WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, March 31, 2016

WAKATI WA SHIDA ZETU TUNAONA UTUKUFU WA MUNGU?





March 31

Yohana 3:20  

Kwa nini tunamkimbia Mungu Tafakari ya leo inatupa jibu rahisi sana kwa nini  tunamkimbia Mungu, tunamkimbia Mungu kwa sababu sisi binadamu tunataka kufanya au kuendelea kuishi katika misha ya dhambi ambayo yako kinyume na maagizo yake; Yohana 3:20  kwa kuwa kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.   

Tafakari ya leo inatueleza sababu nyingine ambayo tunamkimbia Mungu ni kwa sababu ya Machungu tunayo yapata katika maisha yetu kwa sababu tunaona Mungu hana msaada kwetu kutokana na maisha ambayo tunaishi na tabu zote ambazo ziko mbele yetu. Sasa Mungu yuko wapi? Kwa nini amekubali mimi nipate shida zote hizi.

Tafakari inatuongoza kuwa pamoja na yote yanayotokea katika maisha yetu; Lakini bado tunatakiwa kumpa sifa Mungu pamoja na mateso au shida zozote zile kama tunavyosoma katika zaburi 107:1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele; bado tunatakiwa kushukuru wema wa Mungu na sio kumkimbia au kukata tamaa katika majaribu yetu;

Tafakari yetu ya leo inatukumusha kuwa tunamkimbia mungu  kutoka na maisha au mazingira ambayo yanatuzunguka leo hii; 1Peter 5:7 na tumesahau kuwa sisi tumeumbwa katika ulimwengu huu ili mwenyezi Mungu atupime namna gani tunaendelea kumshukuru na kumsifu pamoja na shida zote zinazotuzunguka. Tumepewa akili na uhuru tuutumie tutakavyo lakini bado tunawajibu wa kujaribiwa katika yale ambayo tunayoyafanya; Mungu ameshatoa maelekezo ya nini tufanye na nini tusifanye? Mathayo 10:28 msiwaogope  wauao mwil, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni Yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum

Lakini sisi binadamu tunakuwa na tabia ya kiburi na kuchagua kutenda yale tupendeya ambayo hayampendezi Mungu na hivyo kujiwekea sifa ya Kumkimbia. Waebrania 11:6 lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko , na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao. Tukisoma waraka wa 1 Peter 1:7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima katika kufunuliwa kwake yesu Krsito. sehemu hii ya bibilia inatuonya kuwa hatuna sababu ya kukimbia na kumkimbia Mungu;

Tafari ya leo inatuunganisha vile vile na kisa cha Yona alikimbia wito wa Mungu na akafikiri kuwa amefanikiwa kumbe sio kweli; Tukijua kuwa Mungu ni Alpha na Omega kuwa yeye huishi nyakati zote, na kwa msingi huu kamwe  hatuwezi kuukimbia uso wa Mungu hata kama tutakuwa wanjanja kama nini: mara nyingi tunawaogopa wanaua mwili; tunawaheshima na kuwanyeyekea lakini tunamdharau au kumpuza yule ambaye anao uwezo wa kuua Roho kwa vile hatumwoni kwa Macho hivyo tunafikiri kuwa ni rahisi kumkimbia;

Tafakari yetu vile vile inatukumbusha Maisha ya  ya Mtume Paulo wakati ule akiwa anaitwa Saulo njinsi alivyokuwa mkatiri na muuaji mkubwa wa watu wa Mungu. Matendo ya Mitume 9:3-5 hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini akasikia sauti ikimwambia Sauli Sauli mbona waniudhi? Akasema u nani wewe Bwana? Naye akajibu mimi ndiye Yesu unayeniudhi wewe. Paulo kwa matendo yake mabaya alikuwa anaukimbia uso wa Mungu kwa mauvo yake kwa kutenda vitu ambavyo vilikuwa kinyume na maagizo ya Mumgu.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa hatuwezi kumkimbia Mungu kwa kiburi chetu, majivuno, utajiri, chuki  au kuwafanyia maangamizo watu wa Mungu; kinachotokea tunajiangamiza wenyewe, kwa matendo yetu. Ni bora tuachane na tabia hizi mbaya na kumrudia Mungu kwani Mungu ni rafiki wa kweli anayetupenda sana, na anatamani sana kututuma kwenda kufanya kazi yake katika shamba lake. Amina


Emmanuel Turuka




ASANTE YESU

March 30

Tafakari ya leo tunatakiwa kila iitwayo leo tumshukuru na kusema Asante yesu kwani ametuweka huru, ametuletea amani, ametuondolea zigo la dhambi na ametufungulia na kutusafishia njia ya kwenda mbinguni kwa baba ili tuweze kushiriki karamu katika ufalme ule wa milele bila vikwazo.

Ni jukumu letu kuendelea kujiandaa kwa safari hiyo muhimu. Basi karibu tutafakari wote pamoja




Wednesday, March 30, 2016

YESU AMEFUFUKA - NA AFUFUKE MOYONI MWAKO

March 29

Tafakari ya leo tuendelea kushangilia ushindi wa ufufuo wa mwokozi wetu. Jukume letu basi afufuke kweli kweli moyoni mwetu kwa kuishi na kutenda vile alivyotufundisha. Swali la msingi je tunaipokeaje zawadi hii kubwa ya Damu yake msalabani?

Hii ni tafakari yetu ya leo Amina


Tuesday, March 29, 2016

ASIYE FANYA KAZI NA ASILE


2 Thess. 3:10

March 28

Tafakari ya leo tunaangalia maagizo ya Mtume Paulo alipokuwa akiwafundisha watu wa Tesolonike kuhuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa neema ya Mungu na kwa afya zao kama binadamu ambao bado wana mahitaji yao binafsi. Tunafahamu katika baadhi ya nchi mafundisho haya bibilia hayafuatwi sana kwani kuna watu ambao kwa makusudi kabisa hawataki kufanya kazi; na watu hao wanaafya njema, wana akili za kutosha na wanasababu zote za msingi za kufanya kazi bali hawataki kufanya kazi nab ado serikali zao zinawahudumia katika kuwasaidia kuwalisha. Lakini Mtume Paulo alitaadharisha hili mapema sana ili kuondosha tabia ya uvivu miongoni mwa wanajamii ambayo inaweza kupelekea au jumuia kuwa mtumwa katika jamii husika. Maonyo hayo yalitokana na uzushi wa dini za uongo,  waliokuwa wakitaka kuishi wakitegemea ndugu zao kaka na dada bila kufanya lolote

Tafakari ya leo inatusisitiza kuwa kama una afya njema huna sababu ya kutegemea msaada kutoka kwa watu wengine; Mwenye afya njema anatakiwa asiwe mzigo kwa watu wengine; asiwe tegemezi. Asiwe chanzo cha mtu mwingine kupata dhambi ya masononeko au hasira katika kumsukuma mtu huyo kufanya kazi; tunafahamu kuwa familia bora itakuwa vyema kama inaweza kujitegemea vizuri; Kwa msingi kuwa kazi ni muhimu katika kutunza familia na katika kuwakuza watoto. Inapendeza kuona kuwa tunaishi kwenye jamii zetu bila  kutegemea wengine, na tunatakiwa kuzingatia mafundisho ya Bibilia kuwa familia ndio msingi mkubwa wa kazi ; Mafano mzuri tunaupata kutoka familia takatifu  ya Nazaret inaonesha jinsi familia ya Yesu ilikuwa ya wafanyakazi, maana Yesu mwenyewe aliitwa mtoto wa seremala na hata kuitwa yeye  mselemala.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa  kufanya kazi kunaleta tija na heshima ya utu na  kutambua  kuwa umeumbwa kwa mfano wa Mungu, Hivyo tukumbuke kuwa utafutaji wa ajira ni jukumu kubwa la binadamu ili kujikuza mwenyewe familia yake na jamii nzima na katika kutimiza wajibu wetu kama ilivyoelezwa katika bibilia. Tatizo ambalo binadamu wengi linatukabili ni tumezoea mno kutafutiwa kulalamika kuhusu ugumu wa maisha; hilo ni tatizo ambalo pia tunalipeleka kwa watoto wetu tunawakuza kwenye huo mfumo wa kulalamika kila siku! Hivyo hatuwezi kufikia ndoto  ya malengo ya mafanikio kwa  kushindwa kufanya kazi

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa mafanikio yoyote yanahitaji bidii kama maandiko yanavyosema kuwa asiye fanya kazi na asile, 2 wathesalonike 3:10. Maandiko msingi wake uko kwenye mafanikio ambayo yanatokana na kazi; sote tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili tufikie malengo tuliyojiwekea ndipo mafanikio yataweza kutokea; Tunatakiwa tumtangulize Mungu mbele ili malengo yetu ya kufanya kazi kwa bidii yaendelee kupata kibali toka kwa Mungu ili Mungu awe anatembea na nasi kwa kila jambo na malengo yetu yaweze kutimia; inatupasa kutenda vile alivyoagiza  naye atakusaidia katika kutupa nguvu ya kutimiza malengo yetu kwani tunajua kuwa  Mungu hamtupi mja wake.

Tafakari yetu inaendelea kutukumbusha kuwa tuwapo kazini sio tu nguvu itumike bali pia akili na kauli zetu ziwe zimejaa hekima itokayo kwa Mungu . Tukiwa  kazini ni rahisi watu kutamani kuwa na wewe muda wote kwani kinywa chako huneno yaliyo mema wakati wote. Ukisoma 1Petro 3:10 utaona jinsi Mungu anavyotuagiza kutumia mdomo au kauli zetu katika kutangaza yaliyo mema kwa kulitangaza neno lake “Kwa maana,atakaye kupenda maisha na kuona siku njema,azuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isiseme hila”. Epuka kula na kunywa kupita kiasi, katika mchakato wa kutafuta maendeleo kula na kunywa kupita kiasi kunasababisha kurudisha nyuma maendeleo yako kwani unakuwa unatumia pesa bila sababu za msingi. Mithali 23:21 “ Kwa maana mlevi na mlafi huingia umasikini na utepetevu humvika mtu nguo mbovu,” neno la mungu pia linatuasa kula na kunywa kwa kiasi kwani mlevi na mlafi huishia kwenye umasikini daima mpaka kukosa hata vazi zuri la kuvaa. Chagua marafiki wenye hekima, kwani marafiki nao wana nafasi kubwa katika kutafuta maendeleo yako. Marafiki mwenye hekima watakupa njia mbalimbali za kupata maendeleo. Tukisoma kiatabu cha Matendo 20:35. . “Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu jinsi alivyosema mwenyewe, ni heri kutoa kuliko kupokea,”

Tafakari yetu bado inasisitiza kuwa mafanikio ya kitu chochote yakupasa kutenda yampendezayo Mungu ili kuwe na mwisho mzuri tofauti na kutaka mafanikio ya haraka na kuwa na mwisho mbaya. Hivyo Mungu hapendi watu wavivu. Watu ambao hawajishughulishi; lakini anatak watu ambao wanajishughulisha kwa kazi ambazo ni halali na zinazompendeza yeye; Hivyo ni wajibu wetu kufanya kazi kwa bidii huku tukiomba mwongozo na hekima zetu kwa ajili ya ustawi wetu wenyewe na wa wote wanaotuzunguka.
Hii ndio tafakari yetu ya leo; Amina

Emmanuel Turuka



Sunday, March 27, 2016

KRISTO AMEFUFUKA KWELI KWELI

March 27

Tafakari ya leo tunashagilia ushindi na ufufuo wa Mwokozi wetu kwa nyimbo leo ni siku ya furaha tuna kila sababu ya kuishangilia na kumsujudia kwa ukombozi wake hapa duniani; ni kazi ngumu na aliimaliza kwa mateso makubwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu amina;





Amina

ALELUYA KUU- TUNA KILA SABABU YA KUSHANGILIA

MARCH 26

Tafakari ya leo tukiwatunaendela kusherekea sikukuu ya Pasaka; tunamwimbia Mungu aleluya ya ushindi ambao tumeupata kupitia yeye kwa damu yake takatifu. Asante Bwana wetu Yesu kristo kwa upendo wako juu yetu na kutufungua michochoro ya dhambi ambayo tulikuwa tumefungwa kwa muda mredu katokana na dhambi ya kiburi ambayo ilifanyika katika bustani ya Adeni amina.

Friday, March 25, 2016

BABA YAMETIMIA; MIKONONI MWAKO NAIWEKA ROHO YANGU.



John 19:28-30

Leo ni Ijumaa kuu ni siku muhimu sana katika ukombozi wetu; ni siku muhimu sana katika safari ya usindi wa ukombozi wa maisha yetu kama wakristo ambao tegemeo la ukombozi wetu liko mikononi mwa Bwana wetu yesu kristo; ni siku ambayo Yesu alisulubiwa msalabani kwa dhambi zetu. Ni siku ambayo maadui wake walijua kuwa tayari wameshinda vita ya kumwangamiza baada ya kumtesa na kumdhihaki katika kipindi chote cha mateso na kumsulubisha pale msalabani;

Tafakari yetu leo inatuhamasisha kuwa maadui wa Yesu mafarisayo na wakuu wa sheria walijua wameshinda na wamemwangamiza Yesu kwa kifo cha Msalabani; wakati huo huo wanafunzi wa yesu walikuwa na machungu wasijue nini cha kufanya na walikuwa wamejificha na hawataki kuonekana hadharani; Lakini Yesu baada ya kusulubiwa msalabani na maandiko kutimia aliinua macho mbinguni na kusema yametimia; Ni neno muhimu kwa sababu kunaashiria mwisho mafanikio ya hatua muhimu katika ukombozi wetu. Ni neno hili Yametimia hutumika wakati wa ukamilifu ulio sahihi wa jambo fulani muhimu. Yesu alilitumia neno hili kwa kumaliza kazi ngumu ambayo bwana wake waliompa kufanya , alikuwa akisema kwa bwana - tetelestai - "Mimi kuondokana na matatizo yote ; Nimefanya kazi kwa kadri ya uwezo wangu na nimelaiza salama kwa mafanikio makubwa ya ukombozi wa binadamu. Naamini kuwa hakuna neno nyingine  bora linaloweza kutuonyesha ukuu wa Yesu. 

Tetelestai maana ya kumaliza, yametimia. Ni mara zote neno hili tunalitumia kama furaha na ushindi; Hapa tunasherekea ushindi wa kuishinda dhambi iliyoingia ulimwenguni kupitia Adamu na Hawa na hitimisho lake ni siku hii ya Leo ya Ijumaa kuu.

Tafakari ya leo inaonyesha kuwa Mungu ni mwenye haki; Yeye pia ni huruma ; Mungu ametoa njia ambayo tumekombolewa kwa damu mbadala ya mwokozi wetu Bwana wetu Yesu Kristo. Mwenyezi Mungu ametupenda ametuamini sisi wana wake kwa kumtoa Yesu kuwa ndio daraja letu la ukombozi: warumi 3: 24-26 wamehesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.

Tafakari yetu leo inatuonyesha jinsi  Mungu alivyotimiza ahadi ya kufanya malipo halisi ; Kwa kumtoa Yesu mbele kama malipo ya dhambi zetu.Yesu amekuwa Kipatanisho chetu na Mungu  kupitia damu yake Takatifu; damu pekee ambayo inaweza kweli kulipia dhambi zetu. Hii ilikuwa ni kuonyesha haki ya Mungu , kwani kwa uvumilivu wake wa Uungu amesafisha dhambi zote  zilizofanywa Kwa kipindi cha muda kirefu toka kuumbwa kwa dunia , kwa sababu Mungu si mwepesi wa hasira na mikopo yake iliyojaa huruma iko juu yetu siku zote; hivyo aliamua kutoa Yesu ambaye alizaliwa kama binadamu awe malipo ya kweli kwa ajili ya dhambi zetu , hii ilikuwa kuonyeshaupendo wake kwetu.

Tafakari yetu tunamshukuru Yesu kwa Kilio chake cha ushindi Yametimia; Kwetu Yesu kufa msalabani ni tendo la ushindi mkubwa sana, kwani alishatueleza kuwa Mwana wa Adamu atapata mateso makali na kufa msalabani kisha aatafufuka kutoka kaburini na hiyo inadhihirisha  uishinda dhambi na mauti. Na tukumbuke kuwa sisi ambao tunaamini kuwa Kwa kusulubiwa kwake Krsito tumepata ushindi mkubwa sana ambao wanaamini, Kristo aliyesulubiwa ni neno la wokovu, ni neno la ushindi. Na maneno ambayo Yeye anaongea hapa ni kelele za ushindi. Kwa macho haya si ushindi kelele. Lakini kwa macho ya imani na tukiendela kushukuru kwani kristo anaishi ndani yetu; hivyo mpango wa Mungu na madhumuni ya maisha yangu sasa yametimia. Njia ya uvumilivu, unyenyekevu kusamehe na kuto shindwa hata katika magumu ndio njia ambayo Mungu anataka sisi kuishi nasi mwisho wa safari hii tuweze kusema kama Yesu alivyosema Msalabani YAMETIMIA;

Leo ni siku Muhimu sana katka maisha yetu kama Mkristo, askari shupavu wa Yesu; hivyo Mungu anataka wewe kukamilisha na kuishi maisha yetu kama kristo alivyoishi duniani; kupigana vita vizuri, na tuweze kumemaliza mbio za kumtafuta Mungu kwa ushindi na kuvikwa taji katika makao ya milele; Kwa ushindi wa Yesu tumeondolewa dhambi zote na tumelipwa kwa ukamilifu;

Hii ndi tafakari yetu ya leo katika Ijumaa hii Kuu ambayo ni muhimu sana katika ukombozi wetu kama Wakristo – Amen


Emmanuel Turuka

Thursday, March 24, 2016

PETRO: BWANA HUTA NIOSHA MIGUU YANGU?

       

Yohana 13: 8


Tafakari ya Leo  tunaangalia msimamo wa Peter alipomwambia Yesu Kuwa Bwana , wewe huta niosha miguu mimi?"  katika maisha ya Bwana wetu Yesu maisha yake pamoja na Mitume wake; Mara zote Peter ameonekana daima alileta kauli au hali tata katika Mambo mengi; ya kukataa au kujichanganya mwenyewe alipokuwa akipewa maelekezo na Yesu au kuulizwa swali; Peter pamoja na kukaa na Yesu bado kabisa alikuwa anatumia zaidi akili yake ya kibinadamu katika mambo mengi;  Tukumbuke Yesu alipowaambia mitume wake Mwana wa Adamu alipokuwa anakwenda Yerusalemu kuteseka na kufa: Peter alijibu nini Kamwe, Bwana! Si wewe!

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tulio wengi tunafikiri kama Petro; tumefunuliwa lakini hatuoni ufunuo wa Mungu kwa ajili ya utukufuwa Mungu; tunataka ufuo ambao tunao bado ufanye kazi katika akili na mazingira ya kibinadamu; kwa maneno mengine tunaishi katika kizazi ambacho kina kiburi; kizazi ambacho hakipo tayari kufuata maelekezo; kizazi ambacho hakipi tayari kumtumikia Mungu kwa kuachana na uchafu wetu wa miguu yetu; na tunapotaka kusaidiwa kuoshwa bado tunapinga na hatuoni umuhimu kwa kupata msaada huo;  bado tumeendelea kuwa kizazi ambacho tunataka kuendelea kujisifu; kizazi ambacho hatuoni umuhimu wa nyenyekevu;

Tafakari ya Alhamis Kuu itukumbushe kuwa tunatakiwa  kujithamini, kujijengea upendo , na kutegemea utukufu wa Mungu katika maisha yetu; tukumbuke Yesu alivyoendelea kujibishana na Petro na alivyomwambia;Yeye aliyekwisha kuoga hahitaji kuoga tena bali kusafishwa miguu yake  kwa kuwa mwili wake bado uko safi ; Na wewe ni safi, lakini si nyote; Yesu hapa alionyesha kuwa mbali na kuwasafisha miguu bado sio wote wako safi kwani alijua kuwa yuko mmoja ambaye atamsaliti.

Tafakari ya Leo inatufundisha kuwa tunatakiwa kuwa na subira na kupokea maelekezo kwa unyenyekevu ili kuona baraka ya Mungu juu yetu; alionyesha upendo kwa mitume wake lakini alitaka na mitume waonyeshe upendo miongoni mwao na kwa wale wote ambao watakuwa pamoja nao. Tunatakiwa kutimiza upendo wetu kwa matendo na sio maneno matupu. Petro ametu onyesha kuwa alivyokuwa anamchukulia Yesu ilikuwa tofauti na Yesu alivyokuwa akitaka iwe au ifanyike; Petro alikuwa anamchukulia yesu kama Kiongozi ambaye hastahili kuwaosha miguu mitume wake kwani hiyo ilikuwa ni kazi ya Kitumwa; Mitume walitakiwa mwamwoshe miguu yesu; Lakini yesu anawaonyesha Mitume Hasa Petro kuwa Miguu ni sehemu ya Utakatifu; hivyo kuwaosha wao miguu yao  maisha yao; yesu aliwaosha Miguu yao bila kujali hali ya miguu yao na uchafu na harufu yake; alifanya kwa upendo mkubwa wa kuosha na kuifuta

Pamoja na Udhaifu mkubwa wa Petro kila anapofanya mazungumzo ya muda mrefu na Yesu alikuwa anaharibu , au anaongeza majukumu zaidi , kama alivyomwambia Yesu, sawa basi isiwe tu miguu yangu, bali mikono yangu, na kichwa change; petro ametuonyesha kuwa amlikuwa na unyenyekevu wa kukubali makosa na kasha kuomba msamaha na kutekeleza yale alioombiwa; tukumbuke kuwa safari yetu ya njia ya maisha ni chafu sana kuliko sisi tunavyofikiria. Maisha yetu yawe kama yale ya Yesu na mitume wake kwani daima alikuwa akiwaelekeza ili waondokane na uchafu wa maisha ya dunia hii; kukaa na kudumu katika usafi wa kiroho ni mtihani mzito kutokana na  ubinadamu wetu na tabia yetu ya kuwa tunajua zaidi na hatutaki kufuata maelekezo kama Petro. Tuendelee kukumbuka kuwa . Hakuna jambo ngumu kukaa katika usafi , sisi wote ni wachafu zaidi kuliko kuliko tulivyo sasa.  Ujio wa Yesu na kuwa tayari kufa msalabani ni sawa na kualikwa kwa hiari kwenda kuoga ili tuwe safi na tuweze kuvaa nguo safi ambazo zimesafisha kwa damu ya mwana kondoo; hivyo sisi bado tunahitaji kutakaswa kila siku kwa damu ya Kristo .

Tafakari yetu ya leo inatukumbusha kuwa kama vile ilivyokuwa kwa Mtume Petro, sisi sote ni wadhambi kwani Yesu katika Mazingira tofauti alishawahi kumwita Petro shetani, na kumwambia aondoke mbele ya uso wake; kwa mawazo na jinsi ambavyo Petro alikuwa akifikiri na kujibu bila kutafakari hata kama nia yake ilikuwa njema katika maona ya kibinadamu; hivyo sote yunaangukia katika mtego huu wa Petro kwani pamoja na nafasi ambayo tumepata kupitia wokovu wetu kwa damu ya Yesu Msalabani bado tunafanya mambo bila kufikiri; kwa njia za kibinadamu hivyo nasi bado tunahitaji msaada na huruma ya Mungu.

Tukumbuke kuwa sisi binadamu wote ni wadhaifu na tutabaki kuwa wadhaifu bado tunaelea katika dimbwi la zambi; tunaendelea kutawalaiwa, kuishi kwetu, kufikiri kwetu, hata wakti mwingine matendo yetu  yamegubikwa na maovu, na tumekuwa na kiburi hata cha kukiri kuwa ni wakosefu; baada yake tumeendelea kujiona kuwa tu watakatifu miongoni mwa wa watakatifu wa kweli japo matendo yetu yamejaa ushetani mtupu. Mtume Petro anatuonyesha kuwa pamoja na udhaifu wake kama binadamu aliweza kutoa maamuzi haraka hata kama yalikuwa yakikingana na mwono halisi wa Yesu lakini alionyesha Imani hata kama ni dhaifu. Alikuwa tayari, kutembea juu ya maji japo alianza kuzama kwa uhaba wa imani; bora yeye aliyejaribu kuliko wale kumi na moja ambao hata hawakutamani kujararibu;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa sisi binadamu tunaishi katika maisha hatarishi sana bila kujitambua na hata pale tunapopatiwa msaada tunakuwa na mwelekeo wa kuukataa kama vile Petro alivyokuwa akimkatalia Yesu alipokuwa akitekeleza tendo kuu la unyenyekevu. Tukumbuke kuwa bila kuwa wanyenyekevu hatuwezi kujitambua kuwa tunatembea katika njia sahihi. Hivyo Alhamis hii Kuu itukumbushe dhana nzima ya kumtumikia Mungu Kupitia unyeneykevu ambao itatuondolea majisifu binafsi; kujiamini na kuto mtegemea Mungu wetu; Narudia tena leo tujikumbushe kuwa daima tunakuwa wepesi wa kuongea hata bila kufikiri matokeo ya baadae; Lakini uzuri wa Petro alikuwa Mtume Pekee ambaye aliweza kujaribu bila kuwa na mashaka. Pamoja na Petro kuitwa ni Mtu mwenye imani , lakini mwepesi wa kukiri na kuomba msamaha. Ndio maana Yesu alimchagua kuwa Nguzo ya Kanisa lake na kiongozi wa Kondoo wake duniani.  

Tafakari yetu ya leo inatuonyesha Yesu ametuonyesha njia ya upendo wa khali ya juu bila kubagua kwani alimwosha miguu hata msaliti wake wakati akijua ndiye atakaye msaliti. Hivyo findisho tunalolipata leo ni kuwa tayari kuwahudumia wengine hata kama hawatupendi, na tutapata kheri sana na faraja kubwa kwa kufanya hivyo; Najua kuna baadhi yetu huwezi kuosha miguu wenzako kwa sababu ya mafanikio ambayo mtu anakuwa anayo na hata kama atafanya hivyo atafanya kwa wale tu wanaofanana; hatuko tayari kuwasaidia yatima, wajane, masikini na wote wenye hitaji la kweli;
Tafakari ya siku hii ya leo ni muhimu sana katika maisha yetu ya kiroho; kwani baadhi yetu sit u tumekuwa wagumu kuwaosha miguu jirani zetu , tunajifunza kwa  Yesu ambaye aliosha miguu ya muuaji wake ( Judas ). 

Je tunaweza sisi kumtendea jema Yule ambaye tunajua hakupendi, anakusengenya, anakuchukia? Tunatakiwa tujifunze Ukarimu wa Yesu kwetu sote bila hakutubagua alitupenda jinsi tulivyo; tunachotakiwa kujifunza hapa ni kuwa  huwezi kuwa mkarimu kwa watu mpaka umejifunza kuwa na subira na kukubali kuwa mtu wa kawaida. Na kubwa zaidi huwezi kuwa Mkarimu bila kumkaribisha Mungu kwa njia ya Roho yake imeweze kuishi ndani yako; binadamu wengi ukarimu wetu tunajaribu kuuonyesha katika tabasamu lakini ndani ya mioyo yetu tu chui wa kuogopwa. Ndio maana mara zote katika mafundisho yake Yesu alisema waogopeni wanafiki na wale ambao wanapenda sana kujikweza;

Tafakari yetu inatuasa kuwa tunaishi katika ulimwengu unaojiendesha kwa kuto kumpa Mungu nafasi; tunawaona watoto wetu wakijiua wenyewe kwa kukata tamaa au kwa kujiingiza katika ulimwengu wa dhambi; Tunashuhudia wanasiasa wakiendelea kuwa waongo na kujilimbikizia mali huku wakiwaacha wajane , Yatima, na wamanchi masikini wakiwa wakiendelea kuteseaka; Hivi Alhamis hii kuu tujirudi kama Mtume Petro ambaye hatimaye alikubali kuoshwa miguu yake na Yesu na kutimiza amri ya upendo na hatimaye kuwa kichwa cha kanisa.

Hii ndio Tafakari yetu ya leo nawatakieni Juma kuu Lenye baraka na Upendo wa Kimungu- Amina


Emmanuel Turuka

Wednesday, March 23, 2016

MSAADA WANGU UTATOKA WAPI?



March 23

Zaburi 121

Tafakari yetu ya leo tusome na kusali pamoja Zaburi hii ya 121 ambayo ni mwongozo mzuri sana katika ulinzi, na mafanikio ya maisha yetu. Kwa zaburi hii Mungu anatenda kazi ya upendo wake kwetu kupitia ulinzi wake katika maisha yetu ya Kila siku. Mungu atabaki kuwa Mungu wakati wote. Tuna kila sababu ya kufurahi na kuringa kama wakristo.

1  Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi?

2  Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

3  Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye;

4  Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5  Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume.

6  Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.

7  Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako.

8  Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Hii ndio Tafakari yetu ya leo tunavyoendela kumshukuru Mungu katika Juma hili takatifu tukisubiri sherehe ya Bwana- PASAKA   - Amina.

 Emmanuel Turuka





Tuesday, March 22, 2016

YESU ALIHESHIMU MAMLAKA YA DUNIA PAMOJA NA TABU ZOTE ALIZOPATA KWANI ALIJUA YAMETOKA KWA MUNGU:




March 22,

Yohana 19:10 – 11

Tafakari ya Leo tunaangalia jinsi Yesu alivyokuwa akiheshimu mamlaka ya dunia ni kweli kwamba Utekelezaji wa sheria  za kidunia ni udhihirisho unaonekana wazi kuwa Mamlaka yao yanatoka kwa Mungu. Jukumu la viongozi wa dunia ni kuwapa watu haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru , ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima upendo. Mathayo 22:21 Akawaambia Basi mlipeni Kaisari yaliyo ya  Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu. Yesu aliheshimu  Mamlaka ya dunia na alikuwa akiikosoa pale ilipokuwa ikikosea.

Tafakari inatuonyesha kuwa kwa upande mwingine hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na wale ambao hutumikia serikali hizo wamepata kibali cha kuongoza toka kwa Mungu japo wakati mwingi hutenda kinyume na maelekezo ya Mungu kwa ustawi wa jamii husika. Anayepinga mamlaka ya serikali ya kidunia anakiuka agizo la Mungu. Sheria inatusaidia kufanya yaliyo mema; Watawala ni watumishi wa Mungu , kujitoa wenyewe kwa utawala wa sheria; Mamlaka ni haki halali ya kutekeleza utii. Ni nguvu ya kushawishi au tabia amri. Wagalatia 5: 22-23  Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha , amani, uvumilivu , wema, fadhili , uaminifu, upole na kujizuia. Juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Warumi 13:4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili  ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Mungu ndiye mwenye mamlaka ya mwisho, na Mungu anatumia serikali za watu wenye mamlaka kwa kusudi lake na letu pia. Biblia inatufundisha kwamba serikali zisizo hudumia watu na kutimiza lengo ambalo Mungu amekusudia Mungu huziondoa.Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba watu wafanye hivyo kwa furaha wala  si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

Warumi 13: 1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye Mamlaka hushindana na agizo la mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao  hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya.basi wataka usimwogope mwenye mamlka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.

Tafakari ya leo inaendelea kutubaanisha kuwa, Mithali 29:18 Pasipo maono watu huacha kujizuia, Bali ana heri mtu Yule ashikaye sheria. Taifa bila nguvu ya Mungu halina baki shagala bagala halifuati sheria. Heri wale wafuatao sheria. Mhubiri 10:17 Heri kwako, nchi mfalame wako akiwa motto wa watu, na wakuu wako hula wakati ufaao, ili makusudi wapate nguvu wala si kwa ajili ya ulevi. 28:2

Viongozi Mithali 11:14 Pasipo Mshauri mzuri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri hujawokovu; mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; kit chakecha enzi kitathibitika milele.  Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; bali yeye apokeaye rushwa huipindua. Yesu alipopelekwa mbele ya Pilato Yohana 19: 10 – 11 Basi Pilato akamwambia husemi name? hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, name nina mamlaka ya kukusulubisha? Yesu akamjibu, wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana dhambi iliyo kubwa zaidi. Yesu hapa anaendelea kutonyesha kuwa mamlaka zote za dunia zinatoka kwa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mamlaka ya Pilato juu ya Yesu bado ilikuwa chini ya Nguvu ya Mungu ambaye alibariki hukumu ya Yesu Kufa Msalabani kupitia mamlaka ya dunia hii kupitia Pilato. Ili Yesu aweze kukamilisha kazi yake ya ukombozi wa Wanadamu ambao walikuwa wamezama katika dimbwi la dhambi; Yesu alipata faraja yake katika wakati huu si kwa sababu ni mapenzi ya Mungu yaliyotimia ndani ya Uongozi wa Pilato; hivyo tunachojifunza hapa ni kuwa Yesu hakuwa na wasiwasi katika mikono ya hofu Pilato , kwani alijua kuwa Pilato alikuwa  katika mikono ya Baba Yesu. Kama 1 Peter 2: 13-17 Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa. Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni mungu. Mpeni heshima mfalme. Mfano wa kuteswa kwa Yesu.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tusifadhaike na watawala ambao wanaweza kuua miili yetu lakini hawana nguvu ya kuua roho zetu, uwezo ambao wamepewa na Mungu unamipaka yake kwa ustawi wetu kama 2 Mambo ya Nyakati 7:14 ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watanyinyenyekesha, na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitaskikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Pilato ana mamlaka;  Herode ana mamlaka;  Askari wana  mamlaka;  Shetani ana mamlaka; Lakini hakuna hata mmoja wao ambaye anamamlaka yanayojitegemea yote wamepewa na Mungu hivyo hatuna sababu ya kuogopa kwani mamalaka yao kwa wao wenyewe hayana nguvu; na Mungu kamwe hatawapa nguvu za kutuangamiza sisi; Hivyo nasema tena hatutakiwi  Kuogopa; tumshukuru Mungu kwa kutupa sisi thamani kubwa kuliko yeyote lakini inatakiwa tutimize wajibu wetu;

Hii ni tafakari yetu ya leo Nawatakie maandalizi Mema ya Juma kuu kuelekea sikukuu ya Pasaka Siku muhimu katika wokovu wetu Amen

Emmanuel Turuka



Monday, March 21, 2016

MAISHA YA KIROHO NI KAMA MATUMIZI YA KAMERA:



March 21

Wafilipi 3:13,14

Tafakari ya leo tunaangalia kazi kubwa ya Kamera ambayo ni kupiga picha mbali mbali, ili kuweze kupata picha nzuri mpiga anatakiwa kuwa makini kwa kulenga vizuri (focus) ili kuondoa vivuli ambavyo vinasababisha picha kuto kuwa nzuri; hii inaonyesha umuhimu wa kuweke mtazamo wake  juu ya nini anatakiwa afanye kuweza kupata picha nzuri. Maisha yetu ya Kiroho ni sawa na Matumizi ya kamera ni muhimu sana tunavyotekeleza maisha yetu ya Kiroho kuhakikisha wewe ni kulenga jambo sahihi. Lazima tukubali kuwa tunaishi katika wakati ambao kuna vitu vingi ambavyo vinaendelea katika maisha yetu na vinatutoa katika mwelekeo sahihi wa kuishi kama wakristo.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa katika maisha yetu ya kila siku, tumekuwa watu ambao tumejawa na wasiwasi na kusumbukiaa kwa mambo mengi ambayo sio muhimu, na tumesahau kuzingatia au kulenga zaidi katika maisha tunayotakiwa kuishi ya kumtumikia Yesu, Mwenyezi Mungu anataka sisi kuzingatia/kulenga (focus)  zaidi katika dhumuni hasa la maisha yetu hapa duniani; Tukumbuke kuwa maisha yetu daima yanalinganishwa na Kamera ili iweze kutoa picha nzuri inahitaji umakini; Je  tunajua kwa nini Mungu anataka sisi kuzingatia Maisha yetu?  Jibu ni rahisi sana kwa sababu Maisha yetu ni kama kamera; ili kufaninikisha lazima tujipange vizuri; katika upigaji, eneo la kupigia picha, khali ya hewa; na mwelekeo wa mpiga picha.Hivyo  maisha yetu tunatakiwa uchaguzi mzuri katika  kila hatua ambayo tunayoishi kwa utukufu wa Mungu .

Tafakari yetu katka Juma hili kuu inaendelea kutukumbusha kwamba katika kila jambo lolote tunalofanya tufanye mambo mazuri ambayo kuongeza thamani chanya kwa maisha yetu; Mambo mema yataongeza kumbukumbu zetu nzuri na uzoefu chanya; kwa kuzingatia  nini ni muhimu tukichambua kama kamera inavyofanya kazi na kutoa picha nzuri. Sisi tunatakiwa tumlenge Yesu uli tuweze kupata picha yetu nzuri, hata pale tunapo patwa na ugumu wa maisha,na shida mbali mbali katika maisha yetu bado tunatakiwa tuondoe hivyo vivuli ili bado iwe kwa yesu. Hatutakiwi tuondoe focus yetu kwa Yesu eti kwa sababu  tu ya Maumivu ambayo tumeyapata katika maumivu yetu; 

Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Daima sisi tunaishia kuchukua picha mbaya kwa vile hatuko tayari kuzingatia taratibu nzuri za kupiga picha. Lazima tukubali kufuata utaratibu ambao kristo anataka sisi tufuate tunapopiga picha za kiroho; tukifanya hivyo tutaweza kutimiza  kutimiza furaha yake ni katika sheria ya Bwana, na juu ya sheria sisi yatupasa kuitafakari mchana na usiku.

Tafakari yetu inaendelea kutukumbusha kuwa mkazo/mlengo/Focus itukumbushe kwamba hatupaswi kuendesha maisha yetu kulingana na maoni au mifano ya marafiki zetu. Tunajua hivi sasa dunia yetu iko katika kipindi ambacho kila kitu cha kibinadamu vinakwenda kwa speed ya haraka sana na tunajiona kuwa sisi ndio wamiliki wa dunia hii na tunaweza kufanya chochote tukipendacho  bila msaada wa Mungu. Kama Warumi 12: 1  Basi  hivyo, ndugu na zangu  , nawasihi kwa huruma zake itoeni miili yenu iwe  dhabibu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye Maana. Luka 9:23 Akawaambia wote, yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake anifuate, hii inatufundisha kuwa kama tutamtanguliza Yesu Mbele ya maisha yetu na tutayatoa maisha yetu kwa ajili ya ufalme wa mungu tutapata Picha nzuri sana katika maisha yetu ya hapa duniani na hata mbinguni. Tunatakiwa kujitoa kabisa kwa Mungu na kutenda haki kwa utukufu wa Mungu.  

Tafakari ya leo  inatuelekeza katika ukamilifu wa kweli tunapojiandaa kutumia maisha yetu kama kamera katika maisha yetu ya Kiroho; Tunatakiwa kuendelea kujitathimini sisi wenyewe, kuiangalia taswira ya Picha katika kamera kabla ya kuipiga kwa kuangalia kila upande na kila kona hata kuikuza ili kupata taswira halisi kabla ya kukamilisha kitendo cha kupiga picha. Kabla ya kupiga picha tunatakiwa kurekebisha taswira kwa kujiuliza maswali yafuatayo; Je uhusiano wangu na Mungu Ukoje? Je uhusiano na familia yangu pia ukoje? Je uhusiano wangu Kazini ukoje? Je natimiza mwito wa Mungu kama alivyonielekeza kufanya? Je nina mheshimu Mungu pamoja na amri zake? Je nimeweza kufanya kazi yeyote ambayo imekuwa na matunda ya kiroho katika Jamii yangu na kwangu Mwenyewe?

Hii ndio Tafakari yetu ya leo ; kama tutajibu maswali hayo inavyopasa basi matumizi ya kamera ayetu ni ya kuigiwa mfano na Mwenyezi Mungu atakujalia maisha mazuri sana na hata baadae Mbinguni.


Amen

Emmanuel Turuka
(life is like Camera)

 




Sunday, March 20, 2016

JE YATUPASA KULIPIZA KISASI DHIDI YA WENZETU - JUMAPILI YA MATAWI;


March 20

Mathayo 6:14-15

Tafakari ya leo tujikumbusha kuwa mwanandamu anahitaji upeo mkubwa wa nuru ya kiroho ambayo itaweza kumfanya azike tamaa zake na hisia zote za kulipiza kisasi; tunatakiwa kuwa na uwezo wa kujizuia na hasira, kuzikandamiza hasira, chuki kwa moyo mpana na kujenga daraja la msamaha.  Kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima, kukutukana, kukusababishia hasira,kukudharau, kukudhalilisha na kadhalika sio jambo rahisi. Tumewaona hata watumishi wa Mungu ambao wanaielewa sana bibilia wakishindwa kabisa kuktekeleza kanuni hii.

Tafakari yetu leo tujikumbushe wajibu wa kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini  pasipo  imani  haiwezekani  (Waebrania 11:6). Inatufundisha kuwa mtu  amwendeaye Mungu  lazima  aamini  kwamba  yeye  yuko,  na  kwamba  huwapa  thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na Mungu katika Imani.

Kama ilivyoandikwa hakuna mwenye haki, hata mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba msamaha imeelezwa katika Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi aliweka wapi tumaini lake la msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu." Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo alivyowasamehe ninyi."

Kusamehe kwa kweli hakuhesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini." Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi. Wakolosai 2:13-14 inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani."
Tafakari yetu inazidi kutufunsidha kuwa Zaburi 51:7-12 "Unisamehe nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi."
Zaburi 32:1-6 "Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo hayatamfikia yeye."
Wale walio wanyonge moyo wako mbele ya Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamoja na misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya: kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa mbaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wa ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazo uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha, upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yake kupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katika maisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimayeawe na uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia majeraha ambayo yamejenga chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea msamaha na utakaso wa Mungu ni; katika  imani jambo ni  rahisi na la maana sana kama tunavyofurahia kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia. Lakini kutokana na ubinadamu wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu sana kutoa msamaha wa kweli pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama tunayafuata mafundisho ya yesu na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu kama yeye alivyovaa unyenyekevu na kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na alikuja kukaa nasi na ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu lazima alipite ili kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
Hebu jitafakari kwa nini umekuwa na kiburi cha kushindwa kabisa kumsamehe, jirani yako, ndugu yako ambao wamekukosea kutokana na ubinadamu wao, usijali amekukosea mara ngapi angalia je wewe uko tayari kumsamehe wakati wowote ule?
Hii ndio Tafakari yetu ya leo katika Jumapili hii ya Matawi- Amina

Emmanuel Turuka


Friday, March 18, 2016

JE YATUPASA KUMKIMBIA MUNGU?


Jonah 1:1-17


March 18




Tafakari ya leo imatukumbusha kuwa hata katika tabu zetu, woga wetu wa kutimiza wajibu wetu mbele ya Mungu atutakiwi kumkimbia au kujitenga naye; Daima turudi kwake na kuomba msaada wa Mungu hata kama tumeumizwa namna gani hatuna sababu ya Kumkimbia Mungu. Tukumbuke kuwa hata kama tutajificha wapi; Mungu anatuona na atatutendea mazuri kulingana na unyenyekevu wetu kwake, Hii ni tafakari yetu ya leo

Thursday, March 17, 2016

JE SISI TUNAISHI KAMA TAI?



March 17

1 Wathesalonike 5:11


Tafakari ya leo tukiwa bado  tunaendelea na mfungo wa Kwaresima tunatakiwa tuishi kama Tai; Tai ni Ndege ambaye anaweza kuruka juu kuliko ndege wengine wote na kwa kasi ya ajabu sana. Tai ni ndege ambao wanaruka pamoja bila kubaguana kwa upendo mkubwa;  Tai anaona umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu. Tai anaouwezo wa kuona chakula kama vile samaki, kisha hulenga shabaa toka mbali na kumpata mlengwa. Tai ni ndege mwenye nguvu kuliko ndege wengine. Tai makazi yake yako juu ya miti mirefu sana kuliko ndege wengine. Je sisi kama wakristo maisha yetu ya Kumtumikia Mungu yanalingana na mwenendo huu wa Tai wa kujiamini?

Tafakari ya leo inaendelea kutufundisha kuwa tukiweza kutumia jicho la Tai katika maisha yetu tuishi kwa kufikiria mambo ya badae tunatakiwa tuwe kama Tai tuwe wa moja katika kumtumikia Mungu kama 1 Wathesalonike 5:11 Basifarajianeni na Kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya. Ni ujumbe mzito amba Tai wanaufanya pamoja katika maisha yao kama ndege. Hapa tunatakiwa kwanza ni kuithamini nafsi yako  na kuisikiliza sauti kubwa itokayo moyoni mwako,ikuongozae juu ya kutenda,hii ni sauti ya Mungu iletayo mafanikio,furaha na kila lililo jema.Sauti hii inakupa nguvu ya kutenda miujiza kila wakati,ndiyo inayofanya nuru ya maisha yako ing'ae. Lazima ujikubali kwa kuwa mimi ni zaidi ya nilivyo.Ukiachilia mbali mazingira ninayoishi na sura yangu,mimi ni wa thamani,kama wengine. Wewe ni wa thamani jinsi ulivyo,na thamani yako ni sawa na binadamu wote.Unao uwezo wa kuwa na kuishi maisha ya furaha na mafanikio. Unastahili, wewe ni Matokeo ya kazi kubwa ya Mungu. Tunatakiwa kuanza kujikubali na kuepuka misukumo ya wale wanaokuzunguka. Anza kutazama uwezo ulio nao,tazama chemchem ya mafanikio iliyopo ndani mwako.Sisi sote ni bora .Sisi wote ni wamoja. Huu ni wakati wa kujifunza kuwa wewe, kujikubali, kukua na kubadilika. Anzakujitambua wewe kisha utatambulika kwa wengine. Kama vile Tai walivyojitambua kuwa wao ni ndege bora na wanaweza kruka juu kabisa kuliko ndege mwingine yeyote.


Tafakari ya leo inataka sisi tuvumbue uwezo ulionao.Tumia uwezo tulionao kupaa  juu ya mipaka unayofikiri ipo katika kuutafuta ufalme wa Mungu. Fanya yale unayoyakusudia maishani na uwe vile unavyotaraji kuwa. Umezaliwa kuwa kiongozi wa maisha yako na kuyatawala mazingira yako ili kuufikia uzima wa milele.Unaweza kupaa juu zaidi na zaidi pasipo kudondoka. Vikwazo vijitokezavyo dhana ya kifikra tu. Hatupaswi kuruhusu kuruhusu fikra za wanaokutuzunguka zitufanye tuwe na mawazo mgando ama yenye mipaka na kutuletea mashaka katika safari yetu ya mbinguni. Huwezi kuruka juu kama tutabaki na fikra kama za kuku na kuendelea kukwaruza na kudonoa tu. Amua sasa kuruka juu ili kumtumikia Mungu.


Tunataadharishwa kuwa lazima tuwe kama Tai kuwa na maono na nguvu ya kuamua, ili waweze kutambua na kufanikiwa katika mawindo yetu na kufanikiwa kupata kila kutitakacho; Wakati huo huo, tai unaweza kuona adui zake kutoka mbali, kama vile nyoka amabao anajaribu kuvamia kiota chake ili aweze kuiba mayai yake au kuua vijana wake. Ingawa tai kujenga viota vyao kwenye miamba ya juu na maeneo, nyoka kuwa na tabia na uwezo wa kupanda kwao. Lakini maono kali ya tai yanaamsaidia kuona maadui kutoka mbali na kiota chake. Tukisoma Warumi 14:17 maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furahakatika roho Mtakatifu.

Sisi kama watoto wa Mungu ni lazima kuzingatia malipo mambo mazuri ya amani, furaha, na haki. Tukumbuke kuwa lazima tujiandae kwa nguvu zote tukijua kuwa shetani na wafuasi wake wana uwezo wa kushambulia kiota chetu, ambayo ni Familia yetu, fedha, mahusiano, afya, ustawi wa kiroho, Wakati ulimwengu mapepo ya enzi, mamlaka, na wakuu wa giza hili ambao ni kujaribu kuiba, kuua na kuharibu maisha yetu tele ya Mungu ndani ya familia zetu, wapendwa, na jamii yetu, tunaona ni kutoka mbali na mtizamo na maono nguvu ya Mungu na kuanza kupinga hilo kwa kushambulia yake. adui ambaye anajaribu kuja katika kuwa na hofu na kukimbia mbali 1 Peter 5:8 Muwe na Kiasi na kukesha kwa kuwa mshitaki wenu ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze. Hivyo tunatakiwa tuwe na nguvu za kushindana na adui kama Tai afanyavyo. Tunatakiwa kuendelea kuomba bila kuchoka; ili kwa neema ya Mungu tuendele kupata faraja kubwa sana.


Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa ushindi wetu uko juu ya Mwili na damu ya Bwana wetu Yesu Kristo; Yohana 6: 55-57 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli , na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye Mimi wataishi kwa sababu yangu. Maana yake ni  nini? Sisi , waumini , ni mmoja ambaye kula nyama safi ya maneno ya Yesu kutoka mbinguni kupitia mafundisho Roho Mtakatifu , ambayo daima kutufanya kuishi maisha yake hapa duniani kifalme kama vile tulivyopasa tuishi mbinguni; 1 Kor 2:13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho,tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.


Tafakari ya leo inatufundisha kuwa Tai ni ndege wanaopenda sana  kuwa tayari wakati wa  dhoruba.Tunafahamu kuwa ndege wengine wote hujaribu kuto ruka wakati wa dhoruba na kujificha kwenye viota vyao au mapango yao kwa ukali  wa upepo, Lakini tai hupenda  kuruka  wakati huo kwa kutumia upepo wa dhoruba ili waweze kuruka juu zaidi kwa muda mfupi. Tai ni wanjanja kwani wanjua kwa kutumia upendo wa dhoruba wataruka juu dhaidi bila kutumia nguvu yao watakuwa wanaelea tu na kusukumwa na upepo huo. Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na dhoruba nyingi katika maisha yetu kama shida mbalimbali, majonzi, na majaribu malimbali; tukisoma Yohana 16:33 Haya nimewaambieni mpate kuwa naamani ndani yenu. Ulimwengu mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. Au Kitabu cha Yakobo1:12 Heri mtu astahimiliye maajaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa atalipokea taji la uzima. Bwana alivyowaahidi wampendao. Lakini tukumbuke kuwa tunatakiwa kuhesabu furaha tupu tukiangukia katika majaribu mbalimbali, mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

James 1: 2-4. Tukumbuke jini Mungu alivyomjaribu Ibrahimu kabla ya yeye kuaminiwa kwake kama rafiki yake mpendwa kwa milele

Tulio wengi tukijaribiwa kidogo tu; tunalalamika sana na kukata tamaa baadhi yetu tunakuwa kama Waisraeli walivyokuwa wakimlalamikia Mungu alipowatoa katika nchi ya Mateso Misri; tukumbuke kuwa Mungu anahitaji kutu pima kwa sababu sisi sio viumbe kamili bali tunahitaji kusafishwa kupitia majaribu mbalimbali, na mateso ili tupate kuwa wakamilifu; na mara baada yamajaribu, Mungu hutuimarisha sisi kwa milele yeto; 1 Petro 5: 10 Na mungu wa neema yote aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milelekatika kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yey mwenyewe atawatengeneza na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.

Je sisi ni kama tai ambao daima kujenga viota vyao katika mahali pa juu ambapo adui hawezi kufikia kwa urahisi? Mungu siku zote ana nguvu za kutuinua sisi juu lakini yatupasa kuwa Wanyenyekevu, masikini wa roho,tuwe wapole na tuwe rehema ya Mungu; Tukumbuke kuwa kama tai anavyowapenda watoto wake: Mungu alitupenda sisi zaidi, kwani ni upendo gani mkubwa wa kumtuma Mwana wake wa pekee kuja dunia kuishi nasi na kasha kufa katika kifo cha aibu msalabani ili nasi tuweze kingia katika ufalme wa mbinguni;



Tunafunga Tafakari yetu ya leo kuwa kwa kutilia mkazo jambo kuwa kama ilivyo kwa tai katika anga inawakilisha siri ya Mkristo ambaye amejifunza na kuwa tayari kumpigania Mungu katika khali yeyote ile katika ulimwengu wa roho, tunafahamu kuwa tupo kwenye changamoto nyingi kama upepo wa mashaka na dhoruba za maisha bali tunatakiwa kutegemea zaidi msaada wa Mungu. Hivyo tukiweza kumtegemea Mungu yeye atatufanya sisi tuweze kupaa juu zaidi na kuelee katika dhoruma yeyote ile bila shaka lolote.

Tunatakiwa kuwa kama Tai ili tuweze kuweza kufurahia maisha utakatifu, ni moja ya siri kubwa ya imani. Tunatakiwa kutenda kama Yesu na kuishi maisha ya mkristo kwa uadilifu mkuu na  ili tuweze kushinda maisha ya ufalme wa mbinguni.  Tunatakiwa tuwe, si jogoo wala kuku .

Hii ndio tafakari yetu ya leo



Emmanuel Turuka