May 4
Mathayo 18: 3-4
Tafkari yetu leo tunaangalia jinsi Yesu alivyotuagiza kuwa tukiwa
kama motto mdogo ni rahisi sana kuingia katika ufalme wa Mungu; Je Kwa nini
yesu anataka sisi tuwe na fikra na akili za motto mdogo katika kuridhi ufalme
wa mbinguni? Watoto wadogo mara zote ni wategemezi wa wazazi wao kwa kila kitu;
ni wasikivu, na pale wanapokosea wataumia watalia lakini mwishoni
hujinyenyekeza na kuomba msamaha, hawana kiburi, hawafikirii madaraka , wala
mali na kila kitu mbele yao wanachokipata wanashukuru na kufurahia; hupenda
kujifunza na hata wakikosolewa hucheka na kujaribu tena;
Tafakari yetu leo wazo kubwa ni ugumu wa sisi kama watu wazima
ambao tayari tumeshakuwa na akili zetu zimeshakuwa na tunakuwa na ugumu wa
kujinyenyekeza mbele ya mungu tukitambua kuwa sisi tunaweza kujitegemea sisi
wenyewe na hatuhitaji msada wa Mungu; Yesu hapa anatukumbusha kuwa ili ukuu war
oho unahitaji unyenyekevu ambao watoto wanao na sisi watu wazima tunapingana
nao; tukumbuke kuwa unyenyekevu ni hatua ya kiroho ya kukua na sio hatua ya kujidumaza; Yesu
anatufundisha kuwa lazima tubadilike kama tunataka kuingia katika ufalme wa
mbinguni; Lazima tutubu makosa yetu kwa moyo na kuweka kusudio la kuacha
kutenda dhambi au kuendelea kutenda dhambi. Lazima tabia zetu kuhusu dhambi
ziwe za kupinga dhambi.
Tafakari yetu tukisoma 1 Wakoritho 14: 20 inatukumbusha
kuwa Ndugu zangu, msiwe watoto katika
akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu
mkawe watu wazima. Akili ya
watotohawafikirii mabaya; ma hawafikirii kutendewa mabaya humpenda kila mtu,
humwamini kila mtu, humfurahia kila mtu wamwonaye; hivyo sisi kama wakristo
tunatakiwa kubadilika kuwa wema, kuishi katika maadili mema, kutenda mema, na
tukifanya hivyo thawabu yetu itakuwa kubwa mbele ya Mungu; ndio hata tukisoma
kutoka Injili ya Yohana 3:3-5 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin,
nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?
Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa
maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kwa kuzaliwa kwa mara nyingine ni kuwa tayari
kubadilika na kuuvaa unyenyekevu ambao ni msaada mkubwa katika matendo yetu
katika kukamilisha safari yetu ya Mbinguni;
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mtoto hana hadhi yeyote ndani ya
familia au jamii; kwa vile huonekana kuwa ni tegemezi basin a hana nafasi ya
kufanya maamuzi yeyote; Hili ni tatizo kubwa kwetu kwani tunapenda kuheshimiwa,
kunyenyekewa, hata wakati mwingine kuabudiwa; tunatakiwa tuwe watu ambao sio
kitu katika ulimwengu huu bali tukijua kuwa Mungu ndio tegemeo letu na ngao na
kinga yetu; Kama vile watoto wanavyowategemea wazazi wao kwa kila kitu nasi ni
wakati wetu wa kumtegemea Mungu kwa kila kitu.
Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment