WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, March 22, 2016

YESU ALIHESHIMU MAMLAKA YA DUNIA PAMOJA NA TABU ZOTE ALIZOPATA KWANI ALIJUA YAMETOKA KWA MUNGU:




March 22,

Yohana 19:10 – 11

Tafakari ya Leo tunaangalia jinsi Yesu alivyokuwa akiheshimu mamlaka ya dunia ni kweli kwamba Utekelezaji wa sheria  za kidunia ni udhihirisho unaonekana wazi kuwa Mamlaka yao yanatoka kwa Mungu. Jukumu la viongozi wa dunia ni kuwapa watu haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru , ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima upendo. Mathayo 22:21 Akawaambia Basi mlipeni Kaisari yaliyo ya  Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu. Yesu aliheshimu  Mamlaka ya dunia na alikuwa akiikosoa pale ilipokuwa ikikosea.

Tafakari inatuonyesha kuwa kwa upande mwingine hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na wale ambao hutumikia serikali hizo wamepata kibali cha kuongoza toka kwa Mungu japo wakati mwingi hutenda kinyume na maelekezo ya Mungu kwa ustawi wa jamii husika. Anayepinga mamlaka ya serikali ya kidunia anakiuka agizo la Mungu. Sheria inatusaidia kufanya yaliyo mema; Watawala ni watumishi wa Mungu , kujitoa wenyewe kwa utawala wa sheria; Mamlaka ni haki halali ya kutekeleza utii. Ni nguvu ya kushawishi au tabia amri. Wagalatia 5: 22-23  Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha , amani, uvumilivu , wema, fadhili , uaminifu, upole na kujizuia. Juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Warumi 13:4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili  ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. Mungu ndiye mwenye mamlaka ya mwisho, na Mungu anatumia serikali za watu wenye mamlaka kwa kusudi lake na letu pia. Biblia inatufundisha kwamba serikali zisizo hudumia watu na kutimiza lengo ambalo Mungu amekusudia Mungu huziondoa.Waebrania 13:17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba watu wafanye hivyo kwa furaha wala  si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.

Warumi 13: 1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye Mamlaka hushindana na agizo la mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao  hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya.basi wataka usimwogope mwenye mamlka? Fanya mema nawe utapata sifa kwake. Kwa sababu hiyo tena mwalipa kodi; kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi iyo hiyo.

Tafakari ya leo inaendelea kutubaanisha kuwa, Mithali 29:18 Pasipo maono watu huacha kujizuia, Bali ana heri mtu Yule ashikaye sheria. Taifa bila nguvu ya Mungu halina baki shagala bagala halifuati sheria. Heri wale wafuatao sheria. Mhubiri 10:17 Heri kwako, nchi mfalame wako akiwa motto wa watu, na wakuu wako hula wakati ufaao, ili makusudi wapate nguvu wala si kwa ajili ya ulevi. 28:2

Viongozi Mithali 11:14 Pasipo Mshauri mzuri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri hujawokovu; mfalme awahukumuye maskini kwa uaminifu; kit chakecha enzi kitathibitika milele.  Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; bali yeye apokeaye rushwa huipindua. Yesu alipopelekwa mbele ya Pilato Yohana 19: 10 – 11 Basi Pilato akamwambia husemi name? hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, name nina mamlaka ya kukusulubisha? Yesu akamjibu, wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana dhambi iliyo kubwa zaidi. Yesu hapa anaendelea kutonyesha kuwa mamlaka zote za dunia zinatoka kwa Mungu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Mamlaka ya Pilato juu ya Yesu bado ilikuwa chini ya Nguvu ya Mungu ambaye alibariki hukumu ya Yesu Kufa Msalabani kupitia mamlaka ya dunia hii kupitia Pilato. Ili Yesu aweze kukamilisha kazi yake ya ukombozi wa Wanadamu ambao walikuwa wamezama katika dimbwi la dhambi; Yesu alipata faraja yake katika wakati huu si kwa sababu ni mapenzi ya Mungu yaliyotimia ndani ya Uongozi wa Pilato; hivyo tunachojifunza hapa ni kuwa Yesu hakuwa na wasiwasi katika mikono ya hofu Pilato , kwani alijua kuwa Pilato alikuwa  katika mikono ya Baba Yesu. Kama 1 Peter 2: 13-17 Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya bwana; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa. Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni mungu. Mpeni heshima mfalme. Mfano wa kuteswa kwa Yesu.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa tusifadhaike na watawala ambao wanaweza kuua miili yetu lakini hawana nguvu ya kuua roho zetu, uwezo ambao wamepewa na Mungu unamipaka yake kwa ustawi wetu kama 2 Mambo ya Nyakati 7:14 ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watanyinyenyekesha, na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitaskikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Pilato ana mamlaka;  Herode ana mamlaka;  Askari wana  mamlaka;  Shetani ana mamlaka; Lakini hakuna hata mmoja wao ambaye anamamlaka yanayojitegemea yote wamepewa na Mungu hivyo hatuna sababu ya kuogopa kwani mamalaka yao kwa wao wenyewe hayana nguvu; na Mungu kamwe hatawapa nguvu za kutuangamiza sisi; Hivyo nasema tena hatutakiwi  Kuogopa; tumshukuru Mungu kwa kutupa sisi thamani kubwa kuliko yeyote lakini inatakiwa tutimize wajibu wetu;

Hii ni tafakari yetu ya leo Nawatakie maandalizi Mema ya Juma kuu kuelekea sikukuu ya Pasaka Siku muhimu katika wokovu wetu Amen

Emmanuel Turuka



No comments:

Post a Comment