March 8
Zaburi ya 119:68
Tafakari ya leo tunaangalia wa Mungu katika Maisha yetu; zaburi ya 119:68
wewe ni mwema na mtenda mema nifundishe amri zako. Hapa tunaona kabisa kuwa kwa
asili Mungu ni Mwema sana katika kila upande tunaougusa katika msiaha yetu. Tukisoma
Injili ya Marko 10:18 Yesu akawaambia,
kw nini kuniita mwema? Hakunaaliye mwema ila mmoja ndiye Mungu. Na
tunapotafsiri uzuri wa mungu pia tunaangalia Matendo; matendo ya Mungu yameajaa;
Wema; Huruma; pendo lisilo kauka; ukarimu wa khali ya juu na daima hutupa sisi
vyote tuviombavyo bila kinyongo.
Tafakari ya leo inatukumbusha je tumeweza kufukiria njinsi Mungu alivyo
mwema kwetu pamoja na mizogo yetu yoye, matatizo yetu bado Mungu amekuwa mwema
sana kwetu; kwani anasema kuwa pamoja na shida na kiburi chenu bado nataka
nitawashushia Baraka ambazo zitatupa sisi furaha sio kwa sababu tunastahili la hasha bali kwa
sababu ya wema wangu. Ni kweli kuwa Mungu ni kwa ajili yetu. Yeye ndiye
muhimili wa upendo wetu kwa asababu ya utakatifu wake na wema wake kwetu.
Hebu
tuangalie zaburi ya 145: 9 Bwana ni mwema kwa watu wote, na rehema zake zi juu
ya kazi zake zote. Hivyo jukumu letu ni kumuhimidia yeye na kulisifu jina lake. Hivyo ni wajibu
wetu kuonya jinsi bwana alivyo mwema. Sisi binadamu wote katika maisha yetu
hapa dunia au tumepotea kwa dhambi zetu na kuwa mbali na Mungu au tumeokolewa
kutokana na dhambi kwa msaama wa upendo wa Mungu kupiti Damu ya bwana wetu Yesu
Kristo.
Tukisoma
waraka wa Mtume wa Paulo kwa Warumi 2:4 Au waudharau wingi wa wema wake na
ustahili wake na uvumilivu wake; usije ya kuwa wema wa Mungu wauvuta upate
kutubu? Daima sisi wanadamu tunajiona kuwa tuko sahihi kwa matendo yetu ukweli
ambao sio kama Mtume Paulo anavyotukumbusha Roman 1:18 kwa maana ghadhabu ya
Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanandamu
waipingaokweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya mungu yajulikana yamekuwa dhahiri
ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia.
Tafakari
ya leo Tunataadhirishwa kuwa pamoja na wema wote wa Mungu lakini anatuacha
katika tama za mioyo yetu, tufuate uchafu, hata tukavunjiana heshima miili
yetu. Anatuacha tuendelee na jeuri yetu , kiburi chetu, majivuno yetu, uongo na
hata pale ambapo hatuwatii wazazi wetu.
Mungu anatuangalia tu bali wema wake uko palepale kama tuko tayari kumpokea
na kufuata taratibu ambazo anataka sisi tufuate. Mungu daima huwaadhibu
wakosefu lakini mara nyingi hukumu yake ya adhabu uchelewa ili wakosefu wapte
kutubu; ama kweli Mungu ni mwema sana kwetu. Lakini tujue kuwa hakuna upendeleo
yeye hutupa sisi nafasi zaidi ya kujirekebisha kupitia toba.
Tafakari
ya leo pia inaendelea kutuonyesha wema wa Mungu kwetu, hata alipotuandalia Bustani ya Adeni alijua
kuwa mwanadamu atamgeuka lakini kwa wema wake hauacha kutekeleza mipango yake.
Alijua kabisa Hawa atadanganywa na Nyoka naye atamdanganya Adamu na hatimaye
Adamu atavunja agano lake na Mungu kwa dhambi ili kiburi cha kuto tii amri ya
Mungu. Na mungu alijua maumivu yote ambayo yatatokana na dhambi hii ya Adamu na
Hawa. Tunajifunza hapa kuwa bado Mungu ameendelea kuonyesha wema wake kwetu
pamoja na kumchukia kwa dhambi zetu.
Pamoja na kuyaona
haya kabla ya Kumuumba binadamu kwa wema wake alimuumba mwanadamu pamoja na
usaliti wote ambao atafanya. Katika matendo yetu yote ambayo mengi
yanamkasirisha Mungu wetu kama kitabu cha Kutoka 34.6-7 Bwana akapita mbele
yake, akatangaza, Bwana Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si
mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu
elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenyekumhesabia mtu
mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenyekuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na
wana wa wana waopia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
Tafakari ya leo
ina umuhimu mkubwa sana kwetu kwani inatufundisha kuwa Mungu kila kitu
amekifanya kizuri kwa wakati wake; na ameweka hiyo milele ndani ya mioyo yao. Ndio
maana mioyo yetu daima inakuwa katika mahangaiko mpaka pale inapata faraja ya
Mungu kupiti wema wake ambao tunaupata kwa njia ya kitubio. Kwa hiyo tukiacha
uovu wetu na kutenda yaliyo halali na haki tutaziponya roho zetu na zitakuwa hai bali tukifanya machukizo
yatokanayo na dhambi na kuto tubu, tutakufa na uovu wetu hapo tusitegemee wema
wa Mungu. Yatupasa tutupilie mbali
kabisa makosa yetu, na tujifanyie moyo mpya ili kufurahia wema wa mungu.
Hii ni tafakari
yetu ya leo. Amina
No comments:
Post a Comment