WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, April 25, 2016

ZAO LA CHUKI KATIKA MAISHA YETU;


April 25

WAEFESO 4:31,32

Tafakari yetu ya leo tunaangalia ni zao la chuki na hasara yake katika maisha yetu ya kiroho; tukumbuke kuwa zao la chuki huzaa hasira na ghadhabu. Tukisoma Waefeso 4:31,32 inatukumbusha kuwa Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheana  kama na Mungu katika Kristo alivyosamehe ninyi. Lakini tukumbuke kuwa sisi sote  tumesulibiwa pamoja na Kristo, hivyo hatutakiwi kukaribisha chuki ndani ya maisha yetu;

Tafakari yetu inaweka sawa kuwa zao la chuki husababisha hasira ambayo huleta uchungu hivyo Mara nyingi UCHUNGU husababisha akili kushindwa kufanya kazi ipasavyo.        Ni hali ya kutokuwa na furaha, kujawa hasira zilizotokana na kutendewa mabaya.  Ni hali ya kuhisi huzuni nzito ambayo wakati mwingine inaweza kuchangamana na maumivu makali katika fahamu za mtu, ambayo yaweza kusababisha mwili kunyong'onyea na kusababisha akili kupoteza uwezo wa kufikiri vizuri. Bibilia inatukumbusha kuwa ili kuweza kuondokana na zao hili la chuki basi Wakolosai 3:1-3 basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu, yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu


Tafakari yetu pia inatueleza kuwa zao la chuki pia huleta ghadhabu ambayo nia  hali ya mtu kuwa na maamuzi ya pupa pasipo kujali madhara yake. Hali hiyo yaweza kumfanya mtu kuwa na majibu ya mkato mkato, kutopenda kuulizwa ulizwa; humfanya mtu kuwa mgomvi na  kutopenda kuwa na subira;  Chuki husababisha kuvunja amri za Mungu kwani bila kutarajia hujikuta mtu kufanya matendo ambayo hayampendezi Mungu kama vile kuwa chanzo cha matusi; hasira; kukosa upendo ndio maana tukisoama Mithali 22:24-25 inatukumbushja kuwa Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi; Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi; Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.

Tafakari yetu pia inatukumbusha kuwa zao la chuki husababisha sadaka yako isipokelewe mbele ya madhabau ya Mungu; mathayo 5:23,24  Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Tukumbuke kuwa Mungu huchukizwa na sadaka za mwenye dhambi. Sadaka za mtu mwenye dhambi hazipokelewi mbele za Mungu.  Chuki ni ubaya ambao Mungu haupendi; tukumbuke kuwa  ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na wema - kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Tafakari yetu msisitizo mkubwa ni Chuki huleta ubaya, na huleta kisasi kwa sababu ya ghadhabu hivyo tunakumbushwa kuwa hatutakiwi kulipiza kisasi, bali tujiepushe na ghadhabu ambayo ni zao la chuki; Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili ya mambo mabaya uliyofanyiwa. Huwezi kulipa kisasi bila ya kumchukia huyo unayejilipizia kisasi kwake. Na Biblia inasema hivi: 1 Yohana 3:15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajuaya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. Ni kweli Chuki huzaa kisasi, na huzaa dhambi ya kuua!  Isaya 59:2b inasema; dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.



Tafakari yetu inatutaka kujikosoa wenyewe na kutubu kwa kujiepusha na dhambi ya chuki tunatakiwa tujenge upendo kwani Upendo huvumilia, hufadhili, upendo hauhusudu; 1Wakorintho 13:4 – 8 upendo hautakabari; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli huvumilia yote; huamini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote. Tukumbuke kuwa upendo huu umo ndani yako, na ndio unaokufanya uwe kiumbe kipya.
Tukumbuke maneno ya Yesu aliposema Mathayo 4:11, 12  Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia;kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Hii ni tafakari yetu ya leo ni  zao la chuki ni hasira, ghadhabu; na kadhalika tujiepushe kusongwa na maudhi pamoja na makwazo mbali mbali yatokanayo na chuki. Amina

Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment