JANUARY 5. 2019
WARUMI 4
Mungu anajua kuwa Sisi ni Watu wa mashaka: umeshaona hata akina mama wakati mwingine wanawaonea mashaka watoto wao:
Mtoto kifanya kosa ambalo pengine mama halijemfurajisha ataanza kushanga na kusema kwa hasira kweli huyu ni mwanangu?
Ndio maana Mungu daima anajua kuwa sisi ni Watu wa mashaka;
Je kama una matatizo katika maisha Yako una amini kuwa Mungu anaweza kuyamaliza?
Je unamwamini Yesu?
Kama unaamini kwa nini uwe na mashaka: Ni wakati sahihi kuyaleta mashaka yako mbele ya Yesu:
Hebu leo tumwangalie baba yetu Ibrahim alipewa ahadi na Mungu kuwa baba wa mataifa: Alijiangalia hali yake na ya mkeo Sara alijawa na mashaka na alijiuliza maswali mengi yaliyo ongeza mashaka:
Je unafikiria brahim alichaguliwa kwa sababu gani kuwa baba wa mataifa? Ni kwa sababu ya Matendo yake mazuri? Au Imani yake pamoja na mashaka yake?
Tukisoma warumi 4: 3 Maana maandiko yanatupa Sisi jibu;
Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
Kubwa hapa Aliweza amini uwezo wa Mungu usio onekana na kuyaweka mashaka yake pembeni:
Leo yatupasa tuwe kama Ibrahim tuwe watu wa kuamini uwezo wa Mungu hata katika mazingira magumu;
kama Warumi 4:18 inavyotukumbusha 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
Je wewe na Mimi katika shida zetu tunaweza kuweka mashaka yetu pembeni na kumwamini Mungu kupitia bwana wetu Yesu Kristo kuwa ni mweza wa yote hasa yale ambayo yanaonekana kushindikana kabisa Kwetu:
Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa mashaka hayazidi nguvu ya Imani: na ili kulishinda hili tuepuke kujiuliza maswali ambayo hutapata majibu bali yatakuongezea mashaka zaidi: ni wakati wa kutumia msemo huu Mimi sijui ila Mungu anajua: kama Zaburi ya 139:1-3 Ee BWANA, umenichunguza na kunijua.2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
Baba yetu Ibrahim alilielewa hili Ndio maana mashaka yake hayakuweza kushinda imani yake:
Je sisi Leo tunaweza kuiga tabia hii;
ya kumwachia Mungu atende ndani yetu? Je leo sisi tunaweza kuondoka mashaka na kuamini kwa dhati ili nasi tuhesabiwe wenye haki?
Warumi 4: 20-21 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; 21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
Basi tuhitimishe somo letu Leo kwa kuzingatia Jambo moja ili kuhesabiwa wenye haki mbele ya Mungu mashaka yetu yasizidi Imani yetu: Imani ni funguo pekee wa kutimiza ahadi ya Mungu ili tuhesabiwe haki;
Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019
No comments:
Post a Comment