JANUARY 2. 2019
LUKA 17: 5-6
UKIWA NA IMANI THABITI WEWE NI MSHINDI
Tabia moja kubwa ya imani iko kwenye dhana ya kushinda: Imani daima huwa na tabia ya kuwa chanya; hii ni nguvu ambayo Mungu ametujalia lakini kutokana na uninadamu wetu tunashindwa kuitumia nguvu hii; ambayo Mungu ameweka ndani yetu:
Ebu tuangalie nguvu kama ya uponyaji iko ndani yetu lakini inavigezo ambavyo lazima tuvikamilishe ili iweze fanya Kazi ipasavyo;
Kwa Maneno mengine silaha kubwa ambayo tumejaliwa kama Wakristo ni IMANI: ambayo inaonyesha ukuu wa Mungu wetu; ukuu wa Bwana wetu Yesu Kristo na Ukuu wa Roho Mtakatifu
Kwa msingi huu Imani ni silaha moja muhimu sana katika ulimwengu huu uliojaa maovu;
Ndio maana unapokuwa na Imani kwa Mungu wewe jihesabie kuwa ni Mshindi; Mwenjili Marko 11: 22-23 alithibitisha hili aliposema:
Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. 23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
Nguvu tuliyopewa ni kubwa sana lakini hatujui jinsi ya kuitumia: ili tuweze kuitumia vizuri tunahitaji kutokuwa na mashaka: Yatupasa kuwa wanyenyekevu; hata katika mashaka yetu tukiweza kujinyenyekeza na kufuata nini Mungu anataka sisi tuwe lazima tutapata ushindi:
Kwa msingi huu ukiwa na Imani thabiti Mungu hukupa wewe nguvu ya ushindi ya kuweza kutenda lolote njema kwako na kwa wengine:
Tujikumbushe juu ya watumishi wa Mungu Ibrahimu, Yosefu; Musa, Daudi , Yohana , Paulo na wengine wengi walikuwa na mashaka Yao katika maisha ambayo yalikuwa kikwazo baada ya kujinyenyekeza na kuipokea imani ya kweli na kutimiza maagizo ya Mungu waliishia kuwa washindi:
Na sifa nyingine waliyopata kutokana na kuamini na kuishi kwa imani waliitwa watoto wa Mungu;
Ikiwa na imani huogopi kitu unatenda kwa kadiri inavyokupasa kutenda kama Paulo anavyosema 2 Timothy 1:12; Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, wala sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.
Imani inahitaji uthabiti: Tatizo ambalo liko ni imani ya binadamu ambayo hubadilika badilika kufuatia jinsi mtu anavyojisikia na ukubwa wa tatizo analokabiliwa nalo:
Changamoto yetu kubwa Sisi binadamu ni kweli kabisa wakati binadamu anapopatwa na matatizo imani yake hushuka na wakati anavyo kuwa katika Mafanikio Imani yake huwa juu sana;
Kinyume chake Mungu ni yule yule katika wakati wote: Hivyo wajibu wetu tunatakiwa tuombe katika mazingira yote: tukijua kuwa Mungu wetu ni mkubwa kuliko matatizo yetu; kama alivyoagiza;
Yakobo 1:6-8. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.
Ni kweli kabisa Mungu kupitia Imani anakuwa ngome kwa wale wote wanaoamini: na pale tunapokuwa na mashaka juu ya neno lake au kulibadilisha lilingane na jinsi sisi tunavyotaka hapo tunapoteza nguvu ya Imani
Tutaendelea Kesho na asante sana kuungana Nami katika siku ya 2 ya Safari yetu ya siku 365
🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI
2019
No comments:
Post a Comment