WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, January 18, 2019

SIKU 18: AKISI YA IMANI

JANUARY 18:                  2019

WAEBRANIA 11:6

WAFILIPI 4:12-13

WAKATI WA MASHAKA  IMANI  THABITI INAHITAJIKA:

Somo letu leo tunakumbushwa kuwa wakati wa mashaka; tabu; wakati ambapo tunakabiliwa na sinto fahamu; tunatakiwa kuendelea kusimam imara kumwamini Mungu kama zaburi ya 23 inavyotukumbusha.

Imani iliyojaa Matendo Ndio iwe  kimbilio letu kwa Mungu na tukumbuke Mungu hutenda Kazi ndani ya wote wanao matumaini kwa imani wakati wowote ule wa maisha Yao:

Imani Yako ijae Matendo na kuamini kwa dhati kuwa Mungu ni mwanzo na mwisho wa kila Jambo katika mazingira yeyote yale:

Tujifunze hili Imani tunapoitenda kwa Matendo yatupasa kuhakikisha kuwa  pasiwepo yeyote wa kumwamini zaidi ya Nguvu ya Mungu:

Tumeona katika simulizi mbalimbali wale wote waliokubali kutembea kwenye kasi ya imani kwa kumtegemea Mungu  walifanikiwa sana.

Jiulize wewe sasa,ni nini kinachokupunguzia mwendo kasi wa kuamini katika imani na kufuata sheria za Mungu?

Usikubali mtu akupunguzie mwendo kasi wa utekelezaji wa imani yako kwa vitendo: Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Mfano mzuri ni kutoka kwa Yesu mwenyewe alipata mitihani mingi katika maisha yake ya utumishi: Siku zote alikuwa mshindi kwa sababu alimtumaini Mungu na kuishi kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu:

Shida yetu tumekuwa wepesi sio wa kuamini bali kujijengea hofu tunapokabiliwa na Matatizo: Mungu anakuwa sio kimbilio letu:

Hofu; hofu hututawala na kutufanya kukata tamaa mapema: Tuyakumbuke maneno ya Paulo kwa Wafilipi 4:12-13 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Tukiwa na Imani yetu thabiti kwa Mungu tutayaweza na kuyashinda yote:

Hili ndilo somo letu la leo Imani sahihi ni msingi wa mafanikio yetu yote:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Thursday, January 17, 2019

SIKU 17: AKISI YA IMANI

JANUARY 17.                        2019

HEKIMA YA KIMUNGU HUZAA IMANI BORA (2)

Tuanze na nasaa kutoka kwa Yakobo 3:13 N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

Tukumbuke kuwa hekima inakwenda zaidi ya elimu ya kawaida ni utaratibu ambao unatuwezesha sisi kuweza kutumia akili yetu na uwezo wetu wa kufikiri kuona na kuelewa ;

Angalisho maarifa na hekima itujengea Imani juu ya kumtambua Mungu na kutekeleza maagizo yake kwa vitendo; kama  Zaburi ya 111:10 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.
Vile vile Mithali 9:10 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu

Hekima iliyo bora tukumbuke inatoka kwa Mungu: Yakobo 3:17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Uwiii nimeipenda hii Ndio hekima tunayotakiwa kuiomba tuwe nayo;

Somo letu linatukumbusha kuwa hekima na Imani vinatakiwa viende pamoja: Ni ukweli ambao hauepukiki  kuwa hekima inatusaidia sisi kuelewa na kuweza kuitekeleza imani kwa ufasaha zaidi; kusikiliza sauti ya Mungu ni hekima na na kutenda Jambo ambalo hujeliona ni Imani :

Fundisho tunalipata pia kupitia Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; kuweza kuitenda Imani ni kujenga nyumba yako juu ya mwamba:

Tukumbuke kuwa kama Zaburi 19:7 Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia mjinga hekima. Ni kweli kuwa sheria nyingine za Mungu zinahitaji Imani zaidi Mfano mpende adui yako; utekelezaji wa sheria hii inahitaji Imani ya khali ya juu: umeshaumizwa lakini sheria inakutaka mpende huyu utapata thawabu tele: ikiwa na Imani na kuweza kutekeleza hili utapata thawabu ambayo haionekani: huijui Bado: Imani: Imani:

Kwa hiyo: Hekima uleta uelewa wa Jambo na Imani huleta uthubutu na kutenda: ni kweli kuwa Imani tamanio ambalo liko mbele yako ambalo halijekamilika au hujeliona lakini unaamini kuwa litakamilika kwa uwezo wa Mungu: Luka 18:22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate. Kwa nini alifhadhaika kwa sababu hakuwa na Imani thabiti kuweza kuyaishi maneno ya Yesu:

Tumkumbuke Daniel aliamini kwa Mungu wake na hata alipotupwa kwenye Shimo la simba alimwamini Mungu wake kuwa atakuwa salama na ikawa Hivyo: Daniel 6:22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.

Hekima ni Msingi mkubwa sana wa Imani Yetu: Mithali 19:8 Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Tukisoma pia
Methali 8: 34-35 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
35 Maana yeye anionaye mimi aona uzima, Naye atapata kibali kwa BWANA.

Tukumbuke  kuwa kibali kitapatikana kwa kutenda kupitia Imani: hekima huzaa imani ya kweli kama utaweza kuishi katika katika Msingi huu:

ukiwa na hekima daima utakuwa mnyenyekevu na mwenye kuonyesha tabia njema:

Utakuwa mtu wa Matendo mema:
Utakuwa mtu wa matendo mema:
Utakuwa mtu unayeweka mbele maslahi ya watu wengine na mbele:
Utakuwa mtu unayependa kuishi kwa amani na kuzuia kila dalili ya Matendo yanayo haribu amani:
Utakuwa mtu uliyejaa huruma: mpole;?mwema na uliyejaa msamaha:
Hekima itakuepusha na Unafiki: utakuwa mtu mkweli: mwaminifu: mtenda haki:

Kwa kutekeleza haya inajenga Imani ya kweli ya Matendo:

Tukamilishe somo letu kwa kauli Hii: Imani na hekima huenda sambamba na vyote vina mtegemea Mungu; Mithali 16:9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Wednesday, January 16, 2019

SIKU 16: AKISI YA IMANI

JANUARY16.                        2019

BUSARA NI MUHIMU KATIKA KUTEKELEZA IMANI (1)

Somo letu leo ebu tuangalie namna gani busara huimarisha Imani: sio tu Imani ya mapito ya Dunia bali Imani juu ya uwezo wa Mungu;

mtaalamu mmoja Albert Einstein. wakati mmoja alipokuwa akiendele na mihadhara yake alikuwa akitoa katika vyuo vikuu mbalimbali  kuhusu somo la theory yake ya relativity;

Einstein  pamoja na akili na busara zake hakuwa na leseni ya kuweza kuendesha gari hivyo alikuwa na dereva ambaye alikuwa akimzungusha wakati wote wa mihadhara katika vyuo mbalimbali;

Aliamini uwezo wa dereva wake na hakuwa na mashaka kabisa na uwezo wa dereva wake alimwamini kwa matendo yake: Imani ni Matendo:

Siku moja walipokuwa wakielekea katika moja ya mhadhara; dereva wake alimwambia kuwa unajua umekuwa nami kwa muda mrefu katika hii mihadhara  unajua kuwa mimi nimesikiliza midhara yako kwa muda mrefu:
Alimwambia Dr Einstein kuwa mimi ninaweza nikatoa mhadhara leo:

Dereva Alikuwa na Imani na kujiamini kuwa anao uwezo wa kufundisha:  Alitaka kuonyesha kwa vitendo: Imani bila Matendo inakuwa imekufa:

Dereva alijenga imani katika Jambo ambalo hajawahi fanya: lakini aliamini atafanikiwa: Einstein alicheka na kukubali kwa mashaka: Hakuwa na Imani kuwa anaweza kufanya Kazi katika ubora unaotakiwa: Hekima yake ikamsukuma akubali lakini imani yake ilikuwa haba:

Hatimaye alisema ngoja tujaribu kwani watu wa chuo hicho hawajewahi niona mimi hivyo hawatanifahamu nimefanana vipi;

Hivyo walikubaliana  dereva alivaa kama Dr. Einstein na Dr. Einstein akavaa nguo za dereva na kofia yake;
Walipofika alitambulishwa kuwa ni Dr. Einstein;

kila kitu kilikwenda vizuri sana kama walivyokuwa wamepanga; Dereva aliweza kutoa mhadhara vizuri sana kuhusu somo la relativity na Einstein  alikuwa amekaa nyuma akisikiliza; na kufurahia umahili wa dereva wake; lakini wakati akiendelea kutoa mhadhara mratibu wa mhadhara alisema kuwa bado walikuwa na dakika 15 zaidi hivyo ni muda ambao unatosha kumwuliza Dr Einstein swali; miongoni mwa watu ambao alikuwa amehudhuria alikuwa Profesa wa hesabu ambaye alimuuliza dr Einstein swali gumu kuhusu formula na lugha ambazo dereva hakuweza elewa kabisa;

Kitu kizuri dereva alikuwa mwepesi wa kufikiri na akamjibu profesa wa hesabu kuwa  suluhu la tatizo ambalo alikuwa ameuliza lilikuwa rahisi sana na alishangaa kwa nini ameuliza umeuliza swali kama hili; kwani kila mtu anaweza kujibu hili swali; hivyo nitamwambia dereva wangu aje hapa na kujibu swali hili; Busara na Imani vinapo fanya Kazi pamoja:

Kwa kuthibitisha hili ngoja sasa nimwite dereva wangu aweze kuja kujibu hili swali; kwa upande mmoja Dr Einstein alikuwa na akili lakini dereva wake alikuwa na mtu mwenye busara/hekima na Imani;

Tunachojifunza hapa kuwa daima tumekuwa hodari sana wa kuweza kuamini na kutenda kwa mambo ya kidunia: Tunatumia busara na Imani vizuri sana katika mambo siyo ya Kimungu

Wakati umefika sasa iwe ni Busara/Hekima na Imani viwe juu ya Mungu: tunapotamani kuimarisha busara na Imani Yetu iwe juu ya Mungu Baba : Mwana na Roho Mtakatifu:

Ni kweli kuwa wewe na mimi tunatamani kuwa na hekima; Tunafahamu kuwa kila siku tunakabiliwa na maamuzi ambayo yanahitaji uwezo wa ufikiri kwa haraka uliojaa busara na Imani:

Daima tunaomba hekima; tukumkuke kuwa sote tumejaliwa maarifa ;  maarifa ni uwezo unaotusaidia sisi kuweza kukusanya taarifa ili kuweza kufikia utatuzi wa shida ambayo iko mbele yetu; Bali tuombe hekima ya kimungu ili tuweze tekekeza Imani katika njia ya Kimungu:
Methali 18:15 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.

Ni ukweli kuwa hekima ni neema kutoka kwa Mungu; ni uwezo ambao unapata ili  Kuyaishi  maisha katika jicho la ukweli na kuitekeleza Imani katika vitendo:

Tuhitimishe somo letu tukiwaza zaidi kutafuta busara/hekima na Imani kwa kutenda vile Mungu anavyotaka Sisi tutende:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

SIKU 15: AKISI YA IMANI

JANUARY 15.                        2019

MTAZAMO WA YAKOBO JUU YA IMANI

Yakobo anaanza kwa kusema kuwa majaribu ni sehemu muhimu sana ya Imani yetu: Yakobo 1:3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

Ni kweli kabisa Imani yetu inapimwa kila siku kupitia matatizo; majaribu na wakati mwingine kupitia mazingira magumu : maamuzi yetu ya kweli na misimamo yetu ya maisha hasa juu ya Mungu ni utekelezaji wa Imani yetu katika mazingira magumu:

Tukiangalia maisha ya wote waliomwamini Mungu mpaka kufa kwao walipita katika mazingira magumu sana ya Imani: Ndio maana Yakobo 3:12 anasema Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Yakobo katika sura ya 3  alitukumbusha umuhimu wa kuamini na kutenda kwa kadiri ya mwongozo wa Mungu;

Tukiangalia katika lugha ya kiafya Imani ni sawa na calories huwezi kuziona bali unaona matokeo yake:
Yakobo ameongelea kuhusu Imani ya kweli ambayo tunatakiwa tuiangalie katika jicho Imani na sio katika jicho kielimu au kisayansi:

tukifanya hivyo basi tutaungana na maneno ya mzaburi 14:1  pale aliposema Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Hatutakiwi kuwa wapumbafu mbele ya Mungu: tunaposhindwa kutekeleza Imani kimatendo tunageuka kuwa wapumbafu mbele ya Mungu:

Msisitizo mkubwa wa Yakobo Imani ni matendo: imani yetu isitawaliwe na unafiki: Imani bila matendo inakuwa imekufa:

Jiulize leo kama wewe unajiona ni mtu wa kuamini kuhusu mafundisho na maagizo yote ya Mungu na ya mwokozi wetu Yesu Kristo je kipimo chako cha matendo ni kwa kiwango gani?

Matendo yako ya imani unatekeleza vipi amri ya upendo? Unampenda jirani yako? Je unasaidia yatima na wajane? Unawatembelea wagonjwa na wahitaji?
Haya ni maswali ya msingi katika kujifunza na kuishi katika imani ya Mungu:

Tukumbuke kuwa msingi wa imani yetu ni upendo na kutenda: Msingi wa Imani yetu ni kushika na kuziishi amri kumi za Mungu: kwa kufanya Hivyo unakuwa kiumbe kipya:

Paulo 2 Wakorinto 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Tukumbuke hata shetani anajua Kuna Mungu: Shetani anajua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu: kwa nini na wewe ambaye sio wa shetani usiamini Hivyo?

Yakobo 2:18-19 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Je ni Matendo gani yatathibitisha Imani yako? Yakobo anafafanua vizuri Jambo hili Yakobo 2:8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

Leo tuhitimishe somo letu kwa kuzingatia kanuni hii kubwa ya Imani:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Thursday, January 10, 2019

SIKU 9. AKISI YA IMANI

JANUARY 09.                        2019

UFAHAMU (ELIMU) NA IMANI

Hosea 4:6

Zaburi 46:10

Mtakatifu Agustino aliulizwa na watu ambao hawana imani walimwonyesha miungu yao na kumwambia huyu ndiye mungu wetu je wewe Mungu wako yuko wapi?

Agustino aliwaambia siwezi kuwaonyesha Mungu wangu sio kwamba hakuna Mungu bali sina Mungu wa kuwaonyesha ninyi kwa kuwa mna macho lakini humwoni yeye aliye yeye ;

Tunachojifunza hapa Hawana imani ya kumwona Mungu ambaye haonekani wala hugusiki kwa mikono Yetu:

Ugumu wa kutekeleza Imani uko wapi? Na kwa nini maneno ya Hosea ni muhimu katika kutekeleza Imani?

Leo tujikumbushe kuwa hakuna tendo ambalo linaweza kufanyika bila Imani na kujiaminisha: Tukumbuke imani isipofanya Kazi hakuna chochote amacho kinaweza fanyika: la Msingi tunahitaji sio tu imani bali Imani sahihi:
Ni imani iliyokuambia unaweza ruka hapa ndipo uanza kufanya kitendo cha kuruka, kutembea, na kadhalika: lazima ujijengee imani ya kutenda Jambo kwanza: Imani hutoa ruhusa ya Jambo kufanyika ni sawa na taa ya kijani inavyoruhusu magari kupita salama katika makutano ya barabara na kuweza kuzuia ajali:

Ndio maana Yesu aliokuwa anafanya miujiza alikuwa akisema sana Neno hili imani yako imekuponya: au imani yako iko wapi?  Kama mtaalamu mmoja alivyowahi sema: Lazima uwe na Imani ya kupokea baraka za Mungu: Imani ni msingi wa kila kitu katika maisha Yetu ya kufuata Yesu: Kwa hiyo kwa maneno ya mtaani tunaweza sema kuwa Imani Ndio ubuyu wa kila siku mtaani:

Imani ya kweli iliyojengwa katika msingi wa kimungu ikipungua Ndio mwanzo wa tatizo: Adamu na Hawa walianguka kwa sababu ya walikosa imani ya kuamini kuwa Mungu ndiye alikuwa sahihi na kimbilio lao la kweli na sio kiburi chao na shetani:

Pale tunapokosa imani ya kweli tunajiletea mashaka na tunaishia kufanya dhambi: Kila dhambi tunayoifanya ni kwa sababu hatuna imani na kuamini juu ya kuwa njia za Mungu ni sahihi zaidi:

Tuna mashaka kwa sababu hatuna imani kuwa Mungu atafanya Kazi katika kila jambo katika maisha Yetu: Tuna karibisha mashaka na hofu zichukue  furaha yetu na amani tukidhani kuwa Mungu hana nguvu ya kuyakabili matokeo hasi ya maisha yetu:

Matokeo yake kama wakristo ni anguko linasababishwa na ukosefu wa  Imani sahihi na kujitengenezea Imani iliyojaa mashaka: imani dhaifu: ni katika mazingira haya umuhimu wa Maarifa( elimu) ni muhimu sana sana katika maisha Yetu:
Ni kweli kabisa imani na ufahamu (elimu) Vina kwenda pamoja: elimu inakusaidia kuielewa zaidi Imani katika usahihi wake: Elimu au maarifa yatakusaidia Sisi kutekeleza imani kwa uhakika zaidi:

Ni sawa kabisa kama utaambiwa sasa hivi ebu twende tukapande bembea: kwanza utajiuliza maswali mengi ili uweze kupata kufahamu zaidi kuhusu bembea na kama ni ya umeme ndio kabisa: utataka upate ufahamu mkubwa kuhusu bembea kabla hujejiridhisha upande Hiyo bembea: ufahamu unahitajika na Imani ya kuamini na kisha kutenda ni lazima:

Ukiwa na ufahamu wa kutosha utakusaidia kuondoa mashaka na uwoga na kuifanya imani ifanye kazi yake kwa usahihi:

Ni kweli kabisa ufahamu unatusaidia sisi kujitambua na kuacha kufuata mambo ambayo yanaweza kututoa Sisi katika Imani hatarishi ya kupotea au kuangamia kwa upumbafu wetu: Ndio maana Hosea anasisitiza Watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa: Maarifa ya utambuzi: maarifa mazuri ya kufuata njia sahihi  ambayo haina mashaka:

Maarifa sio imani: ni ukweli kuwa Imani inahitaji maarifa kama chachu ya kuamini na kutenda: maarifa husaidia kuleta muafaka wa utekelezaji wa Jambo kupitia Imani: kama Paulo alivyosema: Paula alisema Imani bila Matendo ni Kazi bure:

Je wewe na mimi ni aina gani ya wakristo? Ukristo wetu umebeba Imani ya kiwango gani? Imani imara au tumekuwa wakristo wa Imani haba?

Tukumbuke bila imani thabiti ukristo wetu uko mashakani:

Je Wewe ni imara kama Imani yako: Kwetu kama wakristo kuwa imara ni uwezo wetu wa kumtegemea Mungu Baba; Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu;

Ni wakati wetu sasa tuwe na Imani kwa Mungu kumpigania Mungu kwa nguvu zote bila woga na kuamini kuwa Mungu ni kila kitu na kuiweka Imani juu ya kila kitu au mtu: Paulo na Titasi walivyoamua kumtumikia Mungu katika mazingira magumu ya kutisha lakini Mwisho walitambua kuwa Mungu ni kweli kabisa bila imani wasingeweza kumtumikia Mungu:

Tuhitimishe somo letu kwa maneno ya Paulo  ufahamu unatusaidia sisi kujifunza kutokana na yaliyopita yasasa na kupitia Imani inavileta vyote pamoja na hapo tunapoona nguvu ya Matendo mbele ya Mungu wetu:

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Wednesday, January 9, 2019

SIKU 8. AKISI YA IMANI

JANUARY 8.                        2019

YERAMIHA 31:16-17

1 PETRO 5: 7

KWA NINI UNANILILIA MIMI?

Tukumbuke kuwa Mungu anatujalia sisi tukifanikiwa kufanya uchaguzi sahihi wa mambo: tunapoweza kuchagua kuishi maisha yetu kulingana na neno lake: matarajio yake; na njia zake sahihi anatujalia sisi nguvu za ziada:

Kwa msingi tunakumbushwa umuhimu wa kuendelea kumtumaini Mungu katika kila jambo;

Imani yetu iwe imara katika nafasi ya kwanza:

Mashaka yanapo tusonga juu ya Imani Yetu hatutakiwi kukata tamaa na kuvunjika moyo Neno linakuja kwako kusema nawe; Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana. ndio maana

Yeramiha 31:16-17 anatukumbusha kuwa  “BWANA asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo BWANA. Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema BWANA;

Leo tunakumbushwa kuwa pale tunapolia kwa uchungu: tunapo lia kwa kukata tamaa na kujiona kutokufanikiwa tuna amua kwa makusudi kusimama mbali na imani ya kweli ya kumtumaini Mungu;

Leo tunahimizwa kulia kwa furaha tunaposifu kazi na ukuu wa Mungu kwani kulia kwa namna hii ni kulia ambako kumejaa imani na uzuri wake ni kuwa tunakuwa tunalia machozi ya furaha; machozi ya shukrani; machozi ya imani:

Tunakumbushwa kuzingatia kuendelea kuomba kwa Imani tunapokuja mbele za Mungu katika maombi: hatutakiwi kumwomba Mungu tukilalamika, tukinung’unika pamoja na kulia na kuomboleza kwingi.

Matendo ya aina hii ni dalili tosha ya kukosa imani. Waebrania 11:6 Hivyo pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.

Ni kweli kabisa imani inakupa ujasili na nguvu ya kuringa ukijua kuwa unafanikiwa; Waebrania 4: 16 tuje kwa ujasiri mbele ya kiti cha neema ili tupewe rehema na neema ya kutusaidia wakati wa uhitaji;
Tukiwa wajasili maombi yetu yana mpendeza Mungu naye hutubariki kulingana na mapenzi yake; Mungu hapendi sisi tulie lie bure bila sababu ya maana; 

Imani itakuondolea mashaka: Na mashaka hukuletea wewe kulialia maana maandiko yanasema zuia sauti yako usilie na macho yako yasitokwe machozi maana watarudi tena toka nchi ya adui.

Unapolia lia ovyo unamkaribisha shetani naye hukuongoza katika njia na mawazo mabaya; tuya kumbuke
maneno ya Yesu alipomwambia yule Mwanamke Mjane wa Naini akitoka kwenye lango la mji kwenda kumzika mwanae wa pekee alimwambia usilie.

Mwanamke mjane aliamini na kuondoa mashaka yake na kijana wake alifufuliwa:

Ni wakati sasa wa  wewe na mimi tuache kulia lia ovyo bali tumkimbilie Kristo na shida zetu kama Barua ya

1 Petro 5: 7 inasema umtwike Mungu fadhaa zako maana anajishughulisha mno na mambo yako;

Tukumbuke kuwa tunapolia na Imani tumepewa ya kujiamini ili tutende na kupata majibu tunazuia nguvu ambayo iko ndani yetu ya kutenda miujiza: tunatakiwa kuwa jasili:

Tumkumbuke Musa alimlilia Mungu 
Mungu anamuuliza Musa mbona unanililia  mimi? Mungu akamwambia Musa Mbona unaniomba mimi wakati una kila kitu cha kutatua tatizo lako: Mungu alimpa Musa fimbo ambayo ilikuwa ni mwongozo na msaada katika safari yao nzima.

Ndipo alipomwambia inua fimbo yako. Na itakupa jibu la shida yako:

Je sisi tunapomlilia Mungu tunajua nini Mungu ametukabidhi sisi ili tuweze kushinda shida na matatizo ambayo yako mbele yetu?
Yatupasa kuamini na kuishi katika imani ya kweli tukiamini kuwa Mungu atatuvusha salama katika matatizo yetu yote;

Somo letu leo linatukumbusha  kuwa huu sio wakati wa kulia ni wakati wa kutambua ni silaha gani Mungu ametujalia sisi ili itusaidie wakati wa shida zetu; tuwe imara; tuwe shupavu kuondoa mashaka ambayo yanatufanya sisi  kulia lia ovyo.

Tujivike Imani; Imani iwe ngao yetu na msaada wetu:

Amina Amina Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Tuesday, January 8, 2019

SIKU 7. AKISI YA IMANI

JANUARY.  7              2019

WAEBRANIA 11:6

Warumi 11:8 – 19

Yakobo 2: 14-26

TUNAMPENDEZAJE MUNGU

Lazima tukubali kuwa bila Imani hatuwezi mpendeza Mungu: Tukiweza kuishi katika imani tujue wazi tunampendeza Mungu:

Ukristo wetu umejengwa chini ya msingi imara wa Imani: na msingi huo ni wewe na mimi: kwa kuwa msingi bora wa Imani ndipo tunaweza
Kupata kibali na baraka kutoka kwa Mungu juu ya maisha yetu: kwa nini tunapata kibali? Kwa sababu tumeamini: kama Paulo anavyosema:
Waebrania 11: 16 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Kama nilivyosema katika masomo yaliyopita kuwa kuwa kuna njia mbili ambazo ni msingi wa maisha yetu;  kwa kuona (sight) ambayo ndio njia iliyozoeleka sana; kila kitu msingi wake unakuwa ni kwa kuona;

Na njia ya pili ni kwa imani hii msingi wake kila kitu msingi wake ni imani; na kuamini katika vitu ambavyo havionekani; hii ndio njia ya Mkristo wa kweli kuamini ukuu wa Mungu na matendo yake: huu Ndio msingi wa ukristo wetu:

Kwa imani Abeli alimwabudu Mungu; kwa imani Enoki alitembea na Mungu na kwa Imani Noha aliweza kufanya kazi na Mungu;

Maisha ya imani yanaanza utayari wa kukubali mwito wa Mungu; Mwito wa kwanza ni kuacha dhambi; na hatua ya pili ni kukubali maelekezo ya Mungu bila kuwa na mashaka:

Kwa Imani Abramu aliitikia wito wa Mungu wa kwenda nchi ambayo Mungu alitaka yeye aweze kwenda: tunaona utayari  wa Abramu kuacha kila kitu ambacho alikuwa nancho na kwa macho ya imani kukubali kwendakwenye nchi mpya;

Kuishi kwa imani ni sawa na kuendesha gari katikati ya ukungu mzito kwani hujui hata wapi unakwenda; lakini unajiamini na unaendelea kuendesha; na ukiamini kuwa ukungu utakwisha mara moja na utaanza kuona vizuri; hivyo ndivyo kuishi kwa imani:

Abramu lisubiri kwa unyenyekevu ahadi ya Mungu iweze kutimia; kitu kikubwa katika imani ni kusubiri; tukumbuke kuwa muda ambao tunasubiri kabwe hautaweza kupotea bure; ni wajibu wetu kuondoa mashaka

Ni kweli kabisa Mungu anaweza kutujaribu sisi kwa namna tofauti sana na kutupitisha katika tanuri la Moto lakini siku zote tukiwa na Imani thabiti ambayo inahitaji matendo haitaruhusu mashaka kama Yakobo 2: 14-26 inavyotufundisha;

Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa:

Jambo la msingi katika kujenga imani ni kuondoa mashaka na kuamini: Mungu atatumia kila kitu katika maisha yako kukufanya wewe uwe Karibu naye: Mashaka na woga  haviwezi ushinda msingi imara ambao unaujenga ndani yako:

Ukristo wetu ukijengwa katika msingi imara wa Imani hakuna chochote cha kutushinda: mashaka na majaribu juu ya imani yetu na juu ya Mungu wetu lazima vitajitokeza kwa nguvu: lakini haviwezi shinda kama msingi wake ni imara:

Tunapo hitimisha somo letu leo jiulize swali la msingi wewe ni imara katika IMANI au wewe ni vuguvugu katika IMANI?

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Monday, January 7, 2019

SIKU 6: AKISI YA IMANI

JANUARY 6.         2019

FUNZO  KUTOKA KWA ABRAMU

Lengo la Mungu ni kutuongoza sisi katika mwelekeo mzuri katika maisha Yetu na ametujalia Sisi zawadi ya Imani kama dira ya kufuata:

Jambo la msingi ambalo lazima tulikumbuke ni kuwa dira yetu sio njia iliyonyoka:

Tukumbuke kuwa kadiri tunavyo songa mbele katika njia hiyo ndivyo tunavyo kutana na vikwazo ambavyo vinapima imani yetu mbele ya Mungu:

Mara nyingi katika vikwazo hivi tunaanza kukata tamaa  na kuacha kumwamini Mungu na kuanza kutegemea akili zetu wenyewe:
Tuna amua kubadilisha mwelekeo na kupuuza mwongozo wa Mungu kupitia imani na kukaribisha mashaka na woga kuchukua nafasi ya zaidi ya Imani:
 
Abramu ni mfano wa mtu ambaye imani yake ilikumbwa na hofu pamoja na Mungu kumpa maelekezo na ahadi nzito na Nzuri kama tunavyo soma katika:

Mwanzo 12:1-3 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;

2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Ni kweli kabisa katika Imani na utii Abramu aliweza kuacha makazi yake na kwenda nchi ya ahadi kanani kama alivyokuwa amehaidiwa na Mungu’

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu BWANA aliyemtokea.

Mungu alitaka Abramu aweke masikani kanani: kutokana na matatizo Abramu aliona Kanani sio mahala pazuri pa kuishi akatunga na uwongo pia ili aweze kupikelewa Misri hii ilikuwa Safari yake binafsi kwa sababu Kanani kulikuwa na njaa:

Ni kweli kabisa kama Abramu angeweza kutimiza maelekezo ya Mungu katika Safari yake yote na kufanya makazi kama Mungu alivyomwagiza na kumwabudu yeye Mungu angemlinda na kumpatia mahitaji yake:

Alichokiona Abramu ilikuwa ni ukame na njaa Imani yake ilijaa mashaka: Mungu kwake ilikuwa sio kipimo tena kwa wakati huu:

Leo sote tunakumbushwa kuwa kubadilika kwa mazingira: hali ya kiuchumi isiwe  sababu ya msingi kuacha kumwamini Mungu:

Leo tusiwe kama Abramu tuhakikishe kuwa tukipata mwongozo wa Mungu tuutekeleze mpaka Mwisho bila kutafuta sababu na wala mazingira yasiwe na nafasi ya kubadilisha Imani kuwa mashaka au woga: mazingira na akili zetu zisiwe sababu ya kupoteza imani yetu kwa Mungu: Bali viwe vitu vya kutujenga Sisi:

Abramu alifikiri kuwa kwa kwenda Misri  ilikuwa ni jibu sahihi la kukwepa njaa: Alisahau kuwa alikuwa amepoteza Imani mbele ya Mungu:

Mara nyingi tunasahau kuwa Mungu wetu yeye ni mlinzi wetu na mpaji wa Riziki zetu za kila siku:

Mara nyingi tunajiona kuwa sisi ndio wenye mamlaka zaidi ya Mungu:

Abramu alitakiwa kubaki katika Mungu na kubaki kanani pamoja na mashaka yake yote yaliyo mpata: Wajibu wake ulitakiwa kuendelea kumtumaini Mungu na kuiweka Imani yake juu ya Mungu:

Mungu alikuwa na mpango mzuri na Abramu : hata Leo sisi tunaendelea kusahau kuwa Mungu ni kila kitu kwetu  na ana mpango mzuri Kwetu ni wajibu wetu kuendelea kumwamini:

Mpango ambao utashindwa mbele ya Mungu: Tukumbuke kuwa Mungu hayuko karibu na wenye kiburi bali hufanya Kazi na wanyenyekevu wenye Imani ya kweli :

Hilo ndilo somo letu la leo kuhusu Imani: Imani yako imeendelea kukua katika mashaka ??

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Sunday, January 6, 2019

SIKU 5: AKISI YA IMANI

JANUARY 5.        2019

WARUMI 4

Mungu anajua kuwa Sisi ni Watu wa mashaka: umeshaona hata akina mama wakati mwingine wanawaonea mashaka watoto wao:

Mtoto kifanya kosa ambalo pengine mama halijemfurajisha ataanza kushanga na kusema kwa hasira kweli huyu ni mwanangu?

Ndio maana Mungu daima anajua kuwa sisi ni Watu wa mashaka;

Je kama una matatizo katika maisha Yako una amini kuwa Mungu anaweza kuyamaliza?

Je unamwamini Yesu?

Kama unaamini kwa nini uwe na mashaka: Ni wakati sahihi kuyaleta mashaka yako mbele ya  Yesu:

Hebu leo tumwangalie baba yetu Ibrahim alipewa ahadi na Mungu kuwa baba wa mataifa: Alijiangalia hali yake na ya mkeo Sara alijawa na mashaka na alijiuliza maswali mengi yaliyo ongeza mashaka:

Je unafikiria brahim alichaguliwa kwa sababu gani kuwa baba wa mataifa? Ni kwa sababu ya Matendo yake mazuri? Au Imani yake pamoja na mashaka yake?

Tukisoma warumi 4: 3 Maana maandiko yanatupa Sisi jibu;

Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.

Kubwa hapa Aliweza amini uwezo wa Mungu usio onekana na kuyaweka mashaka yake pembeni:

Leo yatupasa tuwe kama Ibrahim tuwe watu wa kuamini uwezo wa Mungu hata katika mazingira magumu;

kama Warumi 4:18 inavyotukumbusha 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Je wewe na Mimi katika shida zetu tunaweza kuweka mashaka yetu pembeni na kumwamini Mungu kupitia bwana wetu Yesu Kristo kuwa ni mweza wa yote hasa yale ambayo yanaonekana kushindikana kabisa Kwetu:

Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa mashaka hayazidi nguvu ya Imani: na ili kulishinda hili tuepuke kujiuliza maswali ambayo hutapata majibu bali yatakuongezea mashaka zaidi: ni wakati wa kutumia msemo huu Mimi sijui ila Mungu anajua: kama Zaburi ya 139:1-3 Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.

Baba yetu Ibrahim alilielewa hili Ndio maana mashaka yake hayakuweza kushinda imani yake:

Je sisi Leo tunaweza kuiga tabia hii;
ya kumwachia Mungu atende  ndani yetu?  Je leo sisi tunaweza kuondoka mashaka na kuamini kwa dhati ili nasi tuhesabiwe wenye haki? 

Warumi 4: 20-21 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; 21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

Basi tuhitimishe somo letu Leo kwa kuzingatia Jambo moja ili kuhesabiwa wenye haki mbele ya Mungu mashaka yetu yasizidi Imani yetu: Imani ni funguo pekee wa kutimiza ahadi ya Mungu ili tuhesabiwe haki;

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

SIKU 4; AKISI YA IMANI

JANUARY 4

JE TUNAISHI KATIKA MASHAKA

Ni Jambo ambalo halikwepeki kabisa kuhusu masha katika imani na katika maisha Yetu ya ya kila SIKu kama nilivyoeleza kidogo katika maelezo yaliyotangulia: kwa upande mwingine mashaka huchochea imani:

Tukisoma kitabu cha Mhubiri: Maombolezo: Habakuki na Zaburi tunaoma mashaka ambayo watumishi wa Mungu walikuwa wakiyapitia:

Lakini hata nasi katika maisha yetu ya kila siku tunaishi katika mashaka makubwa: Maswali kama:

je nimefanya uchaguzi sahihi?
Je Jambo hili nimelifanya ipasavyo?
Je nguo hii naihitaji au niirusdishe dukani?

Tuna mashaka kuhusu jambo ambalo liko mbele yetu mashaka yaliyojaa woga;

Tuna mashaka kuhusu watu wengine juu ya maisha yetu suspicion.

Tuna mashaka juu ya maisha Yetu ya kutojiamini na kujitoa thamani wenyewe:

Tuna mashaka juu ya kila kitu  katika maisha Yetu (skepticism).

Tuna mashaka juu ya Mungu Bado akili yetu haijeweza kuacha kudadisi kuhusu ukuu na uweza wa Mungu.
(uncertainty).

Yaani maisha Yetu ni mashaka mashaka tu:

Yesu alimwambia Tomaso mwenye imani haba: Yesu alijua kuwa Tomaso anaimani na anaamini lakini imani yake ilijengwa katika mashaka: Imani yake ilijengwa katika kuona kwanza:

Ndio maana wengi wetu Imani yetu imejengwa katika msingi wa Tomaso: ni imani ambayo imezungukwa na mashaka: na ni kweli kuwa mashaka sio kinyume cha imani; ila kutoamini ni kunyume cha imani. Mashaka ni kutokuwa na uhakika: kupata ugumu katika maamuzi:

Waebu 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Ni kweli mashaka ni sehemu ya kuifikia imani; hii yote inatokana na ukweli kuwa binadamu tunakosa ushupavu wa kumwamini Mungu na maagizo yote yanayo husiana na Imani: katika maisha yetu ni rahisi kabisa na kuwa na uhakika wa 2+2=4: je jibu hili linaweza badilisha maisha au kusudi lako la maisha? Tuendelee kutembea pamoja katika Safari hii ya Imani:

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
49009

Friday, January 4, 2019

SIKU 3: AKISI YA IMANI

JANUARY 3.              2019

IMANI NA MASHAKA VINAPO NGONGANA

MARKO 9: 14-24

WAEBRANIA  12:1

Kama tulivyoona katika masomo yaliyopita kuwa Imani hufanya Kazi yake vizuri sana pale ambapo mashaka hakuna :

Mashaka ni adui mkubwa sana wa Imani: Lakini Imani ya kibibilia inahimili mashaka;

Tukumbuke kuwa Mungu anapenda Sisi kumtumaini yeye katika kila jambo katika maisha Yetu yote: Hivyo hata katika mashaka Mungu Bado anatuopoa sisi kama alivyomwopoa Petro:

Tukisoma Mathayo 14: 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

Tukumbuke kitendo cha Petro kuyaangalia maji na dhoruba yalimjengea mashaka; Lakini tukubali ukweli huu Kitendo cha Petro kushuka kutoka kwenye mashua na kuwa tayari kutembea juu ya maji ni uwepo wa imani ya kweli mbele ya Yesu :

Tukumbuke kuwa mashaka kama yaliyompata Petro sio kuwa Petro alikuwa hana Imani kabisa isipokuwa imani yake ilitoweka kufuatia mazingira ambayo yalikuwa mbele yake baada ya kupoteza umakini wa wapi aangalie na nani amemwambia ashuke kwenye Chimborazo:

Kwa kupoteza mwelekeo akaanza kuzama: Mathayo 14:31 Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Wengi wetu tuko kwenye kundi la Petro na ukristo wetu: la kutoamini katika njia inayotakiwa ya kuamini kuanzia mwanzo wa tukio mpaka Mwisho wake:

Tumkumbuke Tomaso hakuamini kuwa Yesu amefufuka na amewatokea mitume wenzake: Sio kuwa Tomaso alikuwa hajui nguvu za Yesu lakini mazingira ambayo Yesu alikufa na kuzikwa yalimpa wasiwasi mkubwa hata alipopata taarifa kuwa amefufuka na wamemwona hakuweza amini:

Tomaso aliona jinsi Yesu alivyokuwa alifanya miujiza yote ile lakini Bado alikuwa amejawa na mashaka tunakumuka jinsi Yesu alivyomwambia Tomaso tukisoma; Yohana 20:27 Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye.

Tukumbuke kuwa kuamini ni rahisi sana lakini kuishi katika uhalisia wa kuamini ni kazi nzito: wakati mwingine nafasi katika jamii: uwezo wa kifedha; uwezo wa maarifa na kadhalika unaweza kubomoa Imani yako kama Mkristo:

Methali 3:5–6. Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

Kumweka mashaka katika ukristo wetu ni kujirudisha nyuma katika imani ambayo Mungu kaiweka kwetu kupitia Mwanae Yesu Kristo: Ndio maana katika Injili ya Yohana Yesu anaongelea sana Imani Imani Imani;

Yesu anataka Sisi tutue mzigo mzito tulioubeba ulioja mashaka; Anataka Sisi tumwamini Yeye; Ndio maana amesisitiza sana kuwa Yeye ni njia na uzima: yeye ni maji ya uzima: Yeye ni mkate wa uzima na kadhalika;

Leo tuamue kuwa  ni wakati umefika wa kutua huu mizigo mzito wa mashaka: Mashaka katika imani isiwe kikwazo katika Mbio za kutenda miujiza: tumtumiini yeye naye atakuwa nasi: Waebrania 12:2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Tukumbuke kuwa hatuwezi kuishi Imani ya ukristo kama hata Mungu tunamwonea mashaka; Leo jiangalie wewe kama Mkristo ambaye mkono wa Mungu umekubariki na kukupitisha katika Magumu mengi na kukupatia faraja: na Bado baada ya kuvushwa na kupata Mafanikio Bado wamekuwa na mashaka na Mungu:

Ni wajibu wetu Leo kuipokea Imani na kuishi ili tuweze kutenda Kazi ya Mungu Kwa uhakika wote na kuweza kufanya miujiza:

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
2019

Thursday, January 3, 2019

AKISI YA IMANI -

JANUARY 2.        2019

LUKA 17: 5-6

UKIWA NA IMANI THABITI WEWE NI MSHINDI

Tabia moja kubwa ya imani iko kwenye dhana ya kushinda: Imani daima huwa na tabia ya kuwa chanya; hii ni nguvu ambayo Mungu ametujalia lakini kutokana na uninadamu wetu tunashindwa kuitumia nguvu hii; ambayo Mungu ameweka ndani yetu:

Ebu tuangalie nguvu kama ya uponyaji iko ndani yetu lakini inavigezo ambavyo lazima tuvikamilishe ili iweze fanya Kazi ipasavyo;

Kwa Maneno mengine silaha kubwa ambayo tumejaliwa kama Wakristo ni IMANI: ambayo inaonyesha ukuu wa Mungu wetu; ukuu wa Bwana wetu Yesu Kristo na Ukuu wa Roho Mtakatifu

Kwa msingi huu Imani ni silaha moja muhimu sana katika ulimwengu huu uliojaa maovu;

Ndio maana unapokuwa na Imani kwa Mungu wewe jihesabie kuwa ni Mshindi; Mwenjili Marko  11: 22-23 alithibitisha  hili aliposema:
Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. 23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. 

Nguvu tuliyopewa ni kubwa sana lakini hatujui jinsi ya kuitumia: ili tuweze kuitumia vizuri tunahitaji kutokuwa na mashaka: Yatupasa kuwa wanyenyekevu; hata katika mashaka yetu tukiweza kujinyenyekeza na kufuata nini Mungu anataka sisi tuwe lazima tutapata ushindi:

Kwa msingi huu ukiwa na Imani thabiti Mungu hukupa wewe nguvu ya ushindi  ya kuweza kutenda lolote njema kwako na kwa wengine:

Tujikumbushe juu ya watumishi wa Mungu Ibrahimu, Yosefu; Musa, Daudi , Yohana , Paulo na wengine wengi walikuwa na mashaka Yao katika maisha ambayo yalikuwa kikwazo baada ya kujinyenyekeza na kuipokea  imani ya kweli na kutimiza maagizo ya Mungu waliishia kuwa washindi:
Na sifa nyingine waliyopata kutokana na kuamini na kuishi kwa imani waliitwa watoto wa Mungu;

Ikiwa na imani huogopi kitu unatenda kwa kadiri inavyokupasa kutenda kama Paulo anavyosema 2 Timothy 1:12; Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.

Imani inahitaji uthabiti: Tatizo ambalo liko ni imani ya binadamu ambayo hubadilika badilika kufuatia jinsi mtu anavyojisikia na ukubwa wa tatizo analokabiliwa nalo:

Changamoto yetu kubwa Sisi binadamu ni kweli kabisa wakati binadamu anapopatwa na matatizo imani yake hushuka na wakati anavyo kuwa katika Mafanikio Imani yake huwa juu sana;

Kinyume chake Mungu  ni yule yule katika wakati wote: Hivyo wajibu wetu tunatakiwa tuombe katika mazingira yote: tukijua kuwa Mungu wetu ni mkubwa kuliko matatizo yetu; kama alivyoagiza;

Yakobo 1:6-8. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

Ni kweli kabisa Mungu kupitia Imani anakuwa ngome kwa wale wote wanaoamini: na pale tunapokuwa na mashaka juu ya neno lake au kulibadilisha lilingane na jinsi sisi tunavyotaka hapo tunapoteza nguvu ya Imani

Tutaendelea Kesho na asante sana kuungana Nami katika siku ya 2 ya Safari yetu ya siku 365

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
2019

Wednesday, January 2, 2019

AKISI YA IMANI

SIKU 1: JANUARY 1, 2019

Waebrania 11:1,3

Warumi 10:17

Kheri ya Mwaka mpya 2019:  Leo naomba kuwakaribisha katika mwendelezo wa siku nyingine 365 ambapo tutaangalia Akisi ya Imani katika maisha yetu kama wakristo;

Imani ndio msingi wa kwanza wa mkristo

Imani ina umuhimu mkubwa katika maisha Yetu ya kiroho kama mkristo

Imani ni muhimu sana katika kuimarisha sheria ya Mungu. Na kwa upande mwingine Kufuata amri za Mungu ndiyo njia bora ya kujenga imani yetu

Mtitiriko wake ni kuwa Tunapoishi kulingana na amri hizo, tunaona wazi zaidi kwamba zina mwongozo wenye upendo ambao ni kielelezo cha imani:

Mtume Paulo katika Waebrania 11:1,3 anasema kuwa Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

Jambo la pili imani huhusisha usikivu kama Paulo anavyotukumbusha katika
Warumi 10:17, chanzo cha imani ni kusikia. Imani katika Kristo inakuja kwa kusikia:

Je unapenda kusikia Habari Za kristo au Habari za shetani:

Tunakumbuka tukisoma Mwanzo 3:1-8 jinsi nguvu ya kusikia ilivyo haribu nguvu na baraka zote walizopata
Adam na Hawa katika bustani ya Edeni.

Huu ni utangulizi tu katika Safari yetu ya Akisi ya Imani kwa mwaka huu 2019:

Kama utakuwa na nafasi Karibu sana nitaweza kukutumia mfululizo huu:

Na kama hutakuwa na nafasi katika Safari hii ya kiroho:

Nawatakieni kheri na fanaka kwa kuvuka salama mkiwa na afya njema;

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
2019