2 Thess. 3:10
March 28
Tafakari ya leo tunaangalia maagizo ya Mtume
Paulo alipokuwa akiwafundisha watu wa Tesolonike kuhuhusu umuhimu wa kufanya
kazi kwa neema ya Mungu na kwa afya zao kama binadamu ambao bado wana mahitaji
yao binafsi. Tunafahamu katika baadhi ya nchi mafundisho haya bibilia
hayafuatwi sana kwani kuna watu ambao kwa makusudi kabisa hawataki kufanya
kazi; na watu hao wanaafya njema, wana akili za kutosha na wanasababu zote za
msingi za kufanya kazi bali hawataki kufanya kazi nab ado serikali zao
zinawahudumia katika kuwasaidia kuwalisha. Lakini Mtume Paulo alitaadharisha
hili mapema sana ili kuondosha tabia ya uvivu miongoni mwa wanajamii ambayo
inaweza kupelekea au jumuia kuwa mtumwa katika jamii husika. Maonyo hayo
yalitokana na uzushi wa dini za uongo, waliokuwa wakitaka kuishi
wakitegemea ndugu zao kaka na dada bila kufanya lolote
Tafakari ya leo inatusisitiza kuwa kama una afya
njema huna sababu ya kutegemea msaada kutoka kwa watu wengine; Mwenye afya
njema anatakiwa asiwe mzigo kwa watu wengine; asiwe tegemezi. Asiwe chanzo cha
mtu mwingine kupata dhambi ya masononeko au hasira katika kumsukuma mtu huyo
kufanya kazi; tunafahamu kuwa familia bora itakuwa vyema kama inaweza
kujitegemea vizuri; Kwa msingi kuwa kazi ni muhimu katika kutunza familia na
katika kuwakuza watoto. Inapendeza kuona kuwa tunaishi kwenye jamii zetu bila
kutegemea wengine, na tunatakiwa kuzingatia mafundisho ya Bibilia kuwa familia
ndio msingi mkubwa wa kazi ; Mafano mzuri tunaupata kutoka familia takatifu
ya Nazaret inaonesha jinsi familia ya Yesu ilikuwa ya wafanyakazi, maana
Yesu mwenyewe aliitwa mtoto wa seremala na hata kuitwa yeye mselemala.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kufanya
kazi kunaleta tija na heshima ya utu na kutambua kuwa umeumbwa kwa
mfano wa Mungu, Hivyo tukumbuke kuwa utafutaji wa ajira ni jukumu kubwa la
binadamu ili kujikuza mwenyewe familia yake na jamii nzima na katika kutimiza
wajibu wetu kama ilivyoelezwa katika bibilia. Tatizo ambalo binadamu wengi
linatukabili ni tumezoea mno kutafutiwa kulalamika kuhusu ugumu wa maisha; hilo
ni tatizo ambalo pia tunalipeleka kwa watoto wetu tunawakuza kwenye huo mfumo
wa kulalamika kila siku! Hivyo hatuwezi kufikia ndoto ya malengo ya mafanikio kwa kushindwa kufanya kazi
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa mafanikio
yoyote yanahitaji bidii kama maandiko yanavyosema kuwa asiye fanya kazi na
asile, 2 wathesalonike 3:10. Maandiko msingi wake uko kwenye mafanikio ambayo
yanatokana na kazi; sote tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili tufikie malengo tuliyojiwekea
ndipo mafanikio yataweza kutokea; Tunatakiwa tumtangulize Mungu mbele ili
malengo yetu ya kufanya kazi kwa bidii yaendelee kupata kibali toka kwa Mungu ili
Mungu awe anatembea na nasi kwa kila jambo na malengo yetu yaweze kutimia; inatupasa
kutenda vile alivyoagiza naye
atakusaidia katika kutupa nguvu ya kutimiza malengo yetu kwani tunajua kuwa Mungu hamtupi mja wake.
Tafakari yetu inaendelea kutukumbusha kuwa tuwapo
kazini sio tu nguvu itumike bali pia akili na kauli zetu ziwe zimejaa hekima
itokayo kwa Mungu . Tukiwa kazini ni
rahisi watu kutamani kuwa na wewe muda wote kwani kinywa chako huneno yaliyo
mema wakati wote. Ukisoma 1Petro 3:10 utaona jinsi Mungu anavyotuagiza kutumia mdomo
au kauli zetu katika kutangaza yaliyo mema kwa kulitangaza neno lake “Kwa
maana,atakaye kupenda maisha na kuona siku njema,azuie ulimi wake usinene
mabaya na midomo yake isiseme hila”. Epuka kula na kunywa kupita kiasi, katika
mchakato wa kutafuta maendeleo kula na kunywa kupita kiasi kunasababisha
kurudisha nyuma maendeleo yako kwani unakuwa unatumia pesa bila sababu za
msingi. Mithali 23:21 “ Kwa maana mlevi na mlafi huingia umasikini na utepetevu
humvika mtu nguo mbovu,” neno la mungu pia linatuasa kula na kunywa kwa kiasi
kwani mlevi na mlafi huishia kwenye umasikini daima mpaka kukosa hata vazi zuri
la kuvaa. Chagua marafiki wenye hekima, kwani marafiki nao wana nafasi kubwa
katika kutafuta maendeleo yako. Marafiki mwenye hekima watakupa njia mbalimbali
za kupata maendeleo. Tukisoma kiatabu cha Matendo 20:35. . “Katika mambo yote
nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge na
kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu jinsi alivyosema mwenyewe, ni heri kutoa
kuliko kupokea,”
Tafakari yetu bado inasisitiza kuwa mafanikio
ya kitu chochote yakupasa kutenda yampendezayo Mungu ili kuwe na mwisho mzuri
tofauti na kutaka mafanikio ya haraka na kuwa na mwisho mbaya. Hivyo Mungu
hapendi watu wavivu. Watu ambao hawajishughulishi; lakini anatak watu ambao
wanajishughulisha kwa kazi ambazo ni halali na zinazompendeza yeye; Hivyo ni
wajibu wetu kufanya kazi kwa bidii huku tukiomba mwongozo na hekima zetu kwa
ajili ya ustawi wetu wenyewe na wa wote wanaotuzunguka.
Hii ndio tafakari yetu ya leo; Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment