WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, May 30, 2016

TWATAKIWA KUWA NA NIA YA THABITI;



May 30

Wagalatia 6:9

Tafakari ya leo tunaangalia dhana nzima ya maisha yetu tukijua kuwa Maisha yetu yamezungukwa na mitihani mingi sana. Lakini ili tuweze kukabiliana vizuri na mitihani hiyo ya maisha lazima tujijengee nidhamu ya hali ya juu na nia madhubuti ili tuweze kushinda. Hivyo hivyo katika kuimarisha ukristo wetu; lazima daima tuweke katika akili zetu malengo yetu ni yapi; Tujifunze kusahau yaliyopita; lazima tuondoa katika akili yetu dhan zima ya mambo magumu ambay tunafikiri hayawezekaniki; na kujiondole avipingamizi vinavyokuzunguka wewe mwenyewe ambavyo kwa namna moja au nyingine hukurudisha nyuma; hatutakiwi kufikiria mambo hasi; hatutakiwi kutaka tama na kuishi kwa kunungunika;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tuishi katika malengo makuu mawili; kuishi maisha yenye mwelekeo na maisha yaliyojaa shauku; Mwenyezi Mungu siku zote ametupa sisi njia na mbinu za kushinda; lakini wajibu wetu lazima tuwe na nia ya ushindi; nia ambayo haiwezi kukatisha tama na yeyyote Yule; Mwenyezi Mungu kwa kutambua ushindani wa maisha ambao uko mbele yetu alitupa sisi maarifa kwani kwa maarifa sisi tutakuwa huru na kufanya maamuzi sahihi; Ametupa sisi uhuru wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi; lakini kwa udumafu wetu hata pale ambapo maji ni mengi lakini bado tunalalamika kuwa tunaona kiu; kwa nini khali kama hii inaweza tokea Jibu ni rahisi tu ni ukosefu wa Maarifa sahihi na kujiamini.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa lazima tuachane na vitu vyote ambavyo vinazuia na kuchelewesha utekelezaji wa mipango endelevu ya kuwa na nia nzuri ya kufanya mazuri katika maisha yetu katika kuufikia uzima wa kweli; Ili tuweze kufanya vizuri tunahitaji kutayarisha akili zetu ili ziweze  kuwa tayari kupokea matokeo ya matendo mazuri. Tukikumbuka kuwa kuweka Nia ni kitu muhimu katika maisha yetu; ni tendo linalotufanya sisi kuendelea kutenda jmabo wakati tayari tulikuwa tumeanza kukata tama; Kuweka nia kutufanya sisi tusiwe na mawazo ya kuacha kutenda jambo iwe katika kazi; maisha ya kawaida na hata kwenye ndoa zetu; Kuweka nia kunatusaidia sisi kupambana na dhoruma za maisha na vishawishi mbali mbali;  hakuna kati yetu anaweza kufanikiwa bila kuwa na nia dhabiti. Hata kuishi kwa mafanikio katika maisha ya kumpigania Kristo kunahitaji kuwa na nia dhabiti; wagalatia 6:9 inatufundisha kuwa Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

Tafakari yetu inatufundisha kuwa ujasili unategemezwa na nguvu ya Mungu kwa kuomba na kumtegemea yeye  kwani katika 2 Wakorinto 12:9 anatuhakikishia kuwa Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Tunachotakiwa kukumbuka kuwa wakati wako Mungu aliokupa katika kufanikiwa haya ya moyo wako ni wakati wako na unatakiwa kuufanyia kazi bila kuogopa; tukumbuke kuwa unapokabiliwa na vipingamizi vyovyote unachotakiwa kusema kuwa kwa nguvu za Mungu hakuna awezaye kusimamisha hiki ambacho nimepanga au lengo ambalo nimetaka kulifikia. Nguvu za Mungu zimenijengea nia madhubuti katika moyo wangu na utendaji wangu; Popote nitakapo kanyaga nguvu na Baraka na Mwongozo wa Mungu u juu yangu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa sisi binadamu tukumbuke kuwa kitu cha thamani sana ambacho tunakimiliki ni kuwa na NIA thabiti; hata kama utakuwa na Pesa lakini huna NIA ni kazi bure mali zako zitapotea bure. Hivyo hatak kama tutakuwa tukitembea katika bonde la uvuli wa mauti kama tuna nia na tunamtegemea Mungu hakuna kitu ambacho kitaturudisha nyuma lazima tuwe na NIA thabiti ya kuvuka na kufika katika uvuli ambao umejaa majani mabichi.

Hii ndio tafakari yetu ya leo;

Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment