WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, April 5, 2016

KICHEKO BORA KIMEJAA IMANI - FURAHA YAKE NI YA MILELE




April 5

Mwanzo 18:9 -15

Tafakari ya leo tuangalie jinsi imani inavyotuwezesha kutuletea kicheko; na kicheko cha imani ni kicheko chenye ushindi mkubwa sana; kwani kinakuwa kimejaa matumaini ya Mungu yaliyojaa ukamilifu wa ahadi yake kwako; ni kicheko ambacho kitadumu katika maisha yako yote; Tukisoma Hadithi ya Abraham alivyotembelewa na wageni watatu kitabu cha Mwanzo 18:9 -14 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.  Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.  Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.  Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?  Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?  Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.  Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka. 

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa pamoja na kicheko cha matumaini lakini Sara aliguna na kuwa na mashaka juu ya uwezo wake wa kuzaa akiangalia ukuu wa umri wake akiwa amesahau kuwa ahadi yiho ilikuwa imetolewa na Mungu katika umbo la kibinadamu kama wageni ambao walitembelea nyumba yao. Sara bado anatuwakilisha sisi binadamu pamoja na  furaha kubwa ya imani ambayo mungu huwa tayari ametuandalia ili tuweze kuifurahia bado hatuwezi kucheka au kuifurahia bila kuwa na mashaka katika mioyo yetu. Abraham na Sara walipata bahati ya kuwa Mungu alikula nao chakula pamoja nao na kutoa hiyo ahadi nzuri kwa Sara. Tukumbuke kuwa habari njema wakati mwingine hatuzipokei katika ukamilifu wake.

Katika maisha yetu tunapopata habari nzuri ambazo tunatakiwa tuzipokea kwa furaha kwa imani yetu sisi tunakuwa mbali na Mungu na kuanza kuwaza kibinadamu zaidi nakuona kuwa hili haliwezekani; Ndio haliwezekani katika upeo na maono yetu bali kwa Mungu hakuna linaloshindikana; Tunatakiwa tubadilike na tubadili uelewa na jinsi ambavyo tunavyoamini vitu; Tuweke imani yetu mbele na daima tutacheka kicheko cha ushindi na Bwana. Tukisoma Warumi 4:17 mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. Luka 1:37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. 

Tafakari yetu pili inatuonyesha kuwa Sara pamoja na kuwa na mashaka na maelekezo ya Mungu vile vile alicheka na akijua kuwa hataweza onekana mbele ya macho ya watu; Lakini Mungu aliyaona matendo yake na alimuuliza kwani ulicheaka Sara? Naye kwa woga akajibu sikucheka; Mungu alisisitiza tena kuwa ulichena na kuonyesha wasiwasi moyoni mwako; fundisho kubwa hapa hatuwezi kuficha matendo yetu au mawazo yetu mbele ya uso wa Mungu. Tunatakiwa daima kukiri udhaifu wetu na kufanya toba ya kweli. Ndio maana Mtoto aliyezaliwa aliitwa Isaka maana yake “ Utacheka”

Ni kweli ukiwa na imani utacheka na bwana; katika mwaka mmoja tu Abraham na Sara walipata motto na wote pamoja walicheka na kumshukuru Mungu baada ya miaka mingi ya Sara kuwa Mgumba Bwana ameshusha Baraka zake kwake na kwa familia yake; Tukiwa na imani ya kweli tunaamini katika maono ya kimungu  na tunaondokana na wasiwasi wa kibinadamu; tunaondokana na mashaka ambayo mwisho wake yanatuangamiza. Hata katika shida zetu tunatakiwa tumtumaini Mungu na tucheke na Mungu katika imani ikiwa ni ishara ya ushindi ya shida zetu; tukumbuke kuwa vicheko na furaha daima vinatuonyesha ni Mungu gani ambaye sisi tunamwabudu kwani mungu wetu ni wa upendo; hapendi watu ambao wamejaa mashaka na ukiwa na mashaka wasiwasi huwezi kuwa na furaha. Ndio maana hata Injili ya Bwana wetu Yesu kristo inajulikana ni habari njema kwa watu wote; ni habbari inayoleta matumaini ya kweli; imeleta furaha ya kweli; imeleta wokovu wa kweli na faraja ya kweli kwetu sote.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tunaweza kuwa na shaka kama Sara kufuatia umri wake mkubwa kuweza kupata motto lakini alijua kosa lake na alikiri na Mungu akamsamehe na kasha alipata motto katika kipindi kile kile ambacho aliambiwa ili furaha yake ikamilike. Imani yake ndiyo iliyompa furaha ya kudumu. Najua sasa hivi mimi na wewe tunamashaka makubwa sana kuhusu shida zetu na tunalia na shida zetu, tunafadhaika na shida zetu, tumesahau kuwa tukiwa na imani dhabiti na tukiamini katika nguvu ya msalaba kamwe hatutakiwi kulia tunatakiwa kucheka kama Sara.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kwanza tunatakiwa kutafakari jinsi Mungu alivyotupenda na kutufikisha hapa tulipo leo; tukiweza kulitafakari hili vizuri hatuna haja ya kuwa na mashaka wakati sauti ya Mungu ikiongea nasi tunatakiwa kuamini na hivyo kufurahi kwa ushindi wa kushinda matatizo yetu; Daima vicheko vyetu vinatakiwa view vya ushindi kwa sababu ya Imani yetu katika uwezo wa Mungu juu yetu; Mungu ni mwaminifu katika ahadi zake; Sara alicheka sana kwa furaha ya Imani baada ya Kumzaa Isaka motto wa ahadi ya Imani; najua Mungu anatufanikisha sana katika masha yetu lakini tulio wengi hatuko kama Sara hatutubu na kumshukuru Mungu na tunajawa na mashaka katika Imani yetu. Hivyo tunakumbushwa leo kuwa ni wakati mzuri wa kutafakari mapito yetu ili vicheko vyetu view vya Imani na vitakavyo dumu milele yote kama tutasikia sauti ya Mungu na kuitii bila mashaka yeyote. Amen

Hii ni tafakari yetu ya Leo


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment