WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, May 19, 2016

TUNATAKIWA KUSIMAMA IMARA:


May 19
Zaburi 46:10
Tafakari ya leo inataka tujiulize kuwa je umewahi kujisikia kuwa maisha yamekuchakaza? Na ukajiona kuwa umebanwa katika ulingo na huna mahali pa kutokea au kujiokoa? Na unajishangaa kwa nini umefika katika wakati kama huo na huna msaada wa njisi ya kujinasua? Hata tukisoma katia katika kutoka katika Bibilia tunawaona wana wa Israeli walifikia hatua hii katika Sura ya 14 hawakuweza kujinasua kwa kurudi nyuma au kwenda mbele walikuwa na mwelekeo wa upande mmoja tu na hawakujua nini cha kufanya. Tujiulize tena je umwewahi kukumbwa na khali kama hii katika maisha yako? Unakuwa katika khali ya kupooza, huwezi kwenda kulia wala kushoto na hujui nini cha kufanya; angalisho hapa kuwa hata sisi ambao ni wakristo tunaweza kumbwa na khali kama hii lakini biblia inatufundisha kuwa tukipatwa na khali kama hii kimbilio lisiwe kujiua kama watu wa mataifa wafanyavyo.
Tafakari inatukumbusha kuwa kama wakristo tunatakiwa kuwa watu wa furaha wakati wote na hatutakiwi kuhofu chochote; bali kuwa watu wa shukrani wakati wote; najua tatizo kubwa ambalo linalutusumbua je utakuwaje na furaha wakati uko kwenye dimbwi la matatizo? Je utakuwaje na furaha wakati unamwomba Mwenyezi Mungu akutoe kwenye hizo shida na huoni dalili ya unafuu na shida zinaongezeka? Lakini bado tunasisitizwa na bibilia na mafundisho ya Yesu kuwa tunatakiwa kufungasha matatizo yetu na kumkabidhi Mungu ili yeye pekee abadilishe matatizo yetu kuwa kicheko. Hivyo hatutakiwi kabisa kugeuza mioyo yetu kuwa jehanamu. Tukumbuke kuwa shida nyingi ambazo tunakumbana nazo katika maisha yetu ni sababu ya sauti nyingi ambazo tunazongana nazo katika vichwa vetu, ambazo zimejaa Mawazo Hasi: mara nyingi mawazo yetu hasi yanatokana na ugumu wetu wa kusubiri  neema ya Mungu katika kututoa katika ugumu wetu wa maisha. Tunakuwa hatuna subira hata kidogo; tunalinganisha neema ya Mungu kama vile tunasubiri ahadi ya rafiki ambaye wakati mwingine hana uhakika kama atatekeleza; Tumesahau kuwa ahadi ya Mungu ni ya uhakika.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tujifunze kusubiri ili kuona neema ya Mungu ndani ya maisha yetu na shida zetu; Hapo ndipo tunapotakiwa kusimaa IMARA na kuondoa tabia za kibinadamu za kujiamulia na kutekeleza hatima yetu ambayo mwisho wake haitusaidii kwani haituondoi katika matatizo. Tukishika usukani vibaya tukumbuke kuwa Mungu wakati wote anatusaidia kuonyesha na kuongoza njia ili tusinase katika tope; hataki tuendelee kuzama  Jukumu letu ni kuwa tayari pale Mungu anapoongea nasi na kutoa maelekezo ya namna ya kufanya. Ni jukumu letu kufanya na kusubiri wakati wa Mungu na si wakati wetu. Tumkumbuke Musa alipowavusha wana wa Isarel katika bahari ya sham pamoja na woga na kelele za kuwa tutaangamia; hawakufanikiwa kuvuka mpaka pale Mungu alipomwambia Musa sasa Nyosha Mkono wako , na alifuata maelekezo ya Mungu na Bahari ya sham ikagawanyika sehemu mbili na wakapata njia ya kupita.
Tukumbuke kuwa imani haisikilizi, viashiria vya nita nita, imani haisikilizi watu ambao hawana uvumilivu, imani haisikilizi waoga, walio kata tama bali Imani husikiliza Roho wa Mungu ambaye katika majaribu na shida zote Imani itakuambia Simama Imara na uamini kuwa mimi ndiye mwanzo na mwisho wa Maisha yako. Tukumbuka Hadithi ya Yairo; kama ilivyosimuliwa katika Luka sura ya 8. Alipomlilia Yesu akamponye Binti yake ambaye alikuwa anaumwa sana. Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu Yairo hakufanikiwa kuongea na Yesu na alipokuwa tayari kuongea na Yesu alipwea taarifa kuwa Binti yake amefariki. Hapa Yairo alikuwa kwenye matatizo makubwa ambayo hawezi kujitoa mwenyewe, lakini yesu alimwambia usihofu alikwenda naye nyumbani kwake na Kumfufu Yule Binti yake wa miaka 12. Lisilowezekana kwetu kwa halishindikani kwa Mungu ndio maana tunatakiwa kusisma Imara.  
Kwa hiyo tutakumbusha kuwa katika khali yoyote ile ya matatizo yetu tunatakiwa kutanguliza imani mbele na kumtumaini Mungu tukifuata maelekezo ya kusimama Imara na kumwachia Mungu atuongoze na afanye kazi yake kwetu. Yeye anayafahamu maisha yetu na kila hatua ambayo tunakanyaga. Yeye ambaye anajua idadi ya nywele zetu ; hii ndi tafakari yetu ya leo- Amina

Emmanuel Turuka


         

.







No comments:

Post a Comment