WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, May 23, 2016

JE WEWE NI MASIKINI WA ROHO?


May 23


Mathayo 6: 25-34

Tafakari ya leo tujikumbushe mahubiri ya Yesu alipowahutubia watu zaidi ya 5000 mlimani; Mwinjili Mathayo anaelezea mafundisho ya Yesu akizungumzia zaidi kuhusu Umasikini, Utajiri na Mamlaka. Yesu anatuonyesha kuwa yeye alikuwa kiongozi ambaye alikuwa anajali haki sawa kwa wote; ambaye alikuwa na mawazo ya kiuchumi na ambaye alikuwa hapendi matabaka katika jamii; hasa pale masikini wanapoonewa. Yesu alijidhihirisha kuwa yeye ni mkombozi wa wote; kwani alijua kuwa watu masikini katika jamii wako nasi siku zote; yesu aliona tatizo la tabaka ambalo lilikuwa likiendelea kukua miongoni mwa jamii kati ya walicho nacho na wale ambao walikuwa hawana yaani masikini. Na yesu alionyesha wazi kabisa kuwa anawachukia wanafiki; Yesu ameonyesha sana kuchukizwa na wale ambao wanawadhulumu wengine hasa wanyonge;  ambao wanawatumia masikini katika kujitajirisha; Yeasu mafundisho yake ni ya Haki kwani anapenda kuhubiri haki na kuishi haki;

Tafakari yetu leo inaonyesha msimamo wa Yesu kuwa  anataka sisi tuwe na furaha siku zote lakini furaha yetu ijengwe katika misingi ya haki; kama tunavyosoma katika kitabu cha zaburi 144:15 Bwana, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu?  Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake,  Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake.  Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.  Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele. Hivi ndivyo sisi tunafapaswa kuwa na kwa umasikini huu war oho ni utajiri mkubwa sana mbele ya mwenyezi Mungu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa  Mungu anataka kutubariki sisi lakini ila Baraka zake zikae juu yetu lazima tuwe masinikini war oho; watu ambao tuko tayari kufuata maelekezo ya Mungu. Ili kupata furaha ya ndani kabisa ya Kimungu lazima tujiepushe na makando kando; furaha yetu daima iongozwe na miongozo ya Mungu na sio mambo ya kidunia; Mafundisho ya Yesu Mlimani ni kielelezo cha wazi kuwa ili uwe masikini wa roho na tajiri wa mbinguni watakiwa kufanya nini. Tuzikumbuke zile HERI; kwa mafundisho ya yesu mlimani Heri ni kunyume cha yale dunia inachofanya ili kuitafuta furaha. Na Bahati mbaya furaha hiyo ya dunia ni ya muda mfupi tu; Yesu hakusema heri matajiri lakini yeye alisema heri masikini, heri wanaolia. Heri wanaodhulumiwa, heri wanyenyekevu,heri wenye njaa ya haki; hawa wote ambao wanaombewa heri hizi ni watu ambao ni wanyonge hawana sauti katika mamalaka ya dunia hii na wamekandamizwa na hawawezi kufurahia utukufu wa Mungu japo wanatamani kwa sababu ya dhuluma na nguvu ya giza ambayo imekandamiza; Lakini kwa mafundisho ya yesu Mlimani anawafungua na kuwaondoa gizani na kuwapa nuru mpya ya kufurahia maisha ya yenye utukufu wa Mungu kwani ni masikini wa roho lakini ni matajiri katika ufalme wa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa daima sisi wanadamu hata wale watumishi wa Mungu ambao wanadhani tayari ni masikini wa roho daima wanabadilisha na ulimwengu; wanaingia katika tama za kiulimwengu na katika tabia za kiulimwengu; na rahisi sana kubadilishwa tabia zetu kupitia matumizi ya tekinoloji; muziki, tvs; sinema, mitandao ya kijamii ambayo kwa haraka tu hukutoa kutoka katika maisha ya umasikini wa Kiroho na kukupeleka katika maisha ya Kilimwengu; lazima tutambue kuwa furaha ya kweli hutoka kwa Mungu kwa kufuata maagizo kupitia maandiko matakatifu; hivyo Mbinguni ni kielezo cha furaha; kielelezo cha neema na furaha na neema hiyo itadumu milele na hiyo ndio faida ya kuwa masikini wa Roho; Wokovu ambao tumepewa kupitia Msalaba ni kielelzo cha furaha kubwa kwa masikini war oho lakini ili kufurahia wokovu huu ni lazima tutimize kwa vitendo mahubiri ya Yesu Mlimani;

Tafakari ya leo inataka wewe na mimi tujiulize katika zile kheri tunazitimizaje: je Tunazitimiza kwa vitendo au kwa maneno?
Hii ndio tafakari yetu ya Leo:


 Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment