WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, January 16, 2019

SIKU 15: AKISI YA IMANI

JANUARY 15.                        2019

MTAZAMO WA YAKOBO JUU YA IMANI

Yakobo anaanza kwa kusema kuwa majaribu ni sehemu muhimu sana ya Imani yetu: Yakobo 1:3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

Ni kweli kabisa Imani yetu inapimwa kila siku kupitia matatizo; majaribu na wakati mwingine kupitia mazingira magumu : maamuzi yetu ya kweli na misimamo yetu ya maisha hasa juu ya Mungu ni utekelezaji wa Imani yetu katika mazingira magumu:

Tukiangalia maisha ya wote waliomwamini Mungu mpaka kufa kwao walipita katika mazingira magumu sana ya Imani: Ndio maana Yakobo 3:12 anasema Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Yakobo katika sura ya 3  alitukumbusha umuhimu wa kuamini na kutenda kwa kadiri ya mwongozo wa Mungu;

Tukiangalia katika lugha ya kiafya Imani ni sawa na calories huwezi kuziona bali unaona matokeo yake:
Yakobo ameongelea kuhusu Imani ya kweli ambayo tunatakiwa tuiangalie katika jicho Imani na sio katika jicho kielimu au kisayansi:

tukifanya hivyo basi tutaungana na maneno ya mzaburi 14:1  pale aliposema Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Hatutakiwi kuwa wapumbafu mbele ya Mungu: tunaposhindwa kutekeleza Imani kimatendo tunageuka kuwa wapumbafu mbele ya Mungu:

Msisitizo mkubwa wa Yakobo Imani ni matendo: imani yetu isitawaliwe na unafiki: Imani bila matendo inakuwa imekufa:

Jiulize leo kama wewe unajiona ni mtu wa kuamini kuhusu mafundisho na maagizo yote ya Mungu na ya mwokozi wetu Yesu Kristo je kipimo chako cha matendo ni kwa kiwango gani?

Matendo yako ya imani unatekeleza vipi amri ya upendo? Unampenda jirani yako? Je unasaidia yatima na wajane? Unawatembelea wagonjwa na wahitaji?
Haya ni maswali ya msingi katika kujifunza na kuishi katika imani ya Mungu:

Tukumbuke kuwa msingi wa imani yetu ni upendo na kutenda: Msingi wa Imani yetu ni kushika na kuziishi amri kumi za Mungu: kwa kufanya Hivyo unakuwa kiumbe kipya:

Paulo 2 Wakorinto 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Tukumbuke hata shetani anajua Kuna Mungu: Shetani anajua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu: kwa nini na wewe ambaye sio wa shetani usiamini Hivyo?

Yakobo 2:18-19 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Je ni Matendo gani yatathibitisha Imani yako? Yakobo anafafanua vizuri Jambo hili Yakobo 2:8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

Leo tuhitimishe somo letu kwa kuzingatia kanuni hii kubwa ya Imani:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

No comments:

Post a Comment