WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, March 11, 2016

JE TUNAZITUMIAJE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI;




March 11

MATHAYO 16:19

Tafakari Ya leo inalenga kuonyesha jinsi ambavyo sisi wana wa Adamu tumekabidhiwa funguo za uzima wa milele. Ni zawadi ya pekee sana kwetu kuaminiwa na kukabidhiwa funguo hizi ambazo ni muhimu sana katika safari yetu ya kuelekea kwenye maisha yetu ya baadae; funguo unakupa uwezo, nguvu ya kuingia sehemu ambayo imefungwa au kufunga ili mtu mwingine mwenye nia mbaya asiweze ingia katika nyumba hiyo. Isaya 22:22 anasema kuwa Na ufunguo wa Nyumba ya Daudi nitauweka begani mwake; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.

Tafakari ya leo inatuonyesha kuwa funguo ni Nguvu, ni mamlaka, ni upako kwa sisi wakristo inawakilisha ni nguvu au uwezo ambao Mungu anatujalia sisi binadamu, na inapatikana kwa kila mtu aliyeelewa umuhimu na kuwa tayari  kuzitumia funguo hizo kwa maisha ya Mbinguni. Mwenjili Mathayo anaweka wazi tukisoma Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa Mbinguni; na lolote utakalo lifunga duniani; litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Kwa ujumbe huu tumepewa kibali cha kufanya maamuzi.

Yesu alitoa kibali hiki kwa Peter, kibali ambacho Peter  aliwapa mitume na wafuasi wote na hivyo hivyo kibali hicho kimeruhusiwa kwa wakristo wote ambao wako tayari kutumia nguvu na mamlaka ya funguo na ambao wako tayari kuzitumia. Hata tukisoma Injili ya John 20: 21-23 Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi name nawapeleka ninyi. Naye akisha kusema hayo akawavuvia, akawaambia pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaofungia dhambi wamefungiwa. Wow kweli tumepewa nguvu za ajabu lakini hatujui jinsi ya kuzitumia.

Tafakari ya leo tunavyoendelea na mfungo wa siku arobaini kuelekea siku ya ufufuo ambayo ndio siku maalumu ya mwokozi wetu alipounyesha ulimwengu kuwa yeye ni mbarikiwa wa baba tuna kila sababu ya kusifu na kushangilia. Huku tukijitathimini wenyewe jinsi ambavyo tunanashindwa kuzitumia vizuri funguo za uzima ambazo tumepewa. Yesu aliliona tatizo hili tukisoma Luka 11:52 Ole wenu ninyi wanasheria kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.

Yesu anawaonya wanasheria walikuwa wanatumia vibaya neema na maarifa ya funguo kwa kuto wafundisha watu wengine jinsi ya kutumia funguo za mbinguni ili waweze kufurahi neema ya maisha ya baadae hivyo wao wamekalia neema hiyo kwa faida yao pekee. Mathayo 13: 52 Akawambia, kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.

Funguo ambazo tumepewa zina nguvu sana ambazo zinaweza kufungua hazina na kutoa humo vitu vya thamani kubwa katika maisha ya Kiroho; katika imani funguo ambazo tumepewa ni za kufungua nguvu na uwezo wa Roho Mtakatifu juu ya maisha yetu.
Tafakari ya leo inatuonyesha nini faidia ya kuweza kupata elimu ya kutumia funguo za mbinguni? Funguo ambazo tumezipata tunaweza kuzieleza matumizi yake kama ifuatavyo: Unaweza kuziweka pembeni uzizitumie;  unaweza kuzibeba katika mifuko yako hivyo wakati unapotaka kuzitumia unakuwa na kazi ya kuzitafuta; na unaweza zivaa shingoni na ukapata urahisi wa kuzitumia.

Tatizo la kuzivaa funguo hizo shingoni ni ushahidi kuwa kila mtu ataziona na shetani atakuwa anakushawishi uzivue au uweke mahali ambapo hapaonekani mbele ya Macho ya dunia. Kama wakristo tunatakiwa tuone fahari ya kuzivaa na kuzitumia bila woga wowote. Je unaona aibu kusoma bibilia mbele ya yatu? Au kumtangaza Kristo mbele ya watu? Tukumbuke kuwa pale tunapovaa funguo zetu shingoni kunatupa sisi ujasili wa khali ya juu kuwa wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo. Na uko tayari kumpigania wakati wote.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumtoa mwanae yesu kristo ambaye alitufundisha kuhusu funguo za uzima wa milele, na Baraka zitokanazo na funguo hizo na ametusistiza kuwa lazima tuwe watu wa kuomba msamaha na kusamehe ili tuweze kuzitumia vyema funguo hizi .

Hii nitafakari yetu ya leo Amen

Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment