WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, May 8, 2016

SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUSHEREKEA KIUNGO KIKUBWA CHA FAMILIA- MOTHERS'S DAY



May 8

Mithali 14; 1

Tafakari ya leo tunakumbuka kiungo kikubwa sana cha  familia yetu. Siku ya  kuwaenzi akina mama wote Duniani.  Tukumbuke kuwa mchango  wa  mama zetu na akina mama  wote  ni  mkubwa katika makuzi ya familia. Familia  ni  kielelezo cha juu kabisa cha  jamii yetu. Tukumbuke kuwa jamii ni  zao la familia.  kielelezo cha  familia zetu hakiwezi kukamilika kama hatutaenzi wajibu wa mama  ndani  ya  familia.  Kama  kitabu cha mithali 11- 6 kinavyosema Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata    heshima, Apataye mke apata kitu chema  naye ajipatia kibali kwa BWANA;huu ni ukweli mtupu ndio maana tuna kila sababu ya kusema asante sana kwa upendo wenu huo. 

Je umuhimu wa mama katika familia umejikita zaidi katika malezi? Jibu la  swali Hilo ni  hapana.  Wajibu wa  mama pamoja na ukuu wao katika malezi kwa  kweli wamevuka mipaka.  Ndio maana waswahili hunena kwenye mafanikio makubwa ya  mwanaume yeyote nyuma yake kuna  nguvu ya  mwanamke. Kama Mtaalam mmoja aliwahi sema kuwa  pindi mtoto anapozaliwa na mama anazaliwa pia, mama hakuishi kabla; bali mwanamke anaishi muda wote lakini mama ni kitu kipya kinachokuja baada ya mtoto kuzaliwa;lakini ndio wajenzi wakuu wa familia Mithali 14; 1 inatutaadhalisha kuwa Mwanamke mwenye hekima huijenga   nyumba yake,  bali mpumbavu huibomoa nyumba yake    kwa mikono yake mwenyewe.

Tafakari yetu Leo siku ya kuwashukuru sana  “ Mama” kwa jinsi wanavyojitolea katika kuhakisha kuwa kila kitu ndani ya familia kinakwenda vizuri, kama mama ni legelege ndani ya familia na familia itayumba tu; Ni ukweli usiopingika kuwa katika kila mafanikio makubwa ndani ya familia nyuma yake yuko Mama; Mitahali 5- 18 inaendelea kutufundisha kuwa Chemchemi yako na ibarikiwe  na ufurahie mke wa ujana wako;

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwajalieni busara, upendo, ujasili na unyenyekevu ambao ni daraja la msingi sana katika kuimarisha nyumba bora yenye upendo mkubwa. Kwa namna ya pekee leo napenda kuwakumbuka na kuwashukuru sana na nazidi kumwomba Mungu azidi kuwajalia afya njema na amani katika maisha yenu ya kila siku hii ya kumbukumbu yenu mmekuwa daima kiungo muhimu sana katika maisha yetu na katika ukuaji wa familia. Hekima yenu haina mipaka, upendo wenu hauna mipaka, msamaha wenu hauna mipaka; nasi tunaendelea kumshukuru Mungu katika kuenzi ukuu na ujenzi wa familia zetu;

hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment