APRIL 6
Wafilipi 2:4-8
Kwa haraka haraka
tu Uvumilivu ni uwezo wa, au ni mazoezi ya, kutambua na kuheshimu imani au
matendo ya wengine; uvumilivu uko katika kila nyanya ya maisha yetu, kuanzia
maisha yetu ya kila siku; TATIZO katika maisha ya kawaida sana,
swala la uvumilivu halizungumzwi sana, tunachokiona sana ni mazungumzo ya
kulipa kisasi;Nafikiri itakuwa jambo njema kama tutaendelea
kufundisha na kuhubiri uvumilivu katika nyanya zote. Pengine fujo hizi ambazo
taifa linaendelea kujionea zikizidi kujitokeza zingeweza kukoma au kupungua
Hii inatokana na
kukosekana mambo makubwa matatu ambayo ni ufahamu au maarifa, hekima na hasa
uvumilivu. Kiongozi asiye mvumilivu anaweza kujikuta anatumia mabavu kutawala
ili watu wajue kuwa yupo, ana nguvu na ana mamlaka.
Na hii falfasa ambayo huangukia kwa wananchi vile vile pale ambapo wanakuwa
hawana uvumilivu; Bibilia inatuonyesha mfano mzuri wa bwana wetu yesu ambaye
pamoja na ukuu wake alijishua na kuvumilia yote na kuwatumikia wote bila makuu:
wafilipi 2:4-8 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie
mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna
ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali
alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa
wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Tafakari yetu leo
inatufundisha kuwa ni ukweli ulio wazi kuwa kiongozi anatakiwa kuwa,
mtulivu, mvumilivu na anayetumia zaidi hekima kuliko mabavu, kiongozi
anatakiwa Kuwa na msimamo wa uvumilivu ni moja ya kazi ngumu zaidi
miongoni mwa viongozi dhidi ya wananchi katika jamii. Ni ukweli ambao
haufichiki kuwa viongozi hawakuzaliwa wakiwa wavumilivu, lakini lazima
tujifunze kuwa wavumilivu. Na hii ni kweli hata kwa jamii inatupasa kuvumiliana
na kumaliza tofauti zetu kwa busara ya majadiliano.
Tafakari yeru tunaangalia
hata katika siasa uvumilivu wa kisiasa unakuza utamaduni wa utawala bora
na ukomavu wa demokrasia; na Kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, wananchi
lazima kuwa tayari kuvumilia na kuvumiliana. Tukumbuke kuwa dhana ya uvumilivu
ni ya msingi sana kwa maendeleo kwani inaruhusu mawazo mapya ndani ya jamii;
kupitia dhana hii ya uvumilivu, kiongozi anakuwa tayari kukubali na
kuheshimu maoni na mawazo ya watu wengine na haki zao kwa uwazi na uhuru.
Katika hali hii,uvumilivu huruhusu kuwepo kwa vyombo huru vya habari
kutumika kama chombo muhimu kuwahabarisha wananchi na kuwasilisha madai yao kwa
viongozi wao.
Tukumbuke kuwa demokrasia
inahitaji vyombo vya habari ambavyo hugeuka kuwa daraja la mawazo kati ya
viongozi na waongozwa. Vyombo huru vya habari husaidia wananchi
kuelewa taratibu ambazo zinaimarisha demokrasia.uvumilivu wa viongozi huru
utasaidia kueneza demokrasia na uwajibikaji kwani wananchi wataweza
kukosoa serikali na ujumbe kufikishwa serikalini bila kuogopa.
Tafakari yetu leo
inatuonyesha ukweli kuwa Falsafa ya Uvumilivu hufunza
na kuwakumbusha viongozi na wananchi wake kuwa wanatakiwa kuishi kulingana na
fikira njema. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hayuko tayari kuamsha fikra
mbaya za uvunjajiwa amani bali daima atajitaidi kuziepusha kwa kuendeleza
uamuzi wa uwazi na kwa kutumia njia ya utulivu wa hekima kupitia
uzoefu makini wa kimantiki: Kiongozi mwenye uvumilivu daima hutafakari, na
kuziweka fikira mahali pamoja kabla ya kufanya uamauzi.Msingi wa kimaadili wa
falsafa ya uvumilivu kama mtaalam mmoja alivyo wahi kusema kuwa kwa ufupi
tunaweza kusema kuwa uvumilivu umesheheni nini?
Tafakari yetu inalenga
kurunzi kwa sisi wananchi wa Tanzania bado tuna kila sababu ya kuendelea kuenzi
na kuthamini uvumilivu miongoni mwetu; uvumilivu kati ya wananchi wa dini
tofauti, kusikilizana na kushauriana kwa faida ya taifa letu; tukiweza kuutumia
uvumilivu katika kiwango cha juu tutafanikiwa kuondoa chuki ambayo inaanza
kueneakatika taifa letu; Ni kweli kama tutaweza kuwaweka wenzetu mbele katika
maisha yetu ya kila siku na kuwa tayari kushirikiana nao tutakuwa tumefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kutekeleza injili hii ya uvumilivu.
Hii ndio tafakari yetu ya
Leo; Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment