WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, March 16, 2016

MUNGU NI MSIKILIZAJI MZURI SANA!



March 16

Yohana 15: 14-15

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa kutumia muda wetu mwingi kuongea na Mungu, kwani Mungu ni msikilizaji mzuri sana na hutupa majibu ya maombi yetu. Tunavyoongea na Mungu ni sawa kama tunavyotumia simu katika mawasiliano yetu ya kawaida. Tunavyoongea kwenye simu hatumwoni mtu mwingine kutoka upande wa pili ili tunasikia tu sauti hivyo jukumu letu katika mawasiliano ni kuongea na kusikiliza. Hivyo uhusiano wetu na Mungu ni sawa hivyo hivyo. Tunaongea na Mungu kupitia sala  na tunamsikiliza Mungu kupitia mafundisho ya bibilia kwenye jumuia zetu, nyumba za ibada na katika masifu mbalimbali. Yakobo 5:16 uangameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

Yohana 15: 14:-15 ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Yesu ametoonyesha hapa kuwa yey ni rafiki bora kwani amekuwa msikilizaji mzuri katika maongezi yake na Mungu, kisha ameweza kutuletea sisi ujumbe wa neema kwetu. Asingekuwa msikilizaji mzuri asingeweza kutufahamisha sisi habari njema toka kwa Mungu. Hivyo Mungu ni msikilizaji mzuri sana tunapoongea naye. Mungu anapenda nasi tuweze kuwasiliana naye katika shida zetu na katika mafanikio yetu yote. Hata pale tunaposhindwa katika mahangaiko yetu Mungu anapenda sisi tuongee naye na tumpe taarifa. Na jambo nyingine Mungu anapenda sana sisi tumtarifu mipango yetu kabla hata hatujeanza kufanya. Pale tunapotaka kununua chochote tumshirikishe Mungu kwani  yeye yuko kutuongoza; pale tunapokuwa na mipango ya kusafiri tuongee naye kwani yeye atatembea nasi na atatuongoza. Hata katika maamuzi yetu magumu tuongee na Mungu yeye atatuonyesha njia ya kufikia utekelezaji wa maamuzi yetu.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa Mwenyezi  Mungu ametuagiza tunapongea naye na kumweleza shida zetu, mafanikio yetu au pale tunapoomba msaada hataki sisi tuwe wanafiki hata kidogo; Mathayo 6: 5-7 ; tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin nawaambia wamekwisha kupata thawabu. Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliyesirini; na baba yako aonaye sirini atakujazia. Nanyi mkiwa katika kusali msipayuke payuke, kama watuwa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu yamaneno yao kuwa mengi.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunapoongea na Mungu tunatakiwa tufanye mazungumzo yetu kupitia sala kwa ufasaha kama tunavyongea na rafiki yako mpendwa na unayemweshimu; kwani unapongea na mtu unayemweshimu huwezi tumia menono ya kihuni ya kimtaa mtaa; au kwa sauti ya juu ambapo hata hamwezi kusikilizana; kwa misamiati migumu ambayo hata mwenyewe unapata tabu kuikumbuka;  hutaki kumhdaririsha hata kidogo hata watu wengine wakikusikia ukiongea wafurahie mazungumzo yenu. Ni wazi kuwa kwa kuongea kwa namna hii mwenyezi Mungu atakujibu maombi yako mara moja bila kuchelewa.

Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa tunatakiwa sana tuisome bibilia na kuielewa ili hata tunapoongea, kumsifu au kuomba msaada kwa Mungu tuwe tunajua mwongozo wa namna ya kuongea naye. 1 Petro 3: 15 Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. Na tutaweza tu kuwa tayari kama tutaweza kulielewa na kulishika neno la Mungu; na hata tutakapo kuwa tunaongea naye tutakuwa katika nafasi nzuri. Na ili tuendeleze mahusiano mazuri na Mungu tunatakiwa tutumie muda wetu wa kutosha nay eye, inaweza kuwa kwa kusali pamoja na familia, kusali pamoja na wanajumuia wengine au kwa kusali pekeyako na kwa kufunga Mathayo 6:16-18 tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao,ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin nawaambia, wameshakwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu  kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazia. Yesu hapa anatufundisha kuwa  mfungo hutufanya sisi kuwa karibu zaidi na  mungu lakini kama tutaufanya katika unyenyekevu Mkubwa

Tukumbuke kuwa  mahusiano mazuri yanjengwa katika msingi wa uaminifu;  najua hakuna Ndoa yeyote itadumu au kuwa na mafanikio bila wanandoa kuaminiana; mahusiano ya maisha yetu yanajengwa katika kuaminiana na sio katika sheria. Tunajifunza kwa walimu wa kanisa na wanasheria wakati wa yesu kila kitu chao kilikuwa kimejengwa katika sheria, sheria, sheria. Yesu alituonyesha sisi muhimu wa kuwa waaminifu katika kutekeleza majukumu yetu mbele ya Mungu. Mungu anaitaji Kuwa na Imani na kuwa waaminifu katika kutekeleza maelekezo yake; kwa Imani na Kuamini tutamweka Mungu Mbele katika majukumu yetu. Waebrania 11:1 basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya  mambo yasiyoonekana. Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; Kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yey yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Kuamini ni sawa na Barabara mbili. Ni lazima tumwamini Mungu na Mungu Mungu lazima atuamini sisi, tukizingatia kuwa Mungu ni Yule Yule Jana, leo na Kesho. Mungu ni mwaminifu na wala hatabadilika hata kidogo.

Yesu alituonyesha kupitia agano jipya maisha yake na mawasiliano yake na Mungu hakuwa unazingatia sana sheria Fulani,hata wafuasi wake daima walikuwa wakimwangalia na walikuwa wakishangaa jinsi alivyokuwa akiongea na Mungu kwa utulivu na kwa amani kubwa.

Tukumbuke kuwa mara nyingi tunavyoongea na Mungu tumekuwa watu ambao tunamwogopa tukifikiri kuwa Mungu hutisha, anahasira na sio rahisi kumridhisha; Lakini Yesu ametufundisha kuwa Mungu ni Rafiki yetu wa ajabu na ndio kimbilio letu la kudumu na Mungu anapenda sana kutumia muda wake mwingi nasi kupitia sala zetu na masifu katika ibada zetu;

Tafakari  Ya leo inatushauri kuwa tuondoe vikwazo tulivyojiwekea tunavyoongea na Mungu ili tuendelee kuona uzuri na wema wa Mungu wetu; tunatakiwa tuimarishe mahusiano yetu na Mungu kwa kufuata mafundisho na maagizo yake kama tulivyoelekezwa na Bwana wetu yesu kristo.

Tafakari ya leo inatufundisha kuwa Katika maisha yake Hapa duniani Yesu alikuwa rafiki wa kila mtu alikunywa na wenye dhambi, wakasema , mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Yesu aliwapenda watoto; aliwajali Malaya alipokuwa akiwafundisha kuhusu wokovu ili waachane na dhambi zao na wamrudie mungu; watoza ushuru, wenye dhambi, mwana mpotevu, mwanamke msamalia; na mwanamke ambaye alifumaniwa akizini na ambaye alitakiwa apigwe na mawe mpaka kufa lakini aliyaokoa maisha yake; yesu alimpenda kila mtu hata walimu wa sheria ambao wao walikuwa adui wakuu wa  Yesu. Jambo la msingi tunatakiwa tuimarishe mawasiliano yetu na Mungu Kupitia sala.

Hii ndio Tafakari yetu ya Leo Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment