WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, April 12, 2016

PETRO: ONDOKA KWANGU SHETANI WEWE




April 9

Yohana 1: 42

Tafakari ya leo tunaangalia maisha ya Yesu na wafuasi wake hasa mkasa wetu siku ya leo utakuwa kwa Mtume Petro, ambaye pamoja na udhaifu wake kama Binadamu yeye ndiye alikuwa msingi wa kanisa la Kristo; tukisoma Yohana 1: 42 Petro alikuwa  mfuasi wa kwanza wa Yesu; Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe). Petro alikuwa na sifa nyingi moja alikuwa msemaji, au mropokaji, alikuwa rafiki wa karibu sana wa yesu; petro alikuwa mtu mwenye hari kubwa; nguvu za kuwateka wengine; mwenye msukumo; jambo nzuri yesu aliendelea kumnyosha taratibu ili kuwa kiongozi mzuri wa Kanisa wa baada yake;

Tafakari ya leo tunaona kuwa Petro alikuwa ni mtu wa kwanza kukiri kuwa Yesu alikuwa ni mwana wa Mungu. Petro alikuwa kati ya wale mitume watatu ambao Yesu alikuwa nao karibu sana, na aliokuwa anafanya nao majukumu mazito ambayo yaliwadhihirishia kuwa yeye sio wa kawaida. Ni hao watatu ambao walikuwapo Yesu alipomfufua Yule binti wa Jairus tukisoma Marko 5:37; ni hao watatu walikuwa Yesu alipogeuka sura  Mathayo 17: 1 na ni hao watatu walipewa Jukumu la kuandaa karamu ya Mwisho Luka 22:8
Katika nyakati tofauti Petro ameonekana mwenye ari ya kufanya jambo kubwa lakini punde anakuwa hana imani tena na matokeo yake kupoteza lengo; Mathayo 14: 28-29 alipojaribu kutembea juu ya maji kisha  akaanza kuzama; 

Alikuwa petro ambaye alitamani wajenge vibanda vitatu baada ya tukio la kugeuka Sura Yesu lakini aliposikia sauti toka mbinguni aliogopa na kuanguka chini kujificha. Mathayo 17:4; Ni huyu huyu Petro ambaye alimwita pembeni na kumkataza yesu  asizungumzie Kifo chake Mathayo 16:22 lakini akasahihishwa na Yesu;  Alikuwa Petro ambaye alimkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu na kasha akaambiwa arudishe upanga wake Alani Yoana 18:10; na alikuwa Petro ambaye alimwambia Yesu kamwe hatamwancha au kumsaliti Yesu wakti wote wa Mateso yake. Mathayo 26:33

Tafakari yetu pamoja na mapungufu ya Petro  bado Yesu alimpa cheo cha kuwa ndiye mwamba na juu yake atalijenga kanisa lake; Mathayo 16: 18-19; tunachojifunza katika maisha ya Yesu, na Petro  alipata nguvu kutoka kwa Yesu pale alipomwambia kuwa anaweza tembea juu ya maji na udhaifu wake wa imani ndio ulimfanya aanze kuzama; 1 Yohana 4: 18 katika mifano yote hii Yesu anaelewa udhaifu wetu ambao unatokana na akili zetu na miili yetu ya kibinadamu; tunakosa nguvu na uwezo wa kufanya au kushawishi nini yatupasa kufanya kwa haki; yesu alitambua kuwa mitume wake pamoja na Petro walikuwa hawana nguvu hiyo bado; na hivyo walikuwa hawawezi kuona hata mapungufu yao katika kutimiza kazi ya kitume pamoja naye;

Katika tafakari ya maisha ya Petro tunaona kuwa alikuwa jasiri wa kuweza kujaribu mambo mengi magumu ambayo wafuasi wenzake walikuwa hawawezi kuyafanya; alimwambia Bwana wetu yesu Kristo kuwa bwana mimi nitakuwa nawe wakati wote wa mateso yako; ni Petro Peke yake ambaye aliweza kutoa ahadi hiyo; Pamoja na kuwa hakuweza kuitimiza lakini aliweza kumfuata Yesu katika safari yake ya mateso; Bahati mbaya tendo la Kumkataa Yesu kuwa hamtambui ni sababu ya udhaifu wa ubinadamu wetu; hata kama mimi na wewe tungekuwa katika viatu vya peter pengine tusingeonekana tena mara baadaya kuulizwa mara ya Kwanza. Peter alilia sana mara baada ya jogoo kuwika kwa sababu alijua kuwa amemsaliti Bwana wake na Rafiki yake

Je hadithi hii ya Petro inatufundisha nini sisi; Pamoja na kumwona Petro kuwa na imani haba lakini aliweza kuthubutu alipomwomba Yesu naye atemebee juu ya Maji aliweza kushuka kutoka katika Boti na kuanza kutembea lakini hakuweza kuendelea kuamini kuwa amepewa nguvu na mamlaka ya kutembea juu ya Maji, alipopoteza tu imani hiyo aliaanza kuzama na yesu akamwokoa. Katika maisha yetu ya kawaida sisi tumekuwa ni sehemu ya Petro kwani hatusimami kwenye ukweli wa imani juu ya matendo yetu dhidi ya wenzetu; tu rahisi sana kuacha njia bora ya Mungu kwa kuangalia makando kando ya mapito ya dunia hii; hivyo bado tunaneema ya kusaidiwa na mwokozi wetu pale tunapoelekea kuzama.
Je leo hii katika nafasi ambazo tumezipata za kuweza kuwasaidia wenzetu katika kumjua Kristo na kuishi maisha ya Upendo tunamtumainije Mungu? Je tunafanya jitihada gani za kueneza wokovu wa Mungu kwa wenzetu? Je tumekuwa watu wa kuogopa kulitaja jina la Yesu mbele ya wenzetu? Petro alionyesha mfano mzuri kwani aliweza kuleta wokovu wa kweli kwa Mataifa hasa yale ambayo yalikuwa hayamjui kabisa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa hadithi hii ya Petro inatukumbusha kuhusu maanguko yetu ya wakati tofauti tofauti; kama ilivyokuwa kwa Petro tunajua jinsi vile Mungu alivyoweza kumsamehe na kumtumia katika njia ya ajabu kwa ajili ya wokovu wa binadamu ndivyo Mungu anavyotaka kukutumia wewe leo kwa ajili ya taifa lake; Mungu wetu upendo wake hauna mipaka; neema yake haina mwisho; na msamaha wake ni wa milele; tujikumbushe kuwa hata pale tunapokuwa tumeanguka tujue kuwa bado Mwenyezi Mungu anatuweka katika hesabu yake;
Jambo la msingi leo tunapoyaangalia maisha ya Petro na utumishi wake kwa Krito ni umuhimu wa kusali bila kuchoka tukiruhusu tu maisha ya sala kufa tujue wazi kuwa tunajitengezea maisha ya kushindwa katika vita yetu dhidi ya shetani; mafanikio ya kumpigania Kristo yanapatikana tu kwa kuweka  Mungu mbele katika sala; Hivyo tafakari yetu ya leo inatukumbusha maisha ya sala ni maisha pekee ambayo lazima tuyapiganie siku zote za maisha yetu. Lakini pale ambapo hatufanyi jitihada za kumtafuta mungu kupitia sala tujue kuwa  tunajitafutia matatizo makubwa katika maisha yetu; lazima tutembea pamoja naye katika sala kama Petro alivyofanya;  Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa hatuwezi fanikiwa kwa nguvu na uwezo wetu pekeyetu; yesu alimwambia Petro ondoka mbele yangu shetani wewe kwani alikuwa anataka kuzuia mipango ya Mungu ya wokovu wa Mwanadamu, nasi tunawajibu mkubwa wa kufanya kwa kudumu katika sala wakati wote – hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka




No comments:

Post a Comment