WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, March 2, 2016

JE TUNATEMBEA KATIKA NURU YA BWANA?




March 1

Tafakari ya leo tuangalie wazo nzima la kuwa Mungu ni mwanga na ndani yake hakuna giza. Kwa msingi huu kama sisi tunajiona kuwa tuna ushirika na Mungu hivyo nasi tunapaswa kutembea kwenye mwanga na kuishi kulingana na maelekezo ya Mungu ambayo ni ukweli.

Tukisoma 1Yohana 6-7 tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake yatusafisha dhambi yoye.

Tukumbuke kuwa kwa dhambi zetu tulikuwa gizani lakini kwa kifo cha Mkombozi wetu msalabani Damu yake imetusafisha na kutuondoa katika giza la dhambi ambalo limetuzunguka kwa siku nyingi sana; tatizo letu wanadamu pamoja na kazi kubwa ya Bwana wetu Yesu Kristo kutufia bado tunakawaida ya kurudi katika dimbwi la dhambi na hivyo kuendelea kutembea katika giza.

Tafakari ya leo inatukumbusha kwa mara nyingine tuache kutamani kutembea katika giza bali tutuembee katika mwanga wa kweli tukibadilisha matendo yetu;  swali la msingi je tuko tayari kuziacha dhambi zetu na kumrudia Mungu?

Tukisoma kitabu cha Mithali 1:7 kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, bali wapumbavu huhdarau hekima na adabu. Maonyo dhidi ya kushirikiana na waovu.

Tunapotembea katika mwanga wa Mungu huko tunapata ukweli, amani na matumaini.  Tunajua kazi ya mwanga katika maisha yetu. Na tunajua madhara ya giza katika maisha yetu. Nuru au mwanga ni jambo au kitu ambacho sisi binadamu wote tunakihitaji kwani mwanga utusaidia sisi kufika pale tunapotaka kufika bila matatizo au bila kupata shida yoyote ya kupapasa au kujikwaa. Lakini tunapotembea katika giza mashaka hutawala, uhakika wa kufika safari yetu salama hutoweka, kwani huna ukakika pale unapokanyaga ni mahali sahihi hivyo tunaishia kujigonga, na hata kutumbukia kwenye korongo.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa Giza limejaa vitisho, giza linasababishamsongo wa ubongo,  giza linakwamisha uwezo wako wa kufikia lengo. Kinyume chake ukitembea kwenye mwanga unafanikiwa kufikia malengo haraka, mwanga unakupa amani, mwanga unakupa afya njema, mwanga unakusaidia kuona kilicho cha hatari mbele yako. Kwa kweli mwanga ni chanzo cha uhuru na furaha. Hivyo ukitembea katika Nuru ya Bwana mateso yote yatokanayo na giza kwamwe hayawezi kukusumbua.

Tafakari ya leo inatushauri kuwa ili kuishi katika furaha ya kweli lazima tupate kibali cha Mungu kupitia mwanga wake, bali tukiendelea kulikumbatia giza kamwe hatutuaweza kupata furaha hiyo. Kwani yeye ndiye njia ya uzima na lazima tupitie katika njia hiyo kwani ndio njia pekee ya uhakika na hiana mashaka hata kidogo hivyo mwanga ni tumaini la kweli katika furaha ya kweli. Yakobo 4:4 Enyi wazinzi, hamjui kuwa ya kwakba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Tunaposema kutembea kwenye mwanga maana yake ni kuishi kulingana na maelekezo na utawala wa Mungu na sio wa kidunia Tunatakiwa kuona vitu jinsi mungu anavyoona na kutekeleza kadiri ya maelekezo yake. Mathayo 6: 22-23 Taa ya mwili ni jicho basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu. Basi mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo. Utawala wa giza ni utawala ule ambao ni kinyume na matendo mazuri ya mungu

Tafakari ya leo inatufundisha kuwa Giza linatutenganisha na neema ya Mungu: tukumbuke kuwa Mungu ni NURU na ametukaribisha sote katika kuipokea na kuifurahia hii nuru; tukumbuke kuwa pale tunapokubali kutembea katika mwanga wa bwana uwepo wake unatemebea nasi daima; Mungu daima hutuongoza tupitapo, tatizo letu tunajifanya tunajua njia ya kupita wakati kumbe sio kweli hivyo tunaishia kwenye giza;  Zaburi ya 27:1 bwana ni nuru yangu na wokovu angu,Nimwogope nani?  Bwana ni ngome ya uzima wangu , Nimhofu nani?

Tunakumbusha kuwa giza ni matendo yote yanayopingana na maelekezo au utendaji mzuri wa Mungu juu yetu; tumepewa akili ili tuweze kufikiri na kutenda vile Mungu anavyotaka sisi tutende ili tuyafurahie maisha ya hapa dunia na kasha mwisho wa safari yetu huko Mbinguni. Giza huaribu akili zetu na utusababishia sisi kupata tabu ya milele.

Tukumbuke Habakuki 1: 13 wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye.


Tafakari ya leo inatusisitizia kuwa tunatakiwa tusimame upande wa Mungu na kumtumikia yeye kwa ukweli ili kufanana na mwanga aliotujalia. Tunapaswa kuwa wakweli kwa matendo yetu na kukiri kuwa giza halina nafasi katika maisha yetu Amen.

No comments:

Post a Comment