WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, April 8, 2016

NIWAJIBU KUSEMA ASANTE MUNGU




April 8

Warumi 1: 21

Ni tabia nzuri kila siku kuanza chochote kwa kumshukuru Mungu kwa wema wake mwingi  juu ya maisha yetu na mafanikio yetu; Mwenyezi Mungu anatupenda sana pamoja na mapungufu yetu yote.  Tafakari ya leo inatukumbusha kuendelea kuomba neema ya kujishusha na kuendelea kuomba huruma ya Mungu. Wema wa mungu kwetu ni wa ajabu sana kwani ametusamehe dhambi zetu zote; ametubariki kupita ufahamu wetu; japo tumekumbolewa katika dambi lakini bado sisi tumekuwa wagumu na tunaendelea kutembea katika dunia iliyo jaa dhambi; Mungu anajua khali za roho zetu, anajua vishawishi vyote tunavyokumbana navyo. Lakini bado tunawajibu mkubwa wa kumshukuru kila siku na katika matendo yetu yote.

Tafakari yetu leo inatuongoza vile vile kusoma kutoka katika waraka wa Mtume Paulo 1Watheselonike 5:18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu; lakini kama hatutakuwa watu wa shukurani katika maisha yetu Mtume Paulo katika waraka wake kwa warumi 1: 28-31 anatuasa kuwa Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.  Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; hasara ya kutomshukuru Mungu kwa wema na mafanikio yetu, hutujengea kiburi na kujiona; hutujengea ukosefu wa upendo miongoni mwetu;

Tukisoma kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati 29:10- 15 tunatuonyesha maana halisi ya kumshukuru Mungu kwani vyote tulivyonavyo viantoka kwake yeye; Kwa hiyo Daudi akamhimidi Bwana, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee Bwana, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele.  Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.  Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote.  Basi sasa, Mungu wetu, twakushukuru na kulisifu jina lako tukufu.  Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.  Kwani sisi tu wageni mbele zako, na wasafiri, kama walivyokuwa baba zetu wote; ni kama kivuli siku zetu duniani, wala taraji ya kukaa hapana.

Tafakari yetu leo hii inaelekeza kuwa ni tendo la shukrani kwa Mungu huongeza zaidi Baraka tukisoma Injili ya Luka 17:12 Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,  wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!  Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.  Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;  akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.  Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?  Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?  Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa. 

Tunapomshukuru Mungu tunadhihirishia ulimwengu kuwa Bwana ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba; katika ukuu wake ndio kimbilio langu; na nina kila sababu  ya   kumshukuru kati ya mataifa, na kuendelea kuliimba jina lake la shukrani wakati wote.

Tuhitimishe Tafakari yetu kwa ujumbe huu mzito kuwa Kushukuru sio jambo rahisi, na daima kitendo cha kushukuru kinatoka kwenye moyo wa mwamini wa kweli ambaye daima anampa sifa yesu za ushindi katika kila jambo na sio kujipa sifa yeye mwenyewe Warumi 1: 21 kwa sababu walipomjua Mungu wala hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Tuatakiwa kujawa na Roho mtakatifu daima, kwani bila nguvu ya Roho wa Bwana hatuwezi kuwa watu wa shukrani daima. Najua tunajisahau san asana katika kutoa asante kwa Mungu wakati wote; Je tunafanya hivyo? Je unawakumbuka wana wa Israeli pamoja na kutolewa katika utumwa Misri bado walikuwa sio watu wa shukrani; walijawa na malalamishi na dhihaka juu ya Mungu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo - Amina

Emmanuel Turuka


 

No comments:

Post a Comment