WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, March 15, 2016

MTAZAMO WAKO DHIDI YA MUNGU UKOJE!



March 15

Wafilipi 2:5

Kwa ujumla Mtazamo/tabia ni zao la ndani ya kila mmoja wetu tunapolinganisha na mazingira yanayomzunguka kama watu na vitu; Tabia inatumika sana wakati unapofanya kitu chochote nje yako mwenyewe yaani kitu ambacho akikuhusu wewe mwenyewe. Neno la Mungu linatukumbusha katika hili kuwa kwa kuwa kwetu wakristo tunatakiwa kuimarisha tabia na kuwa kama Yesu; Tukisoma Wafilipi 2:5 Iweni na nia iyo ndani yenuambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu: Tukisoma Waefeso 4:22 mvue kwa habari ya Mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya;

Wengi wetu kwa urahisi tunaweza kutambua mitazamo mibaya kuonekana katika mazingira tofauti kutoka na vitendo vyetu kama uasi, dharau, kukosekana kwa uvumilivu, kukosekana kwa ushirikiano, kutojali, kuvunjika moyo, kokosekana uhuru, dhulma, kiburi, ubinafsi, Hii ni mifano ya msimamo mbaya ambayo Wakristo wanapaswa kukataa.

Mithali  23:7 hata mshale umchome maini; kama ndege aendaye haraka mtegoni; wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake. Tukumbuke kuwa mtazamo au tabia ni zao la mtu la ndani, limejificha ndani ya mtu ambalo ndilo msingi wa matendo yetu tuyafanyayo. Hakuna mtu yeyote ambaye ajuaye wewe unafikiria nini; ndio maana unaweza ukamchekea mtu na kumwonyesha kuwa wewe ni mtu safi sana kwake bali mtazamo wako uko tofauti sana; kumbe wewe ni adui, mkubwa; Lakini usijisahau kuwa Mungu anajua nini unawaza na nini unataka kumfanyia mwenzako. Hivyo Mtazamo au tabia ni kitu ambacho Mungu tu ndiye anayefahamu na yeye pekee anaweza kukusaidia kukurekebisha kwani mabadiliko hayo lazima yaanzie ndani yako na kwa Masada wake.

Mifano ya tabia mbaya iko mingi hasa kwa sisi wakristo kuna wale ambao wanakwenda kanisani na kushiriki vitu vingi hata uimbaji wa kwaya, utoaji wa michango mikubwa, wenye furaha wakati wote kwa sababu kila kitu kipo sawa kwa upande wao; Kwa bahati mbaya mambo ya kigeuka hasa upande wa uchumi yakianza kwenda vibaya kila kitu uanza kugeuka mahudhurio kanisani yanapungua; watu wanaanza kujijengea chuki na watu wengine na hatimaye chuki hiyo hujengwa dhidi ya Mungu wakiamini kuwa kwao Mungu ni sababu ya anguko lao; hivyo uasi unaanza hapo.

Lakini tukumbuke kuwa mtazamo ulio bora wakati wa shida inatakiwa kwa tuwe karibu zaidi na Mungu - kuangukia miguuni pa Yesu. Biblia inaeleza wazi kwamba Mungu hufanya mambo yote katika wakati wote kwa upendo ule ule bila kubadilika katika mafanikio yetu na katika shida zetu; tukumbuke kuwa shida kamwe haitamshinda mtu mwenye mtazamo sahihi na mwenye kumtegemea Mungu.

Wagalatia 5:19-21 Matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi; husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawatauridhi ufalme wa Mungu.

Tutambue kuwa mtu yeyote ambaye ana tabia mbayo inakwenda kinyume na mamlaka ya dunia pia ana matatizo mbele ya Mungu.Wagalatia 5: 22-23 lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu, wema, fadhili. uaminifu;  upole, kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Mtazamo sahihi mbele ya Mungu:  Zaburi ya 111:10 kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, wote wafanyao hayo wana akili njema, sifa zake zakaa milele. Tukisoma Marko 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwan nguvu zako zote. Yohana 14:15 mkinipenda, mtazanishika amri zangu. Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpigeni Shetani, naye atawakimbia.  Mtazamo wetu lazima heshima, utii, upendo, uaminifu, unyenyekevu, utii, worshipful, na sala.

Mtazamo wetu kuhusu watoto wa Mungu Yohana 13: 34-35 Amri mpya nawapa, mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Warumi 12:10 kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu. Wakolosai 3: 16 Neno la kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana  kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Waebrania 3:13 lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe  mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.

Mtazamo wetu kuhusu watawala wa dunia unatakiwa wa kuheshimu mamlaka, kushirikiana na mamlaka, kuwajibika ipasavyo, kuwa wenyeneyekevu, kutoa msaada unaotakiwa, kuhimizana na kushirikiana. Waebrania 13:17 watiini wenye kuwaongoza na kuwanyenyekea; maana  wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi. 1 Peter 2:13-15 Tiini kila kiamriwacho na watu,kwa ajili ya Bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipizia kisasiwatenda mabaya na kuwasifu watenda mema. Kwa sababundiyo mapenzi ya Mungu Kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu.

Mtazamo wetu kuhusu tukipatwa wakati Mgumu tunatakiwa kuwa wapole, watu wa kushukuru na kuamini kuwa hakuna linaloshindikana mbele ya Mungu. Warumi 8:28  Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake. Mungu anajua mitazamo yetu ndio maana kila mara anawatuma wajumbe wake ambao ni manabii katika kutuelekeza katika mitazamo iliyo bora: Yeramia 1: 17., 19 Haya Basi wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao; Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda maana; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana ili nikuokoe. Au alivyoongea na Ezekieli 2:7 Nawe utawaambia maneno yangu; kwamba watakusikia au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.

Tafakari ya leo inaendelea kutukumbusha kuwa tunatakiwa twende mbele ya Mungu na Mitazamo yenye, utii, unyenyekevu, adabu; ya kushukuru na yenye kuomba msamaha. Mungu pekee yake ambaye anatujua na tabia na mitazamo yetu ambayo iko mioyoni mwetu ambayo uzaa matendo mema au mabaya. Tunatakiwa kutembea katika njia ya bwana ya kumtii, na kutekeleza yale yote anayotuma kufanya au yale ambayo tayari yamekwisha ainishwa katika vitabu vyake na mafundisho yote ambayo Yesu alitufundisha.

Hii ndio tafakari yetu ya leo. Amina

Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment