WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, January 17, 2019

SIKU 17: AKISI YA IMANI

JANUARY 17.                        2019

HEKIMA YA KIMUNGU HUZAA IMANI BORA (2)

Tuanze na nasaa kutoka kwa Yakobo 3:13 N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

Tukumbuke kuwa hekima inakwenda zaidi ya elimu ya kawaida ni utaratibu ambao unatuwezesha sisi kuweza kutumia akili yetu na uwezo wetu wa kufikiri kuona na kuelewa ;

Angalisho maarifa na hekima itujengea Imani juu ya kumtambua Mungu na kutekeleza maagizo yake kwa vitendo; kama  Zaburi ya 111:10 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.
Vile vile Mithali 9:10 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu

Hekima iliyo bora tukumbuke inatoka kwa Mungu: Yakobo 3:17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Uwiii nimeipenda hii Ndio hekima tunayotakiwa kuiomba tuwe nayo;

Somo letu linatukumbusha kuwa hekima na Imani vinatakiwa viende pamoja: Ni ukweli ambao hauepukiki  kuwa hekima inatusaidia sisi kuelewa na kuweza kuitekeleza imani kwa ufasaha zaidi; kusikiliza sauti ya Mungu ni hekima na na kutenda Jambo ambalo hujeliona ni Imani :

Fundisho tunalipata pia kupitia Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; kuweza kuitenda Imani ni kujenga nyumba yako juu ya mwamba:

Tukumbuke kuwa kama Zaburi 19:7 Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia mjinga hekima. Ni kweli kuwa sheria nyingine za Mungu zinahitaji Imani zaidi Mfano mpende adui yako; utekelezaji wa sheria hii inahitaji Imani ya khali ya juu: umeshaumizwa lakini sheria inakutaka mpende huyu utapata thawabu tele: ikiwa na Imani na kuweza kutekeleza hili utapata thawabu ambayo haionekani: huijui Bado: Imani: Imani:

Kwa hiyo: Hekima uleta uelewa wa Jambo na Imani huleta uthubutu na kutenda: ni kweli kuwa Imani tamanio ambalo liko mbele yako ambalo halijekamilika au hujeliona lakini unaamini kuwa litakamilika kwa uwezo wa Mungu: Luka 18:22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate. Kwa nini alifhadhaika kwa sababu hakuwa na Imani thabiti kuweza kuyaishi maneno ya Yesu:

Tumkumbuke Daniel aliamini kwa Mungu wake na hata alipotupwa kwenye Shimo la simba alimwamini Mungu wake kuwa atakuwa salama na ikawa Hivyo: Daniel 6:22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.

Hekima ni Msingi mkubwa sana wa Imani Yetu: Mithali 19:8 Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Tukisoma pia
Methali 8: 34-35 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
35 Maana yeye anionaye mimi aona uzima, Naye atapata kibali kwa BWANA.

Tukumbuke  kuwa kibali kitapatikana kwa kutenda kupitia Imani: hekima huzaa imani ya kweli kama utaweza kuishi katika katika Msingi huu:

ukiwa na hekima daima utakuwa mnyenyekevu na mwenye kuonyesha tabia njema:

Utakuwa mtu wa Matendo mema:
Utakuwa mtu wa matendo mema:
Utakuwa mtu unayeweka mbele maslahi ya watu wengine na mbele:
Utakuwa mtu unayependa kuishi kwa amani na kuzuia kila dalili ya Matendo yanayo haribu amani:
Utakuwa mtu uliyejaa huruma: mpole;?mwema na uliyejaa msamaha:
Hekima itakuepusha na Unafiki: utakuwa mtu mkweli: mwaminifu: mtenda haki:

Kwa kutekeleza haya inajenga Imani ya kweli ya Matendo:

Tukamilishe somo letu kwa kauli Hii: Imani na hekima huenda sambamba na vyote vina mtegemea Mungu; Mithali 16:9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

No comments:

Post a Comment