WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, April 26, 2016

MWILI WAKO NI BUSTANI YA KWELI YAMUNGU?



April 26

Tafakari ya leo tujipime   kama mwili wako  ni  bustani ya kweli ya Mungu?  Tukumbuke kuwa Adam na Hawa baada ya kuumbwa walikabidhiwa bustani ya Aden ambayo ilikuwa na kila kitu.

Mungu aliwaambia kufurahi kila kitu katika bustani ile na walikuwa na mamlaka ya vitu vyote ambavyo vilikuwa katika bustani ile.

Tafakari yetu inatukumbusha jinsi Mungu alivyowaambia vyote tumieni lakini mti huu msiuguse. Hivyo hivyo Mungu anaongea nasi leo akitoa maelekezo kuwa : mwili wako ni bustani Takatifu niliyokukabidhi yafurahie maisha na  vitu vyote ambavyo viko ndani ya mwili wako na  hatutakiwi kuvunja amri za Mungu ambazo ni mwongozo wa maisha yetu bora.

Tafakari yetu inaonya kuwa pamoja na  Yesu kutufia msalabani lakini bado tunatakiwa kutumia mwili wetu ambao  ni bustani ya Mungu kwa hekima kubwa.  Kama tutavunja amri za  Mungu nasi tutakuwa kama Adam  na  Hawa tutalaaniwa na kuondolewa katika bustani ya  uzima wa milele.

Tafakari yetu leo inatupa mwamko Mpya kuwa tunatakiwa kuitunza bustani hii ya ajabu ambayo Mwenyezi Mungu ametutunukia kwa kuimwagilia, kuitilia mbolea, na kuifyeka vizuri kila siku kwa kusali bila kuchoka.

Mungu wetu ni mwingi wa huruma, amejaa upendo na anataka kuona kuwa bustani ambayo ametukabidhi ikiwa inastawi; lakini haiwezi kustawi bila msaada wake na  utayari wetu wa  kufuata amri zake.  Hivyo  ni wajibu wetu kuendelea kuomba na kushukuru wakati wote wa  uhai wetu. 

Hii ndio tafakari yetu ya  leo. Amina

Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment