JANUARY. 7 2019
WAEBRANIA 11:6
Warumi 11:8 – 19
Yakobo 2: 14-26
TUNAMPENDEZAJE MUNGU
Lazima tukubali kuwa bila Imani hatuwezi mpendeza Mungu: Tukiweza kuishi katika imani tujue wazi tunampendeza Mungu:
Ukristo wetu umejengwa chini ya msingi imara wa Imani: na msingi huo ni wewe na mimi: kwa kuwa msingi bora wa Imani ndipo tunaweza
Kupata kibali na baraka kutoka kwa Mungu juu ya maisha yetu: kwa nini tunapata kibali? Kwa sababu tumeamini: kama Paulo anavyosema:
Waebrania 11: 16 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Kama nilivyosema katika masomo yaliyopita kuwa kuwa kuna njia mbili ambazo ni msingi wa maisha yetu; kwa kuona (sight) ambayo ndio njia iliyozoeleka sana; kila kitu msingi wake unakuwa ni kwa kuona;
Na njia ya pili ni kwa imani hii msingi wake kila kitu msingi wake ni imani; na kuamini katika vitu ambavyo havionekani; hii ndio njia ya Mkristo wa kweli kuamini ukuu wa Mungu na matendo yake: huu Ndio msingi wa ukristo wetu:
Kwa imani Abeli alimwabudu Mungu; kwa imani Enoki alitembea na Mungu na kwa Imani Noha aliweza kufanya kazi na Mungu;
Maisha ya imani yanaanza utayari wa kukubali mwito wa Mungu; Mwito wa kwanza ni kuacha dhambi; na hatua ya pili ni kukubali maelekezo ya Mungu bila kuwa na mashaka:
Kwa Imani Abramu aliitikia wito wa Mungu wa kwenda nchi ambayo Mungu alitaka yeye aweze kwenda: tunaona utayari wa Abramu kuacha kila kitu ambacho alikuwa nancho na kwa macho ya imani kukubali kwendakwenye nchi mpya;
Kuishi kwa imani ni sawa na kuendesha gari katikati ya ukungu mzito kwani hujui hata wapi unakwenda; lakini unajiamini na unaendelea kuendesha; na ukiamini kuwa ukungu utakwisha mara moja na utaanza kuona vizuri; hivyo ndivyo kuishi kwa imani:
Abramu lisubiri kwa unyenyekevu ahadi ya Mungu iweze kutimia; kitu kikubwa katika imani ni kusubiri; tukumbuke kuwa muda ambao tunasubiri kabwe hautaweza kupotea bure; ni wajibu wetu kuondoa mashaka
Ni kweli kabisa Mungu anaweza kutujaribu sisi kwa namna tofauti sana na kutupitisha katika tanuri la Moto lakini siku zote tukiwa na Imani thabiti ambayo inahitaji matendo haitaruhusu mashaka kama Yakobo 2: 14-26 inavyotufundisha;
Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa:
Jambo la msingi katika kujenga imani ni kuondoa mashaka na kuamini: Mungu atatumia kila kitu katika maisha yako kukufanya wewe uwe Karibu naye: Mashaka na woga haviwezi ushinda msingi imara ambao unaujenga ndani yako:
Ukristo wetu ukijengwa katika msingi imara wa Imani hakuna chochote cha kutushinda: mashaka na majaribu juu ya imani yetu na juu ya Mungu wetu lazima vitajitokeza kwa nguvu: lakini haviwezi shinda kama msingi wake ni imara:
Tunapo hitimisha somo letu leo jiulize swali la msingi wewe ni imara katika IMANI au wewe ni vuguvugu katika IMANI?
Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019
No comments:
Post a Comment