APRIL 14
Hosea 4:6
Tafakari ya leo tunaangalia jinsi gani tunavoangamia kwa kukosa
maarifa. Je ni maarifa gani hayo ambayo yanatusababisha sisi tuangamie Hosea
natukumbusha kuwa Watu wangu
wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami
nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu
wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. Hii ndio elimu na Maarifa ambayo tunakumbushwa kuwa tumeshindwa
kushika na kufuatilia. La msingi tunatakiwa kugundua kuwa tumekuwa tukikosa
kujua elimu ya Mungu. Kama vile Mungu kupitia Hosea 4:1,2 aliwambia Lisikieni neno la Bwana, enyi wana wa Israeli; kwa
maana Bwana ana mateto nao wakaao katika nchi, kwa sababu hapana kweli, wala
fadhili, wala kumjua Mungu katika nchi. Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua,
na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa kuna uhusiano wa karibu sana kati
ya matendo yetu ya na matendo ya kiroho; matendo yetu daima yanatutuma na
kutufanya uwajibikaji wetu katika maisha ya kiroho yakiwa yanapungua sana;
tunaishia kuwa wabinafsi; tunajiangalia sana wenyewe na tunasahau kabisa nafasi
yetu ya kumtumikia Mungu na kukosa kabisa maarifa katika utumishi wa Mungu
wetu. Bila kujijua watu wengi tunaishi katika giza na kuvunja amri ambazo Mungu
alitaka sisi kuzifuata na kuishi kulingana na amri hizo.
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa maarifa ya Mungu ni ukweli,
mara nyingi hatusikilizi ukweli wa maagizo au mafundisho ya Mungu kupitia Bwana
wetu Yesu kristo au kupitia mitume au wafuasi wake; matokeo yake ndio kiama
chetu au maangamizo yetu kwa kukosa maarifa ya kweli ya ufalme wa Mungu;
Matthew 13:15 Maana mioyo ya watu hawa
imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba;
Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo
yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Tafakari yetu ni kweli watu wengi wanajidai kumtumikia Mungu
lakini katika uhalisia hawafanyi hivyo; utawezaje kumtumikia mungu kwa maneno
na sio matendo? Utawezaje kumtumikia Mungu wakati hufuati amri zake? Huu ndio
ukosekano wa maarifa ambayo yanpelekea watu kufanya matendo ambayo yanapingana
na maneno yao, kuua , kuiba, kudhulumu yatima na hata kosa la uzinzi. Kwa vile
hatuna maarifa yaliyosahii hatuwezi kutatua shida au matatizo yaliyo mbele yetu
matoke yae tunaendelea kuangamia bila wenyewe kujijua. Mungu ametupa sisi
maarifa ya kuwa wakweli ili tuweze kutimiza amri au sheria nyingine zote bila
kushindwa; lakini kwa vile tumekataa maarifa ya kuwa wakweli sasa
tutawezaje kutatua changamoto za kiroho ambazo ziko mbele yetu. Matahali
3: 19- 23 Kwa hekima Bwana aliiweka
misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara; Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu
yadondoza mande. Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika
hekima kamili na busara. Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni
mwako. Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama,
Wala mguu wako hautakwaa. Hiiyote tunatakiwa kuwa na
maarifa ya kimungu.
Tafakari yetu bado inatukumbusha kuwa Mithali 24: 3-4 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu
huthibitika, Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya
thamani na vya kupendeza. Ukweli ambao ndio msingi wa maarifa ya Kimungu ni
chanzo cha mafanikio yote, ukweli utakufany uwe mnyenyekevu, ukweli utakupa
busara; lakini moyo wako ukijaa choyo, wivu, majivuno na unafiki ni wazi kuwa
hii ni kithibitisho cha maangamizi. Hivyo ni wajibu wetu kujitathimini kuhusu
tafakari hii na kumrudia Mungu na kuomba neema ya maarifa yatokanayo na mungu
ambayo ni msingi wote wa upendo, amani, uwajibikaji, huruma kwa wajane na wazee,
na tukumbuke kuwa Busara na Hekima hutolewa na Mungu na katika Mdomo wake ndipo
maarifa na ufahamu hutolewa; Hekima ya Mungu daima inaingia ndani ya Mioyo yetu
na kukaa nasi. Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment