WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, January 18, 2019

SIKU 18: AKISI YA IMANI

JANUARY 18:                  2019

WAEBRANIA 11:6

WAFILIPI 4:12-13

WAKATI WA MASHAKA  IMANI  THABITI INAHITAJIKA:

Somo letu leo tunakumbushwa kuwa wakati wa mashaka; tabu; wakati ambapo tunakabiliwa na sinto fahamu; tunatakiwa kuendelea kusimam imara kumwamini Mungu kama zaburi ya 23 inavyotukumbusha.

Imani iliyojaa Matendo Ndio iwe  kimbilio letu kwa Mungu na tukumbuke Mungu hutenda Kazi ndani ya wote wanao matumaini kwa imani wakati wowote ule wa maisha Yao:

Imani Yako ijae Matendo na kuamini kwa dhati kuwa Mungu ni mwanzo na mwisho wa kila Jambo katika mazingira yeyote yale:

Tujifunze hili Imani tunapoitenda kwa Matendo yatupasa kuhakikisha kuwa  pasiwepo yeyote wa kumwamini zaidi ya Nguvu ya Mungu:

Tumeona katika simulizi mbalimbali wale wote waliokubali kutembea kwenye kasi ya imani kwa kumtegemea Mungu  walifanikiwa sana.

Jiulize wewe sasa,ni nini kinachokupunguzia mwendo kasi wa kuamini katika imani na kufuata sheria za Mungu?

Usikubali mtu akupunguzie mwendo kasi wa utekelezaji wa imani yako kwa vitendo: Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Mfano mzuri ni kutoka kwa Yesu mwenyewe alipata mitihani mingi katika maisha yake ya utumishi: Siku zote alikuwa mshindi kwa sababu alimtumaini Mungu na kuishi kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu:

Shida yetu tumekuwa wepesi sio wa kuamini bali kujijengea hofu tunapokabiliwa na Matatizo: Mungu anakuwa sio kimbilio letu:

Hofu; hofu hututawala na kutufanya kukata tamaa mapema: Tuyakumbuke maneno ya Paulo kwa Wafilipi 4:12-13 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Tukiwa na Imani yetu thabiti kwa Mungu tutayaweza na kuyashinda yote:

Hili ndilo somo letu la leo Imani sahihi ni msingi wa mafanikio yetu yote:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Thursday, January 17, 2019

SIKU 17: AKISI YA IMANI

JANUARY 17.                        2019

HEKIMA YA KIMUNGU HUZAA IMANI BORA (2)

Tuanze na nasaa kutoka kwa Yakobo 3:13 N’nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aonyeshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima.

Tukumbuke kuwa hekima inakwenda zaidi ya elimu ya kawaida ni utaratibu ambao unatuwezesha sisi kuweza kutumia akili yetu na uwezo wetu wa kufikiri kuona na kuelewa ;

Angalisho maarifa na hekima itujengea Imani juu ya kumtambua Mungu na kutekeleza maagizo yake kwa vitendo; kama  Zaburi ya 111:10 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele.
Vile vile Mithali 9:10 Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu

Hekima iliyo bora tukumbuke inatoka kwa Mungu: Yakobo 3:17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Uwiii nimeipenda hii Ndio hekima tunayotakiwa kuiomba tuwe nayo;

Somo letu linatukumbusha kuwa hekima na Imani vinatakiwa viende pamoja: Ni ukweli ambao hauepukiki  kuwa hekima inatusaidia sisi kuelewa na kuweza kuitekeleza imani kwa ufasaha zaidi; kusikiliza sauti ya Mungu ni hekima na na kutenda Jambo ambalo hujeliona ni Imani :

Fundisho tunalipata pia kupitia Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; kuweza kuitenda Imani ni kujenga nyumba yako juu ya mwamba:

Tukumbuke kuwa kama Zaburi 19:7 Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia mjinga hekima. Ni kweli kuwa sheria nyingine za Mungu zinahitaji Imani zaidi Mfano mpende adui yako; utekelezaji wa sheria hii inahitaji Imani ya khali ya juu: umeshaumizwa lakini sheria inakutaka mpende huyu utapata thawabu tele: ikiwa na Imani na kuweza kutekeleza hili utapata thawabu ambayo haionekani: huijui Bado: Imani: Imani:

Kwa hiyo: Hekima uleta uelewa wa Jambo na Imani huleta uthubutu na kutenda: ni kweli kuwa Imani tamanio ambalo liko mbele yako ambalo halijekamilika au hujeliona lakini unaamini kuwa litakamilika kwa uwezo wa Mungu: Luka 18:22 Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate. Kwa nini alifhadhaika kwa sababu hakuwa na Imani thabiti kuweza kuyaishi maneno ya Yesu:

Tumkumbuke Daniel aliamini kwa Mungu wake na hata alipotupwa kwenye Shimo la simba alimwamini Mungu wake kuwa atakuwa salama na ikawa Hivyo: Daniel 6:22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.

Hekima ni Msingi mkubwa sana wa Imani Yetu: Mithali 19:8 Apataye hekima hujipenda nafsi yake; Ashikaye ufahamu atapata mema. Tukisoma pia
Methali 8: 34-35 Ana heri mtu yule anisikilizaye, Akisubiri sikuzote malangoni pangu, Akingoja penye vizingiti vya milango yangu.
35 Maana yeye anionaye mimi aona uzima, Naye atapata kibali kwa BWANA.

Tukumbuke  kuwa kibali kitapatikana kwa kutenda kupitia Imani: hekima huzaa imani ya kweli kama utaweza kuishi katika katika Msingi huu:

ukiwa na hekima daima utakuwa mnyenyekevu na mwenye kuonyesha tabia njema:

Utakuwa mtu wa Matendo mema:
Utakuwa mtu wa matendo mema:
Utakuwa mtu unayeweka mbele maslahi ya watu wengine na mbele:
Utakuwa mtu unayependa kuishi kwa amani na kuzuia kila dalili ya Matendo yanayo haribu amani:
Utakuwa mtu uliyejaa huruma: mpole;?mwema na uliyejaa msamaha:
Hekima itakuepusha na Unafiki: utakuwa mtu mkweli: mwaminifu: mtenda haki:

Kwa kutekeleza haya inajenga Imani ya kweli ya Matendo:

Tukamilishe somo letu kwa kauli Hii: Imani na hekima huenda sambamba na vyote vina mtegemea Mungu; Mithali 16:9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake.

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Wednesday, January 16, 2019

SIKU 16: AKISI YA IMANI

JANUARY16.                        2019

BUSARA NI MUHIMU KATIKA KUTEKELEZA IMANI (1)

Somo letu leo ebu tuangalie namna gani busara huimarisha Imani: sio tu Imani ya mapito ya Dunia bali Imani juu ya uwezo wa Mungu;

mtaalamu mmoja Albert Einstein. wakati mmoja alipokuwa akiendele na mihadhara yake alikuwa akitoa katika vyuo vikuu mbalimbali  kuhusu somo la theory yake ya relativity;

Einstein  pamoja na akili na busara zake hakuwa na leseni ya kuweza kuendesha gari hivyo alikuwa na dereva ambaye alikuwa akimzungusha wakati wote wa mihadhara katika vyuo mbalimbali;

Aliamini uwezo wa dereva wake na hakuwa na mashaka kabisa na uwezo wa dereva wake alimwamini kwa matendo yake: Imani ni Matendo:

Siku moja walipokuwa wakielekea katika moja ya mhadhara; dereva wake alimwambia kuwa unajua umekuwa nami kwa muda mrefu katika hii mihadhara  unajua kuwa mimi nimesikiliza midhara yako kwa muda mrefu:
Alimwambia Dr Einstein kuwa mimi ninaweza nikatoa mhadhara leo:

Dereva Alikuwa na Imani na kujiamini kuwa anao uwezo wa kufundisha:  Alitaka kuonyesha kwa vitendo: Imani bila Matendo inakuwa imekufa:

Dereva alijenga imani katika Jambo ambalo hajawahi fanya: lakini aliamini atafanikiwa: Einstein alicheka na kukubali kwa mashaka: Hakuwa na Imani kuwa anaweza kufanya Kazi katika ubora unaotakiwa: Hekima yake ikamsukuma akubali lakini imani yake ilikuwa haba:

Hatimaye alisema ngoja tujaribu kwani watu wa chuo hicho hawajewahi niona mimi hivyo hawatanifahamu nimefanana vipi;

Hivyo walikubaliana  dereva alivaa kama Dr. Einstein na Dr. Einstein akavaa nguo za dereva na kofia yake;
Walipofika alitambulishwa kuwa ni Dr. Einstein;

kila kitu kilikwenda vizuri sana kama walivyokuwa wamepanga; Dereva aliweza kutoa mhadhara vizuri sana kuhusu somo la relativity na Einstein  alikuwa amekaa nyuma akisikiliza; na kufurahia umahili wa dereva wake; lakini wakati akiendelea kutoa mhadhara mratibu wa mhadhara alisema kuwa bado walikuwa na dakika 15 zaidi hivyo ni muda ambao unatosha kumwuliza Dr Einstein swali; miongoni mwa watu ambao alikuwa amehudhuria alikuwa Profesa wa hesabu ambaye alimuuliza dr Einstein swali gumu kuhusu formula na lugha ambazo dereva hakuweza elewa kabisa;

Kitu kizuri dereva alikuwa mwepesi wa kufikiri na akamjibu profesa wa hesabu kuwa  suluhu la tatizo ambalo alikuwa ameuliza lilikuwa rahisi sana na alishangaa kwa nini ameuliza umeuliza swali kama hili; kwani kila mtu anaweza kujibu hili swali; hivyo nitamwambia dereva wangu aje hapa na kujibu swali hili; Busara na Imani vinapo fanya Kazi pamoja:

Kwa kuthibitisha hili ngoja sasa nimwite dereva wangu aweze kuja kujibu hili swali; kwa upande mmoja Dr Einstein alikuwa na akili lakini dereva wake alikuwa na mtu mwenye busara/hekima na Imani;

Tunachojifunza hapa kuwa daima tumekuwa hodari sana wa kuweza kuamini na kutenda kwa mambo ya kidunia: Tunatumia busara na Imani vizuri sana katika mambo siyo ya Kimungu

Wakati umefika sasa iwe ni Busara/Hekima na Imani viwe juu ya Mungu: tunapotamani kuimarisha busara na Imani Yetu iwe juu ya Mungu Baba : Mwana na Roho Mtakatifu:

Ni kweli kuwa wewe na mimi tunatamani kuwa na hekima; Tunafahamu kuwa kila siku tunakabiliwa na maamuzi ambayo yanahitaji uwezo wa ufikiri kwa haraka uliojaa busara na Imani:

Daima tunaomba hekima; tukumkuke kuwa sote tumejaliwa maarifa ;  maarifa ni uwezo unaotusaidia sisi kuweza kukusanya taarifa ili kuweza kufikia utatuzi wa shida ambayo iko mbele yetu; Bali tuombe hekima ya kimungu ili tuweze tekekeza Imani katika njia ya Kimungu:
Methali 18:15 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.

Ni ukweli kuwa hekima ni neema kutoka kwa Mungu; ni uwezo ambao unapata ili  Kuyaishi  maisha katika jicho la ukweli na kuitekeleza Imani katika vitendo:

Tuhitimishe somo letu tukiwaza zaidi kutafuta busara/hekima na Imani kwa kutenda vile Mungu anavyotaka Sisi tutende:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

SIKU 15: AKISI YA IMANI

JANUARY 15.                        2019

MTAZAMO WA YAKOBO JUU YA IMANI

Yakobo anaanza kwa kusema kuwa majaribu ni sehemu muhimu sana ya Imani yetu: Yakobo 1:3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

Ni kweli kabisa Imani yetu inapimwa kila siku kupitia matatizo; majaribu na wakati mwingine kupitia mazingira magumu : maamuzi yetu ya kweli na misimamo yetu ya maisha hasa juu ya Mungu ni utekelezaji wa Imani yetu katika mazingira magumu:

Tukiangalia maisha ya wote waliomwamini Mungu mpaka kufa kwao walipita katika mazingira magumu sana ya Imani: Ndio maana Yakobo 3:12 anasema Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.

Yakobo katika sura ya 3  alitukumbusha umuhimu wa kuamini na kutenda kwa kadiri ya mwongozo wa Mungu;

Tukiangalia katika lugha ya kiafya Imani ni sawa na calories huwezi kuziona bali unaona matokeo yake:
Yakobo ameongelea kuhusu Imani ya kweli ambayo tunatakiwa tuiangalie katika jicho Imani na sio katika jicho kielimu au kisayansi:

tukifanya hivyo basi tutaungana na maneno ya mzaburi 14:1  pale aliposema Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Hatutakiwi kuwa wapumbafu mbele ya Mungu: tunaposhindwa kutekeleza Imani kimatendo tunageuka kuwa wapumbafu mbele ya Mungu:

Msisitizo mkubwa wa Yakobo Imani ni matendo: imani yetu isitawaliwe na unafiki: Imani bila matendo inakuwa imekufa:

Jiulize leo kama wewe unajiona ni mtu wa kuamini kuhusu mafundisho na maagizo yote ya Mungu na ya mwokozi wetu Yesu Kristo je kipimo chako cha matendo ni kwa kiwango gani?

Matendo yako ya imani unatekeleza vipi amri ya upendo? Unampenda jirani yako? Je unasaidia yatima na wajane? Unawatembelea wagonjwa na wahitaji?
Haya ni maswali ya msingi katika kujifunza na kuishi katika imani ya Mungu:

Tukumbuke kuwa msingi wa imani yetu ni upendo na kutenda: Msingi wa Imani yetu ni kushika na kuziishi amri kumi za Mungu: kwa kufanya Hivyo unakuwa kiumbe kipya:

Paulo 2 Wakorinto 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Tukumbuke hata shetani anajua Kuna Mungu: Shetani anajua kuwa Yesu ni mwana wa Mungu: kwa nini na wewe ambaye sio wa shetani usiamini Hivyo?

Yakobo 2:18-19 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Je ni Matendo gani yatathibitisha Imani yako? Yakobo anafafanua vizuri Jambo hili Yakobo 2:8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

Leo tuhitimishe somo letu kwa kuzingatia kanuni hii kubwa ya Imani:

🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏👏

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Thursday, January 10, 2019

SIKU 9. AKISI YA IMANI

JANUARY 09.                        2019

UFAHAMU (ELIMU) NA IMANI

Hosea 4:6

Zaburi 46:10

Mtakatifu Agustino aliulizwa na watu ambao hawana imani walimwonyesha miungu yao na kumwambia huyu ndiye mungu wetu je wewe Mungu wako yuko wapi?

Agustino aliwaambia siwezi kuwaonyesha Mungu wangu sio kwamba hakuna Mungu bali sina Mungu wa kuwaonyesha ninyi kwa kuwa mna macho lakini humwoni yeye aliye yeye ;

Tunachojifunza hapa Hawana imani ya kumwona Mungu ambaye haonekani wala hugusiki kwa mikono Yetu:

Ugumu wa kutekeleza Imani uko wapi? Na kwa nini maneno ya Hosea ni muhimu katika kutekeleza Imani?

Leo tujikumbushe kuwa hakuna tendo ambalo linaweza kufanyika bila Imani na kujiaminisha: Tukumbuke imani isipofanya Kazi hakuna chochote amacho kinaweza fanyika: la Msingi tunahitaji sio tu imani bali Imani sahihi:
Ni imani iliyokuambia unaweza ruka hapa ndipo uanza kufanya kitendo cha kuruka, kutembea, na kadhalika: lazima ujijengee imani ya kutenda Jambo kwanza: Imani hutoa ruhusa ya Jambo kufanyika ni sawa na taa ya kijani inavyoruhusu magari kupita salama katika makutano ya barabara na kuweza kuzuia ajali:

Ndio maana Yesu aliokuwa anafanya miujiza alikuwa akisema sana Neno hili imani yako imekuponya: au imani yako iko wapi?  Kama mtaalamu mmoja alivyowahi sema: Lazima uwe na Imani ya kupokea baraka za Mungu: Imani ni msingi wa kila kitu katika maisha Yetu ya kufuata Yesu: Kwa hiyo kwa maneno ya mtaani tunaweza sema kuwa Imani Ndio ubuyu wa kila siku mtaani:

Imani ya kweli iliyojengwa katika msingi wa kimungu ikipungua Ndio mwanzo wa tatizo: Adamu na Hawa walianguka kwa sababu ya walikosa imani ya kuamini kuwa Mungu ndiye alikuwa sahihi na kimbilio lao la kweli na sio kiburi chao na shetani:

Pale tunapokosa imani ya kweli tunajiletea mashaka na tunaishia kufanya dhambi: Kila dhambi tunayoifanya ni kwa sababu hatuna imani na kuamini juu ya kuwa njia za Mungu ni sahihi zaidi:

Tuna mashaka kwa sababu hatuna imani kuwa Mungu atafanya Kazi katika kila jambo katika maisha Yetu: Tuna karibisha mashaka na hofu zichukue  furaha yetu na amani tukidhani kuwa Mungu hana nguvu ya kuyakabili matokeo hasi ya maisha yetu:

Matokeo yake kama wakristo ni anguko linasababishwa na ukosefu wa  Imani sahihi na kujitengenezea Imani iliyojaa mashaka: imani dhaifu: ni katika mazingira haya umuhimu wa Maarifa( elimu) ni muhimu sana sana katika maisha Yetu:
Ni kweli kabisa imani na ufahamu (elimu) Vina kwenda pamoja: elimu inakusaidia kuielewa zaidi Imani katika usahihi wake: Elimu au maarifa yatakusaidia Sisi kutekeleza imani kwa uhakika zaidi:

Ni sawa kabisa kama utaambiwa sasa hivi ebu twende tukapande bembea: kwanza utajiuliza maswali mengi ili uweze kupata kufahamu zaidi kuhusu bembea na kama ni ya umeme ndio kabisa: utataka upate ufahamu mkubwa kuhusu bembea kabla hujejiridhisha upande Hiyo bembea: ufahamu unahitajika na Imani ya kuamini na kisha kutenda ni lazima:

Ukiwa na ufahamu wa kutosha utakusaidia kuondoa mashaka na uwoga na kuifanya imani ifanye kazi yake kwa usahihi:

Ni kweli kabisa ufahamu unatusaidia sisi kujitambua na kuacha kufuata mambo ambayo yanaweza kututoa Sisi katika Imani hatarishi ya kupotea au kuangamia kwa upumbafu wetu: Ndio maana Hosea anasisitiza Watu wangu wana angamia kwa kukosa maarifa: Maarifa ya utambuzi: maarifa mazuri ya kufuata njia sahihi  ambayo haina mashaka:

Maarifa sio imani: ni ukweli kuwa Imani inahitaji maarifa kama chachu ya kuamini na kutenda: maarifa husaidia kuleta muafaka wa utekelezaji wa Jambo kupitia Imani: kama Paulo alivyosema: Paula alisema Imani bila Matendo ni Kazi bure:

Je wewe na mimi ni aina gani ya wakristo? Ukristo wetu umebeba Imani ya kiwango gani? Imani imara au tumekuwa wakristo wa Imani haba?

Tukumbuke bila imani thabiti ukristo wetu uko mashakani:

Je Wewe ni imara kama Imani yako: Kwetu kama wakristo kuwa imara ni uwezo wetu wa kumtegemea Mungu Baba; Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu;

Ni wakati wetu sasa tuwe na Imani kwa Mungu kumpigania Mungu kwa nguvu zote bila woga na kuamini kuwa Mungu ni kila kitu na kuiweka Imani juu ya kila kitu au mtu: Paulo na Titasi walivyoamua kumtumikia Mungu katika mazingira magumu ya kutisha lakini Mwisho walitambua kuwa Mungu ni kweli kabisa bila imani wasingeweza kumtumikia Mungu:

Tuhitimishe somo letu kwa maneno ya Paulo  ufahamu unatusaidia sisi kujifunza kutokana na yaliyopita yasasa na kupitia Imani inavileta vyote pamoja na hapo tunapoona nguvu ya Matendo mbele ya Mungu wetu:

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Wednesday, January 9, 2019

SIKU 8. AKISI YA IMANI

JANUARY 8.                        2019

YERAMIHA 31:16-17

1 PETRO 5: 7

KWA NINI UNANILILIA MIMI?

Tukumbuke kuwa Mungu anatujalia sisi tukifanikiwa kufanya uchaguzi sahihi wa mambo: tunapoweza kuchagua kuishi maisha yetu kulingana na neno lake: matarajio yake; na njia zake sahihi anatujalia sisi nguvu za ziada:

Kwa msingi tunakumbushwa umuhimu wa kuendelea kumtumaini Mungu katika kila jambo;

Imani yetu iwe imara katika nafasi ya kwanza:

Mashaka yanapo tusonga juu ya Imani Yetu hatutakiwi kukata tamaa na kuvunjika moyo Neno linakuja kwako kusema nawe; Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana. ndio maana

Yeramiha 31:16-17 anatukumbusha kuwa  “BWANA asema hivi, Zuia sauti yako, usilie, na macho yako yasitoke machozi; Maana kazi yako itapata thawabu, nao watakuja tena toka nchi ya adui; Ndivyo asemavyo BWANA. Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema BWANA;

Leo tunakumbushwa kuwa pale tunapolia kwa uchungu: tunapo lia kwa kukata tamaa na kujiona kutokufanikiwa tuna amua kwa makusudi kusimama mbali na imani ya kweli ya kumtumaini Mungu;

Leo tunahimizwa kulia kwa furaha tunaposifu kazi na ukuu wa Mungu kwani kulia kwa namna hii ni kulia ambako kumejaa imani na uzuri wake ni kuwa tunakuwa tunalia machozi ya furaha; machozi ya shukrani; machozi ya imani:

Tunakumbushwa kuzingatia kuendelea kuomba kwa Imani tunapokuja mbele za Mungu katika maombi: hatutakiwi kumwomba Mungu tukilalamika, tukinung’unika pamoja na kulia na kuomboleza kwingi.

Matendo ya aina hii ni dalili tosha ya kukosa imani. Waebrania 11:6 Hivyo pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana ye yote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.

Ni kweli kabisa imani inakupa ujasili na nguvu ya kuringa ukijua kuwa unafanikiwa; Waebrania 4: 16 tuje kwa ujasiri mbele ya kiti cha neema ili tupewe rehema na neema ya kutusaidia wakati wa uhitaji;
Tukiwa wajasili maombi yetu yana mpendeza Mungu naye hutubariki kulingana na mapenzi yake; Mungu hapendi sisi tulie lie bure bila sababu ya maana; 

Imani itakuondolea mashaka: Na mashaka hukuletea wewe kulialia maana maandiko yanasema zuia sauti yako usilie na macho yako yasitokwe machozi maana watarudi tena toka nchi ya adui.

Unapolia lia ovyo unamkaribisha shetani naye hukuongoza katika njia na mawazo mabaya; tuya kumbuke
maneno ya Yesu alipomwambia yule Mwanamke Mjane wa Naini akitoka kwenye lango la mji kwenda kumzika mwanae wa pekee alimwambia usilie.

Mwanamke mjane aliamini na kuondoa mashaka yake na kijana wake alifufuliwa:

Ni wakati sasa wa  wewe na mimi tuache kulia lia ovyo bali tumkimbilie Kristo na shida zetu kama Barua ya

1 Petro 5: 7 inasema umtwike Mungu fadhaa zako maana anajishughulisha mno na mambo yako;

Tukumbuke kuwa tunapolia na Imani tumepewa ya kujiamini ili tutende na kupata majibu tunazuia nguvu ambayo iko ndani yetu ya kutenda miujiza: tunatakiwa kuwa jasili:

Tumkumbuke Musa alimlilia Mungu 
Mungu anamuuliza Musa mbona unanililia  mimi? Mungu akamwambia Musa Mbona unaniomba mimi wakati una kila kitu cha kutatua tatizo lako: Mungu alimpa Musa fimbo ambayo ilikuwa ni mwongozo na msaada katika safari yao nzima.

Ndipo alipomwambia inua fimbo yako. Na itakupa jibu la shida yako:

Je sisi tunapomlilia Mungu tunajua nini Mungu ametukabidhi sisi ili tuweze kushinda shida na matatizo ambayo yako mbele yetu?
Yatupasa kuamini na kuishi katika imani ya kweli tukiamini kuwa Mungu atatuvusha salama katika matatizo yetu yote;

Somo letu leo linatukumbusha  kuwa huu sio wakati wa kulia ni wakati wa kutambua ni silaha gani Mungu ametujalia sisi ili itusaidie wakati wa shida zetu; tuwe imara; tuwe shupavu kuondoa mashaka ambayo yanatufanya sisi  kulia lia ovyo.

Tujivike Imani; Imani iwe ngao yetu na msaada wetu:

Amina Amina Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019

Tuesday, January 8, 2019

SIKU 7. AKISI YA IMANI

JANUARY.  7              2019

WAEBRANIA 11:6

Warumi 11:8 – 19

Yakobo 2: 14-26

TUNAMPENDEZAJE MUNGU

Lazima tukubali kuwa bila Imani hatuwezi mpendeza Mungu: Tukiweza kuishi katika imani tujue wazi tunampendeza Mungu:

Ukristo wetu umejengwa chini ya msingi imara wa Imani: na msingi huo ni wewe na mimi: kwa kuwa msingi bora wa Imani ndipo tunaweza
Kupata kibali na baraka kutoka kwa Mungu juu ya maisha yetu: kwa nini tunapata kibali? Kwa sababu tumeamini: kama Paulo anavyosema:
Waebrania 11: 16 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

Kama nilivyosema katika masomo yaliyopita kuwa kuwa kuna njia mbili ambazo ni msingi wa maisha yetu;  kwa kuona (sight) ambayo ndio njia iliyozoeleka sana; kila kitu msingi wake unakuwa ni kwa kuona;

Na njia ya pili ni kwa imani hii msingi wake kila kitu msingi wake ni imani; na kuamini katika vitu ambavyo havionekani; hii ndio njia ya Mkristo wa kweli kuamini ukuu wa Mungu na matendo yake: huu Ndio msingi wa ukristo wetu:

Kwa imani Abeli alimwabudu Mungu; kwa imani Enoki alitembea na Mungu na kwa Imani Noha aliweza kufanya kazi na Mungu;

Maisha ya imani yanaanza utayari wa kukubali mwito wa Mungu; Mwito wa kwanza ni kuacha dhambi; na hatua ya pili ni kukubali maelekezo ya Mungu bila kuwa na mashaka:

Kwa Imani Abramu aliitikia wito wa Mungu wa kwenda nchi ambayo Mungu alitaka yeye aweze kwenda: tunaona utayari  wa Abramu kuacha kila kitu ambacho alikuwa nancho na kwa macho ya imani kukubali kwendakwenye nchi mpya;

Kuishi kwa imani ni sawa na kuendesha gari katikati ya ukungu mzito kwani hujui hata wapi unakwenda; lakini unajiamini na unaendelea kuendesha; na ukiamini kuwa ukungu utakwisha mara moja na utaanza kuona vizuri; hivyo ndivyo kuishi kwa imani:

Abramu lisubiri kwa unyenyekevu ahadi ya Mungu iweze kutimia; kitu kikubwa katika imani ni kusubiri; tukumbuke kuwa muda ambao tunasubiri kabwe hautaweza kupotea bure; ni wajibu wetu kuondoa mashaka

Ni kweli kabisa Mungu anaweza kutujaribu sisi kwa namna tofauti sana na kutupitisha katika tanuri la Moto lakini siku zote tukiwa na Imani thabiti ambayo inahitaji matendo haitaruhusu mashaka kama Yakobo 2: 14-26 inavyotufundisha;

Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 na mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?
17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 18 Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
19 Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
25 Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?
26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa:

Jambo la msingi katika kujenga imani ni kuondoa mashaka na kuamini: Mungu atatumia kila kitu katika maisha yako kukufanya wewe uwe Karibu naye: Mashaka na woga  haviwezi ushinda msingi imara ambao unaujenga ndani yako:

Ukristo wetu ukijengwa katika msingi imara wa Imani hakuna chochote cha kutushinda: mashaka na majaribu juu ya imani yetu na juu ya Mungu wetu lazima vitajitokeza kwa nguvu: lakini haviwezi shinda kama msingi wake ni imara:

Tunapo hitimisha somo letu leo jiulize swali la msingi wewe ni imara katika IMANI au wewe ni vuguvugu katika IMANI?

Amina 🙏🏿🙏🏿🙏🏿Amina 👏👏👏Amina

Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019