WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, March 2, 2016

MIMI NA NYUMBA YANGU TUTAMTUMIKIA BWANA



March 2
JOSHUA 24: 14 -15

Tafakari ya leo tunaangalie ujumbe huu mzito toka  kwa Mtumishi Joshua katika huu ujumbe huu mzito, kuwa yeye na nyumba yake, watamtumikia Bwana. Tukumbuke kuwa Joshua mwana wa Nuni alikuwa amejaa roho ya hekima; maana Musa alikuwa amemwekea mikono yake juu yake na aliishi miaka mia moja na kumi, alimtumikia Mungu katika kipindi hicho chote, aliweza kuona jinsi watu walivyoweza kushindwa kumtumikia Mungu kwa dhati.

Kwa nini Joshua alitambua kuwa nyumba ndio msingi mkubwa wa ibada. Familia ndio msingi pekee wa imani, lakini tunahitaji familia iliyo bora. Tunaona familia aliyokuwa na mfano mzuri wa kuigwa ilikuwa ya Joseph, Mary na Yesu.

Nyumba bora inajengwa katika msingi bora tabia, na tabia njema ndio msingi mzuri wa familia bora ambayo ndio msingi pekee wa ibada na imani. Bibilia inatufundisha kuwa familia lazima ijengwe katika msingi wa Tabia bora. Tukumbuke kuwa familia ni msingi imara kabisa wa imani yetu;  katika Familia wazazi wetu ndio msingi wa familia, ndio maana Joshua alisema kuwa yeye na familia yake watamtumikia Bwana. Wazazi ndio kielelezo cha familia ndio maana bibilia inatukumbusha kuwa tunatakiwa tuwaheshimu wa wazazi wetu ili tupate Baraka ya kuishi mimi miaka mingi yenye kheri hapa dunia.

Joshua alipokuwa na wana wa Israeli alitambua mapungufu haya; ndipo alipowaambia ni wakati wa kufanya maamuzi ni nani utamtumikia Mungu au Miungu ya uongo; na aliwaambia kuwa Mungu Kabwe alazimishi sisi kumtumikia yeye; anatupa sisi uhuru wa kuchagua ndio maana Joshua alitumia hekima hiyo kuwaambia wana mtumikia nani? Lakini yeye na nyumba yake watamtumikia Bwana.
Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kama wazazi tunamchango, mkubwa sana katika kutimiza wazo hili la Joshua; Kama wazazi tunatakiwa kuwajengea watoto wetu, misingi mizuri toka mwanzo wanavyokuwa kwa kuwafundisha maadili mema ya kibibilia na kushiriki ibada kwa moyo ili nao wawe sehemu ya ujumbe wa Joshua. Ni jukumu letu wazazi kuhakikisha kuwa tunatekeleza ujumbe kwa kujenga familia ambayo inampenda Mungu na Kumwogopa Mungu.

Kama familia tunatakiwa kuendelea kuomba ili tuweze kuwa na familia ambayo inasikiliza na kuishi kulingana na bibilia inavyotufundisha. Tunatakiwa kuomba neema ya Mungu itawale, familia zetu na neema yake daima yake ndiwe iwe ni dira ya maisha na mafanikio yetu.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa tunatakiwa tuyaangalie maisha yetu toka huko nyuma mpaka leo hii na mafanikio ambayo tumepata je tumeona ukuu wa mungu?

Familia bora ni ile ambayo inatambua kuwa mafanikio na mitihani yote ya maisha ni mpango wa mungu hivyo tunawajibu wa kusema asante. Na hivyo kuwa tayari kumtumikia Mungu wakati wote. Familia bora inamshukuru Mungu kwa kujaliwa neema za mafanikio na kuwa tayari kutoa na kusaidia wahitaji;

Tafakari hii inatukumbusha umuhimu wa kufanya ibada; hapo tunatimiza wajibu wetu wa kumwogopa Mungu,  Joshua 24: 14a kumwogopa Mungu ni kuonyesha, utii na unyenyekevu kuwa wafuasi ambao tunasali toka ndani kwa imani kubwa. Je sisi wazazi tunaonyesha kuwa ni watu wenye Imani thabiti na wamwogopa Mungu?

Kama wazazi tutaonyesha unyenyekevu juu ya Mungu wetu na watoto wetu watakuwa hivyo; Kama wazazi tutakuwa mfano mzuri katika ibada na kuonyesha mfano mzuri wa kumtolea mungu sadaka na zaka au fungu la kumi na watoto wetu watakuwa hivyo na Mungu atatuneemesha kama kitabu cha malaki kinavyotufundisha. Ujenzi wa nyumba bora ya kumtumikia Bwana inahitaji misingi Imara ya Imani ambayo inatokana na wazazi.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa mimi na nyumba yangu tutaweza tu kumtumikia Mungu kwa tutaweza kutemebea katika matendo yetu mazuri na sio maneno matupu. Hivyo matendo ndiyo yajengayo familia bora; Joshua 24:14b anatukumbusha kuwa kuwe na mwamko wa pekee bila huruti, mwamko wa kiimani na kila sehemu ya maisha yetu lazima ikabidhiwe kwake. Kusimkaribishe kabisa shetani. Familia ikisimama katika umoja wake tutaweza kumtumikia Mungu kwa furaha na faraja kwa mafanikio makubwa sana na neema ya Mungu itakuwa juu ya familia yote.

Tafakari ya leo inatuonyesha jinsi familia nyingi leo hii zinavyoshindwa kwa umoja wake kumtumikia Bwana. Familia zetu zimejaa mifarakano, magomvi tabia mbaya, wakati huo huo wazazi wakionyesha mifano mibaya kwa watoto wao na kupelekea watoto pia kuishi maisha ambayo hayampendezi kabisa Mungu. Wakati umefika tunatakiwa kurudi katika misingi ya Imani kama Joshua alivyotuonyesha umuhimu wa familia katika kumtumikia Bwana. Hatujechelewa tunachotakiwa ni kuanza sasa kuziimarisha familia zetu na kumtumikia Bwana kwa moyo wetu wote.


Tafakari pia inatukumbusha kuwa Mungu hapendi wanafiki, hivyo hili ni somo muhimu sana kwetu, kama kweli tunaamua kumtumikia Mungu tufanye hivyo kwa dhati kabisa. Mungu anatujua sisi kuwa sio wakamilifu, lakini anamchukia sana mtu mnafiki ambaye hujionyesha kwa maneno bali matendo yake ni ya shetani. Mungu ametupa uchaguzi wa chochote tunachotaka kukifanya au kukifuata, au jinsi ya kuishi na hatimaye hata njisi ya kuabudu na kumsifu Mungu, lakini Mungu anapenda sisi tufanye uamuzi sahihi kama Joshua na familia yake walivyofanya  wa kumtumikia BWANA hii ndio tafakari yetu ya leo. 

AMINA

No comments:

Post a Comment