WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Saturday, March 5, 2016

ADUI YAKO AKIWA NA NJAA MLISHE NA MNYWESHE;


March 5

Romans 12:20

Tafakari ya leo tunaangalia maadui wa kiroho ni nani katika maisha yetu? Pengine maadui wa kiroho si maadui bali na nani? Ninaposhambuliwa na adui wa kiroho katika maisha yangu ya Kiroho na kuniumiza kwa wakati huo huo wananisaidia kupata neema ya uvumilivu kutoka kwa Mungu. Tukisoma Mithali 27: 6 Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa adui yetu anaweza kuwa rafiki mzuri wa kiroho kwani kwa maumivu ambayo atakupatia yanaweza kukupa wewe saburi katika maisha yako ya kiroho, anaweza kuwa msaada mkubwa kwa wewe kuanza kujitathimini na kuwa karibu zaidi na Mungu kwa maumivu yake kwako. Ndio maana yesu alitufundisha tuwapenda adui wetu. Tukisoma Luka 6:27 lakini nawaambia ninyi mnaosikia, wapendeni adui zenu watendeeni mema wale ambao wanawachukia ninyi. Ni kweli kabisa ni rahisi kusoma kuliko kutenda hasa ukiwa katikati ya mtafaruku au maumivu yanayosababishwa na adui. Nafahamu kabisa haingii akilini kumpenda mtu ambaye ameharibu maisha yako, je unaanzaje kusali na kumwombea mtu wa aina hiyo? Ni swali gumu katika upeo wa kibinadamu lakini kwa neema ya Mungu hakuna kinachoshindikana. Tukumbuke katika safari ya kiroho hatuwezi kulikwepa hili pamoja na machungu yote, maamuvu yote, tabu zote alizosababisha bibilia inatukumsha kuwa hatutakuwa hurumpaka tumewapenda adui zetu na Mwenyezi Mungu atatubariki.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa yatupasa kuwasalimia kwa upendo tunapokutana nao bila kuwakimbia kuwaonyesha upendo wa Kristo katika uso wako na matendo yako; tunapaswa kuongea nao vizuri kwa kuondoa hasira na kiburi na chuki ambayo tunayo kama sehemu ya kulipiza kisasi. Tunatakiwa kuyakubali maumivu ambayo wamesababisha na kuendelea kuomba neema ya mungu ili kuleta upatanishi wa kweli. Kwa kufanya hivyo tutakuwa sehemu ya uponyaji wa maaumivu yetu . lakini wewe au mimi tunatatkiwa kuwa watekelezaji wa kwanza kwa kuondoa daraja la chuki miongoni mwenu.

Tukisoma Luka 6: 28 tunakumbushwa kuwa wabarikieni wale wote ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wanawaonea ninyi. Tunakumbushwa hatuna sababu ya kuwasemea vibaya wale wote waliowaumiza tukumbuke kuwa kila wakati tunapofungua mdomo mithali 18:21 mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; na wao waupendao watakula matunda yake. Hivyo tunatakiwa kuomba neema ya msamaha na kupunguza kusema tena na tena jinsi ulivyoumizwa kwani kwa kuendelea kusema inaleta wakati mgumu wa kusamehe maumivu yaliyotokea.

Madui ambao nawaongelea leo ni wale watu ambao daima tupo pamoja, tunaonana kila siku, tunafanya kazi pamoja, tunasali pamoja na pengine tunaishi  karibu na tayari tumeshajiwekea ukaribu na undugu ambao unazidi urafiki wa kawaida. Ni wale watu ambao tayari umeshawaamini sana ndio daima wanaokuangusha na kukuumiza; watu unao wapenda sana wamaweza kuwa ndio sababu ya anguko lako; marafiki ambao wanaweza geuka kuwa maadui ni kama watoto wako, wazazi wako, mume au mke wako;

Tafakari ya leo inatuonyesha ugumu wa kutekeleza hili kwani tunatakiwa kuwapenda japo wametuumiza kwa kiwango chochote kile wanaweza wakawa wametunyanyasa, wametutesa, na kutuumiza kwa msingi wowote ule ambao umesababisha kuharibu kabisa mwenendo wa maisha na imani pia. Lakini Bado yesu anatilia mkazo Mpende adui yako. Tatizo amri hii haiepukiki kwani hii ni hatua pekee kuelekea kwenye msamaha. Hatuwezi kubarikiwa mpaka tumewasamehe waliotuumiza. Romans 12: 20 – 21 aduia yako akiwa na njaa mlishe akiwa na kiu mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema

Tafakari ya leo inatuasa kuwa tuondoe mawazo mabaya katika mioyo yetu, hakuna sababu ya kuwa na mawazo mabaya mioyoni mwetu juu ya wengine, hata kama wewe sio muuaji lakini una mawazo mabaya ya chuki ndani ya nafsi yako juu ya mwenzako ni sawa tu na kuua. Kama wewe sio mzinzi lakini unamawazo machafu moyoni mwako yenye mwelekeo huo ni sawa tu ma kuzini. Tunakumbusha kuwa uadui miongoni mwetu na kuumizana ni kwa sababu tu ya tabia zetu mbaya ambazo husababishwa na mawazo mabaya ya ubinafsi. Wivu, choyo, hasira na kutokuwa na hofu ya Mungu.

Kwa hiyo kuwapenda adui zetu haitulazimu sisi kufanya vile wanavyofanya kwetu, bali kuwaonyesha upendo, kuwaonyesha msamahaa wa makosa yao; sio lazima tukubaliane nao katika hoja zao lakini kuonyesha upendo katika majadialaino nao kuwapa maelekezo kulingana na mwongozo wa Mungu. Adui siku zote ana chuki na anataka akuone wewe unashindwa, unaanguka , unaaibika; wanapenda kusambaza sumu uchukiwe, ulipize kisasi na kadhalika. 

Tafakari yetu inaonyesha lengo la adui kuwa wewe uchukiwe na. Hivyo yesu anatukumbusha kuwa tunaweza kusikitika juu yao au kukasirika kwa matendo yao lakini bado tunatakiwa kuwapenda. Mithali 25: 21 -22 Adui yako akiwa ana njaa mpe chakula; tena akiwa ana kiu mpe maji ya kunywa. Maana utatia makaa ya moto kichwani pake, na bwana atakupa thawabu.

Hii ni tafakari yetu ya leo – AMINA


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment