JANUARY 8. 2019
YERAMIHA 31:16-17
1 PETRO 5: 7
KWA NINI UNANILILIA MIMI?
Tukumbuke kuwa Mungu anatujalia sisi tukifanikiwa kufanya uchaguzi sahihi wa mambo: tunapoweza kuchagua kuishi maisha yetu kulingana na neno lake: matarajio yake; na njia zake sahihi anatujalia sisi nguvu za ziada:
Kwa msingi tunakumbushwa umuhimu wa kuendelea kumtumaini Mungu katika kila jambo;
Imani yetu iwe imara katika nafasi ya kwanza:
Mashaka yanapo tusonga juu ya Imani Yetu hatutakiwi kukata tamaa na kuvunjika moyo Neno linakuja kwako kusema nawe; Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana. ndio maana
Yeramiha 31:16-17 anatukumbusha kuwa “BWANA asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo BWANA. Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema BWANA;
Leo tunakumbushwa kuwa pale tunapolia kwa uchungu: tunapo lia kwa kukata tamaa na kujiona kutokufanikiwa tuna amua kwa makusudi kusimama mbali na imani ya kweli ya kumtumaini Mungu;
Leo tunahimizwa kulia kwa furaha tunaposifu kazi na ukuu wa Mungu kwani kulia kwa namna hii ni kulia ambako kumejaa imani na uzuri wake ni kuwa tunakuwa tunalia machozi ya furaha; machozi ya shukrani; machozi ya imani:
Tunakumbushwa kuzingatia kuendelea kuomba kwa Imani tunapokuja mbele za Mungu katika maombi: hatutakiwi kumwomba Mungu tukilalamika, tukinung’unika pamoja na kulia na kuomboleza kwingi.
Matendo ya aina hii ni dalili tosha ya kukosa imani. Waebrania 11:6 Hivyo pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.
Ni kweli kabisa imani inakupa ujasili na nguvu ya kuringa ukijua kuwa unafanikiwa; Waebrania 4: 16 tuje kwa ujasiri mbele ya kiti cha neema ili tupewe rehema na neema ya kutusaidia wakati wa uhitaji;
Tukiwa wajasili maombi yetu yana mpendeza Mungu naye hutubariki kulingana na mapenzi yake; Mungu hapendi sisi tulie lie bure bila sababu ya maana;
Imani itakuondolea mashaka: Na mashaka hukuletea wewe kulialia maana maandiko yanasema zuia sauti yako usilie na macho yako yasitokwe machozi maana watarudi tena toka nchi ya adui.
Unapolia lia ovyo unamkaribisha shetani naye hukuongoza katika njia na mawazo mabaya; tuya kumbuke
maneno ya Yesu alipomwambia yule Mwanamke Mjane wa Naini akitoka kwenye lango la mji kwenda kumzika mwanae wa pekee alimwambia usilie.
Mwanamke mjane aliamini na kuondoa mashaka yake na kijana wake alifufuliwa:
Ni wakati sasa wa wewe na mimi tuache kulia lia ovyo bali tumkimbilie Kristo na shida zetu kama Barua ya
1 Petro 5: 7 inasema umtwike Mungu fadhaa zako maana anajishughulisha mno na mambo yako;
Tukumbuke kuwa tunapolia na Imani tumepewa ya kujiamini ili tutende na kupata majibu tunazuia nguvu ambayo iko ndani yetu ya kutenda miujiza: tunatakiwa kuwa jasili:
Tumkumbuke Musa alimlilia Mungu
Mungu anamuuliza Musa mbona unanililia mimi? Mungu akamwambia Musa Mbona unaniomba mimi wakati una kila kitu cha kutatua tatizo lako: Mungu alimpa Musa fimbo ambayo ilikuwa ni mwongozo na msaada katika safari yao nzima.
Ndipo alipomwambia inua fimbo yako. Na itakupa jibu la shida yako:
Je sisi tunapomlilia Mungu tunajua nini Mungu ametukabidhi sisi ili tuweze kushinda shida na matatizo ambayo yako mbele yetu?
Yatupasa kuamini na kuishi katika imani ya kweli tukiamini kuwa Mungu atatuvusha salama katika matatizo yetu yote;
Somo letu leo linatukumbusha kuwa huu sio wakati wa kulia ni wakati wa kutambua ni silaha gani Mungu ametujalia sisi ili itusaidie wakati wa shida zetu; tuwe imara; tuwe shupavu kuondoa mashaka ambayo yanatufanya sisi kulia lia ovyo.
Tujivike Imani; Imani iwe ngao yetu na msaada wetu:
Amina Amina Amina
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019
No comments:
Post a Comment