WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, March 31, 2016

WAKATI WA SHIDA ZETU TUNAONA UTUKUFU WA MUNGU?





March 31

Yohana 3:20  

Kwa nini tunamkimbia Mungu Tafakari ya leo inatupa jibu rahisi sana kwa nini  tunamkimbia Mungu, tunamkimbia Mungu kwa sababu sisi binadamu tunataka kufanya au kuendelea kuishi katika misha ya dhambi ambayo yako kinyume na maagizo yake; Yohana 3:20  kwa kuwa kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.   

Tafakari ya leo inatueleza sababu nyingine ambayo tunamkimbia Mungu ni kwa sababu ya Machungu tunayo yapata katika maisha yetu kwa sababu tunaona Mungu hana msaada kwetu kutokana na maisha ambayo tunaishi na tabu zote ambazo ziko mbele yetu. Sasa Mungu yuko wapi? Kwa nini amekubali mimi nipate shida zote hizi.

Tafakari inatuongoza kuwa pamoja na yote yanayotokea katika maisha yetu; Lakini bado tunatakiwa kumpa sifa Mungu pamoja na mateso au shida zozote zile kama tunavyosoma katika zaburi 107:1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele; bado tunatakiwa kushukuru wema wa Mungu na sio kumkimbia au kukata tamaa katika majaribu yetu;

Tafakari yetu ya leo inatukumusha kuwa tunamkimbia mungu  kutoka na maisha au mazingira ambayo yanatuzunguka leo hii; 1Peter 5:7 na tumesahau kuwa sisi tumeumbwa katika ulimwengu huu ili mwenyezi Mungu atupime namna gani tunaendelea kumshukuru na kumsifu pamoja na shida zote zinazotuzunguka. Tumepewa akili na uhuru tuutumie tutakavyo lakini bado tunawajibu wa kujaribiwa katika yale ambayo tunayoyafanya; Mungu ameshatoa maelekezo ya nini tufanye na nini tusifanye? Mathayo 10:28 msiwaogope  wauao mwil, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni Yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum

Lakini sisi binadamu tunakuwa na tabia ya kiburi na kuchagua kutenda yale tupendeya ambayo hayampendezi Mungu na hivyo kujiwekea sifa ya Kumkimbia. Waebrania 11:6 lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko , na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao. Tukisoma waraka wa 1 Peter 1:7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima katika kufunuliwa kwake yesu Krsito. sehemu hii ya bibilia inatuonya kuwa hatuna sababu ya kukimbia na kumkimbia Mungu;

Tafari ya leo inatuunganisha vile vile na kisa cha Yona alikimbia wito wa Mungu na akafikiri kuwa amefanikiwa kumbe sio kweli; Tukijua kuwa Mungu ni Alpha na Omega kuwa yeye huishi nyakati zote, na kwa msingi huu kamwe  hatuwezi kuukimbia uso wa Mungu hata kama tutakuwa wanjanja kama nini: mara nyingi tunawaogopa wanaua mwili; tunawaheshima na kuwanyeyekea lakini tunamdharau au kumpuza yule ambaye anao uwezo wa kuua Roho kwa vile hatumwoni kwa Macho hivyo tunafikiri kuwa ni rahisi kumkimbia;

Tafakari yetu vile vile inatukumbusha Maisha ya  ya Mtume Paulo wakati ule akiwa anaitwa Saulo njinsi alivyokuwa mkatiri na muuaji mkubwa wa watu wa Mungu. Matendo ya Mitume 9:3-5 hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini akasikia sauti ikimwambia Sauli Sauli mbona waniudhi? Akasema u nani wewe Bwana? Naye akajibu mimi ndiye Yesu unayeniudhi wewe. Paulo kwa matendo yake mabaya alikuwa anaukimbia uso wa Mungu kwa mauvo yake kwa kutenda vitu ambavyo vilikuwa kinyume na maagizo ya Mumgu.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa hatuwezi kumkimbia Mungu kwa kiburi chetu, majivuno, utajiri, chuki  au kuwafanyia maangamizo watu wa Mungu; kinachotokea tunajiangamiza wenyewe, kwa matendo yetu. Ni bora tuachane na tabia hizi mbaya na kumrudia Mungu kwani Mungu ni rafiki wa kweli anayetupenda sana, na anatamani sana kututuma kwenda kufanya kazi yake katika shamba lake. Amina


Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment