokuwa kwa Petro tunajua jinsi vile Mungu alivyoweza kumsamehe na kumtumia katika njia ya ajabu kwa ajili ya wokovu wa binadamu ndivyo Mungu anavyotaka kukutumia wewe leo kwa ajili ya taifa lake; Mungu wetu upendo wake hauna mipaka; neema yake haina mwisho; na msamaha wake ni wa milele; tujikumbushe kuwa hata pale tunapokuwa tumeanguka tujue kuwa bado Mwenyezi Mungu anatuweka katika hesabu yake;
Jambo la msingi leo tunapoyaangalia maisha ya Petro na utumishi wake kwa Krito ni umuhimu wa kusali bila kuchoka tukiruhusu tu maisha ya sala kufa tujue wazi kuwa tunajitengezea maisha ya kushindwa katika vita yetu dhidi ya shetani; mafanikio ya kumpigania Kristo yanapatikana tu kwa kuweka  Mungu mbele katika sala; Hivyo tafakari yetu ya leo inatukumbusha maisha ya sala ni maisha pekee ambayo lazima tuyapiganie siku zote za maisha yetu. Lakini pale ambapo hatufanyi jitihada za kumtafuta mungu kupitia sala tujue kuwa  tunajitafutia matatizo makubwa katika maisha yetu; lazima tutembea pamoja naye katika sala kama Petro alivyofanya;  Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa hatuwezi fanikiwa kwa nguvu na uwezo wetu pekeyetu; yesu alimwambia Petro ondoka mbele yangu shetani wewe kwani alikuwa anataka kuzuia mipango ya Mungu ya wokovu wa Mwanadamu, nasi tunawajibu mkubwa wa kufanya kwa kudumu katika sala wakati wote – hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka




Friday, April 8, 2016

NIWAJIBU KUSEMA ASANTE MUNGU




April 8

Warumi 1: 21

Ni tabia nzuri kila siku kuanza chochote kwa kumshukuru Mungu kwa wema wake mwingi  juu ya maisha yetu na mafanikio yetu; Mwenyezi Mungu anatupenda sana pamoja na mapungufu yetu yote.  Tafakari ya leo inatukumbusha kuendelea kuomba neema ya kujishusha na kuendelea kuomba huruma ya Mungu. Wema wa mungu kwetu ni wa ajabu sana kwani ametusamehe dhambi zetu zote; ametubariki kupita ufahamu wetu; japo tumekumbolewa katika dambi lakini bado sisi tumekuwa wagumu na tunaendelea kutembea katika dunia iliyo jaa dhambi; Mungu anajua khali za roho zetu, anajua vishawishi vyote tunavyokumbana navyo. Lakini bado tunawajibu mkubwa wa kumshukuru kila siku na katika matendo yetu yote.

Tafakari yetu leo inatuongoza vile vile kusoma kutoka katika waraka wa Mtume Paulo 1Watheselonike 5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu; lakini kama hatutakuwa watu wa shukurani katika maisha yetu Mtume Paulo katika waraka wake kwa warumi 1: 28-31 anatuasa kuwa Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.  Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; hasara ya kutomshukuru Mungu kwa wema na mafanikio yetu, hutujengea kiburi na kujiona; hutujengea ukosefu wa upendo miongoni mwetu;

Tukisoma kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati 29:10- 15 tunatuonyesha maana halisi ya kumshukuru Mungu kwani vyote tulivyonavyo viantoka kwake yeye; Kwa hiyo Daudi akamhimidi Bwana, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele.  Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.  Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.  Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu.  Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.  Kwani sisi tu wageni mbele zako, na wasafiri, kama walivyokuwa baba zetu wote; ni kama kivuli siku zetu duniani, wala taraji ya kukaa hapana.

Tafakari yetu leo hii inaelekeza kuwa ni tendo la shukrani kwa Mungu huongeza zaidi Baraka tukisoma Injili ya Luka 17:12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,  wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!  Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.  Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;  akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.  Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?  Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?  Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa. 

Tunapomshukuru Mungu tunadhihirishia ulimwengu kuwa Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba; katika ukuu wake ndio kimbilio langu; na nina kila sababu  ya   kumshukuru kati ya mataifa, na kuendelea kuliimba jina lake la shukrani wakati wote.

Tuhitimishe Tafakari yetu kwa ujumbe huu mzito kuwa Kushukuru sio jambo rahisi, na daima kitendo cha kushukuru kinatoka kwenye moyo wa mwamini wa kweli ambaye daima anampa sifa yesu za ushindi katika kila jambo na sio kujipa sifa yeye mwenyewe Warumi 1: 21 kwa sababu walipomjua Mungu wala hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Tuatakiwa kujawa na Roho mtakatifu daima, kwani bila nguvu ya Roho wa Bwana hatuwezi kuwa watu wa shukrani daima. Najua tunajisahau san asana katika kutoa asante kwa Mungu wakati wote; Je tunafanya hivyo? Je unawakumbuka wana wa Israeli pamoja na kutolewa katika utumwa Misri bado walikuwa sio watu wa shukrani; walijawa na malalamishi na dhihaka juu ya Mungu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo - Amina

Emmanuel Turuka