WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, March 7, 2016

JE UNAZITUMIAJE KARAMA ZAKO ZA KIRIHO?


March 7

1 WAKORINTHO 12: 1

Tafakari ya leo tunaangalia jinsi ambavyo tumejaliwa karama nyingi za kiroho na utumiaji wetu; Mtume Paulo anatutabanaisha kupitia waraka kwa Warumi 1:11-12 kuwa natamani sana kuwaona  nipate kuwapa karama ya rohoni, ili mfanwe imara. Yaani tufarajiane mimi na ninyi kila mtu kwa imani ya mwenzake, yenu na yangu. Kwa ujumbe huu kutoka kwa Mtume paulo karama ya kiroho  kazi yake ya kwanza ni kuwaimarisha wengine. Je karama yako inasaidiaje uimarishaji wa imani  ya mtu mwingine? Huluka ya ubinadamu wetu uko zaidi katika kubomoa na sio katika kujenga au kusaidia wengine.

Tafakari ya leo inatuuliza karama ni nini? Tukisoma 1 Wakoritho 7 inatufafanulia kuwa karama ni ufunuo wa Roho; Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. Ni kitu ambacho Roho ukiweka wazi; kinangara katika maisha yako na wengine, ni ufunuo ambao umejaliwa kwa ufupi nu ushuhuda ambao Roho ameufunua kwako kuwa yeye anafanya kazi ndani ya Mwili wako ili kutenda mema au kuleta amani ambayo Mungu amekusudia.

Tunafurahia sana kuwa sehemu ya walalamikaji, wachonganishi, wambea, kuhukumu kuliko kuwa tayari kujenga mahusiano mazuri miongoni mwetu. Kipimo kikubwa kabisa cha karama ya kiroho, ni unyenyekevu na kuwa tayari tuamkapo asubuhi  kumshukuru mungu kwa kuimarisha karama yako na kuitendea kazi nzuri kama ipasavyo kutumika.

Kama waraka kwa Wagalatia 3:5 basi  yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa  kusikia kunakotokana na imani? Waroma 12: 6- 8 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani; ikiwa huduma tuwemo katikahuduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; mwenye kuonya katika kuonya kwake; mwenye kusimamia kwa bidii, mwenye kusimamia kwa bidii,mwenye kurehemu, kwa furaha. Sifa za Mkristo.

Tukumbuke  Musa alivyowaambia wana wa Israeli kwenye kitabu cha kumukumbu la sheria 8:17 hapo usisema moyoni mwako nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulio nipatia utajiri huo. Musa anatuambia kuwa tusiwe na tabia za kujisufu wenyewe kwa mafanikio ambayo yana nguvu na mkono wa mungu kupitia karama zake kwetu. Jukumu letu la msingi kwa karama ambayo umejaliwa unatakiwa kwanza uitumie kwa aji li ya utukufu wa Mungu, na kama tutaweza kuzitumia karama zetu vizuri katika jamii yetu na nafasi  ambazo tumepewandani ya jamii yetu, basi tusitegemee kuwa na viongozi wabadhilifu wala rushwa au wazembe; kwani Miongozo ya  mungu iko wazi kwetu ni ya uadilifu  na upendo wa ajabu kwetu wenyewe na kwa jamii yetu nzima.

Tunasoma kutoka 1Peter 4-10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama utumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema balimbali za Mungu.  Mtu akisema na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata  milele na milele. Amina

Karama ambazo mwenyezi Mungu ametujali ziko katika utumishi mbalimbalikama unabii Waroma 12:6  basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii tutoe unabii kadiri ya imani kwa kuwajenga kuwafariji na kuwatia Moyo. Karama ya huduma kama waraka wa waroma 12:7 unavyotufundisha kuwa  ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake.

Karama ya kufundisha naye aitoa wengi kuwa mitume na wengine kuwa manabii na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu. Swali ambao mtume pauloali uliza kuwa je wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote watenda miujiza? Karama ya kufundishi ni muhimu kwa vile inaeleza kwa ukweli na uwazi kuhusu ukweli kuhusu Mungu ili kuwasaidia wengine kujifunza pia. Karama ya kutoa ni uwezo wa kutoa kwa moyo na kwa upendo kwa sifa na utukufu wa mungu kwa wale wote ambao wana shida na uhitaji.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa karama yako ndio ufunguo wa mafanikio yako; na tunapotumia karama zetu kwa utaratibu ambao Mungu ametujalia sio tu kuwa ulimwengu utafurahia bali neema itarudi kwako. 1 Timotheo 4: 14-15 usiache kuitumia Karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu. Tukumbuke kuwa Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. Ni zawadi toka kwa mungu kwako la msingi tunatakiwa kutambua je ni karama gani Mungu amekujalia?

Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia 3:5  unatufafanulia vizuri sana kuwa Bais, kama yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je Anafanyahayo kwa matendo ya sheria au kusikia kutokana na imani? Miujiza ambayo hufanyika katika imani hudumisha na ukuza imani yaw engine ndilo jambo ambalo karama hutenda. Je karama yako unaitumiaje? Je unaijua Karama yako kwa kazi ya Mungu. Je unaweza kuomba Mungu akuonyeshe Karama yak oleo ili utende kazi ya kuimarisha imani ya watu wengine? Na kwa kufanya hivyo tutaweza kumtukuza Mungu kupitia Bwana wetu yesu kristo ambaye yeye alituonyesha kwa matendo namna ya kutumia Karama hizi kwa sifa na utukufu wa Mungu. 

Tumwombe leo Mungu atufulie karama zetu kuptia roho Mtakatifu ili tuweze kutekeleza wajibu wetu kwa kuimarisha imani yetu na kwa wenzetu, tukijua kuwa Pamoja naye; katia yake  and ndani yake hakuna kinachoshindikana tukijua kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uwezo wake, tena vinarejea kwake. Utukufu unayeye milele na milele amina.

Hii ndio tafakari yetu ya leo. AMINA




No comments:

Post a Comment