WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, January 10, 2019

SIKU 9. AKISI YA IMANI

JANUARY 09.                        2019

UFAHAMU (ELIMU) NA IMANI

Hosea 4:6

Zaburi 46:10

Mtakatifu Agustino aliulizwa na watu ambao hawana imani walimwonyesha miungu yao na kumwambia huyu ndiye mungu wetu je wewe Mungu wako yuko wapi?

Agustino aliwaambia siwezi kuwaonyesha Mungu wangu sio kwamba hakuna Mungu bali sina Mungu wa kuwaonyesha ninyi kwa kuwa mna macho lakini humwoni yeye aliye yeye ;

Tunachojifunza hapa Hawana imani ya kumwona Mungu ambaye haonekani wala hugusiki kwa mikono Yetu:

Ugumu wa kutekeleza Imani uko wapi? Na kwa nini maneno ya Hosea ni muhimu katika kutekeleza Imani?

Leo tujikumbushe kuwa hakuna tendo ambalo linaweza kufanyika bila Imani na kujiaminisha: Tukumbuke imani isipofanya Kazi hakuna chochote amacho kinaweza fanyika: la Msingi tunahitaji sio tu imani bali Imani sahihi:
Ni imani iliyokuambia unaweza ruka hapa ndipo uanza kufanya kitendo cha kuruka, kutembea, na kadhalika: lazima ujijengee imani ya kutenda Jambo kwanza: Imani hutoa ruhusa ya Jambo kufanyika ni sawa na taa ya kijani inavyoruhusu magari kupita salama katika makutano ya barabara na kuweza kuzuia ajali:

Ndio maana Yesu aliokuwa anafanya miujiza alikuwa akisema sana Neno hili imani yako imekuponya: au imani yako iko wapi?  Kama mtaalamu mmoja alivyowahi sema: Lazima uwe na Imani ya kupokea baraka za Mungu: Imani ni msingi wa kila kitu katika maisha Yetu ya kufuata Yesu: Kwa hiyo kwa maneno ya mtaani tunaweza sema kuwa Imani Ndio ubuyu wa kila siku mtaani:

Imani ya kweli iliyojengwa katika msingi wa kimungu ikipungua Ndio mwanzo wa tatizo: Adamu na Hawa walianguka kwa sababu ya walikosa imani ya kuamini kuwa Mungu ndiye alikuwa sahihi na kimbilio lao la kweli na sio kiburi chao na shetani:

Pale tunapokosa imani ya kweli tunajiletea mashaka na tunaishia kufanya dhambi: Kila dhambi tunayoifanya ni kwa sababu hatuna imani na kuamini juu ya kuwa njia za Mungu ni sahihi zaidi:

Tuna mashaka kwa sababu hatuna imani kuwa Mungu atafanya Kazi katika kila jambo katika maisha Yetu: Tuna karibisha mashaka na hofu zichukue  furaha yetu na amani tukidhani kuwa Mungu hana nguvu ya kuyakabili matokeo hasi ya maisha yetu:

Matokeo yake kama wakristo ni anguko linasababishwa na ukosefu wa  Imani sahihi na kujitengenezea Imani iliyojaa mashaka: imani dhaifu: ni katika mazingira haya umuhimu wa Maarifa( elimu) ni muhimu sana sana katika maisha Yetu:
Ni kweli kabisa imani na ufahamu (elimu) Vina kwenda pamoja: elimu inakusaidia kuielewa zaidi Imani katika usahihi wake: Elimu au maarifa yatakusaidia Sisi kutekeleza imani kwa uhakika zaidi:

Ni sawa kabisa kama utaambiwa sasa hivi ebu twende tukapande bembea: kwanza utajiuliza maswali mengi ili uweze kupata kufahamu zaidi kuhusu bembea na kama ni ya umeme ndio kabisa: utataka upate ufahamu mkubwa kuhusu bembea kabla hujejiridhisha upande Hiyo bembea: ufahamu unahitajika na Imani ya kuamini na kisha kutenda ni lazima:

Ukiwa na ufahamu wa kutosha utakusaidia kuondoa mashaka na uwoga na kuifanya imani ifanye kazi yake kwa usahihi:

Ni kweli kabisa ufahamu unatusaidia sisi kujitambua na kuacha kufuata mambo ambayo yanaweza kututoa Sisi katika Imani hatarishi ya kupotea au kuangamia kwa upumbafu wetu: Ndio maana Hosea anasisitiza Watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa: Maarifa ya utambuzi: maarifa mazuri ya kufuata njia sahihi  ambayo haina mashaka:

Maarifa sio imani: ni ukweli kuwa Imani inahitaji maarifa kama chachu ya kuamini na kutenda: maarifa husaidia kuleta muafaka wa utekelezaji wa Jambo kupitia Imani: kama Paulo alivyosema: Paula alisema Imani bila Matendo ni Kazi bure:

Je wewe na mimi ni aina gani ya wakristo? Ukristo wetu umebeba Imani ya kiwango gani? Imani imara au tumekuwa wakristo wa Imani haba?

Tukumbuke bila imani thabiti ukristo wetu uko mashakani:

Je Wewe ni imara kama Imani yako: Kwetu kama wakristo kuwa imara ni uwezo wetu wa kumtegemea Mungu Baba; Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu;

Ni wakati wetu sasa tuwe na Imani kwa Mungu kumpigania Mungu kwa nguvu zote bila woga na kuamini kuwa Mungu ni kila kitu na kuiweka Imani juu ya kila kitu au mtu: Paulo na Titasi walivyoamua kumtumikia Mungu katika mazingira magumu ya kutisha lakini Mwisho walitambua kuwa Mungu ni kweli kabisa bila imani wasingeweza kumtumikia Mungu:

Tuhitimishe somo letu kwa maneno ya Paulo  ufahamu unatusaidia sisi kujifunza kutokana na yaliyopita yasasa na kupitia Imani inavileta vyote pamoja na hapo tunapoona nguvu ya Matendo mbele ya Mungu wetu:

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

No comments:

Post a Comment