WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, April 29, 2016

JE WOKOVU NI HAKI YETU?



April 29

Isaya 55:8-9

Tafakari ya tunaangalia dhana nzima ya wokovu kama ni haki yetu. Ukiisoma na kuielewa Bibilia vizuri inatufundisha kuwa wokovu sio haki yetu bali ni neema ya Mungu tu; tukiangalia katika nyakati tofauti na kwa matukio tofauti Mwenyezi Mungu alitutengenezea njia rahisi ya uokovu kwa kuweka misingi mizuri  ambayo alitutaka sisi tuifuate; lakini katika mazingira haya yote kwa ujinga wetu; kwa kiburi chetu na kwa kukosa maarifa ya kimungu tuliishia kupoteza neema hii ya Kimungu. Tumekuwa watu ambao hatuishi kwatika kiwango ambacho Mungu anaweka sisi tuishi. Angali nini Kilitokea katika Bustani ya Aden;

Tafakari yetu inatukumbusha leo maneno ya  Nabii Isaya 55:8-9 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.  Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maneno haya mazito yanatoka na jinsi ambavyo sisi tumeshindwa kutembea katika njia za bwana. Tulitayarishiwa makao mazuri ili tutembee na bwana tumeshindwa kwa sababu ya Kiburi chetu.

Tafakari yetu leo inatakiwa itukumbushe kuwa tunatakiwa kushukuru kuwa wokovu ni neema ya peeke ambayo tumeipata na nguvu ambayo Mungu ameiweka ndani yake kwa wokovu wetu; ni wajibu wetu kuendelea kufanya maungamo ya dhambi zetu katika kuimarisha hii neema ya wakovu. Ni kweli kuwa sisi sote tumefanya dhambi na kupungukiwa utukufu wa Mungu. Ndio maana kwa upendo wake Mungu bado ameendelea kutuokoa kwa neema yake ili tusiingie katika moto wa milele. Huruma na neema ya Mungu haina mfano sisi ni kama majani yanayopuputika katika mti lakini Mungu kwa upendo wake anatuokota na kutupa sisi huruma ya ya kimungu ya wokovu. Pamoja na dhambi zetu bado tumekaribishwa katika uzima wa milele;

Wakovu wetu u mikononi mwa Bwana kwa upendo wake na huruma yake hataki hata mmoja wetu apotee wajibu wetu ni kuomba msamaha na kuishi kulingana na njia zake; Je wewe na mimi tunatumiaje neema hiiya wakovu. Hii ndio tafakari yetu ya Leo


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment