WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, March 21, 2016

MAISHA YA KIROHO NI KAMA MATUMIZI YA KAMERA:



March 21

Wafilipi 3:13,14

Tafakari ya leo tunaangalia kazi kubwa ya Kamera ambayo ni kupiga picha mbali mbali, ili kuweze kupata picha nzuri mpiga anatakiwa kuwa makini kwa kulenga vizuri (focus) ili kuondoa vivuli ambavyo vinasababisha picha kuto kuwa nzuri; hii inaonyesha umuhimu wa kuweke mtazamo wake  juu ya nini anatakiwa afanye kuweza kupata picha nzuri. Maisha yetu ya Kiroho ni sawa na Matumizi ya kamera ni muhimu sana tunavyotekeleza maisha yetu ya Kiroho kuhakikisha wewe ni kulenga jambo sahihi. Lazima tukubali kuwa tunaishi katika wakati ambao kuna vitu vingi ambavyo vinaendelea katika maisha yetu na vinatutoa katika mwelekeo sahihi wa kuishi kama wakristo.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa katika maisha yetu ya kila siku, tumekuwa watu ambao tumejawa na wasiwasi na kusumbukiaa kwa mambo mengi ambayo sio muhimu, na tumesahau kuzingatia au kulenga zaidi katika maisha tunayotakiwa kuishi ya kumtumikia Yesu, Mwenyezi Mungu anataka sisi kuzingatia/kulenga (focus)  zaidi katika dhumuni hasa la maisha yetu hapa duniani; Tukumbuke kuwa maisha yetu daima yanalinganishwa na Kamera ili iweze kutoa picha nzuri inahitaji umakini; Je  tunajua kwa nini Mungu anataka sisi kuzingatia Maisha yetu?  Jibu ni rahisi sana kwa sababu Maisha yetu ni kama kamera; ili kufaninikisha lazima tujipange vizuri; katika upigaji, eneo la kupigia picha, khali ya hewa; na mwelekeo wa mpiga picha.Hivyo  maisha yetu tunatakiwa uchaguzi mzuri katika  kila hatua ambayo tunayoishi kwa utukufu wa Mungu .

Tafakari yetu katka Juma hili kuu inaendelea kutukumbusha kwamba katika kila jambo lolote tunalofanya tufanye mambo mazuri ambayo kuongeza thamani chanya kwa maisha yetu; Mambo mema yataongeza kumbukumbu zetu nzuri na uzoefu chanya; kwa kuzingatia  nini ni muhimu tukichambua kama kamera inavyofanya kazi na kutoa picha nzuri. Sisi tunatakiwa tumlenge Yesu uli tuweze kupata picha yetu nzuri, hata pale tunapo patwa na ugumu wa maisha,na shida mbali mbali katika maisha yetu bado tunatakiwa tuondoe hivyo vivuli ili bado iwe kwa yesu. Hatutakiwi tuondoe focus yetu kwa Yesu eti kwa sababu  tu ya Maumivu ambayo tumeyapata katika maumivu yetu; 

Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki, wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Daima sisi tunaishia kuchukua picha mbaya kwa vile hatuko tayari kuzingatia taratibu nzuri za kupiga picha. Lazima tukubali kufuata utaratibu ambao kristo anataka sisi tufuate tunapopiga picha za kiroho; tukifanya hivyo tutaweza kutimiza  kutimiza furaha yake ni katika sheria ya Bwana, na juu ya sheria sisi yatupasa kuitafakari mchana na usiku.

Tafakari yetu inaendelea kutukumbusha kuwa mkazo/mlengo/Focus itukumbushe kwamba hatupaswi kuendesha maisha yetu kulingana na maoni au mifano ya marafiki zetu. Tunajua hivi sasa dunia yetu iko katika kipindi ambacho kila kitu cha kibinadamu vinakwenda kwa speed ya haraka sana na tunajiona kuwa sisi ndio wamiliki wa dunia hii na tunaweza kufanya chochote tukipendacho  bila msaada wa Mungu. Kama Warumi 12: 1  Basi  hivyo, ndugu na zangu  , nawasihi kwa huruma zake itoeni miili yenu iwe  dhabibu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye Maana. Luka 9:23 Akawaambia wote, yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake anifuate, hii inatufundisha kuwa kama tutamtanguliza Yesu Mbele ya maisha yetu na tutayatoa maisha yetu kwa ajili ya ufalme wa mungu tutapata Picha nzuri sana katika maisha yetu ya hapa duniani na hata mbinguni. Tunatakiwa kujitoa kabisa kwa Mungu na kutenda haki kwa utukufu wa Mungu.  

Tafakari ya leo  inatuelekeza katika ukamilifu wa kweli tunapojiandaa kutumia maisha yetu kama kamera katika maisha yetu ya Kiroho; Tunatakiwa kuendelea kujitathimini sisi wenyewe, kuiangalia taswira ya Picha katika kamera kabla ya kuipiga kwa kuangalia kila upande na kila kona hata kuikuza ili kupata taswira halisi kabla ya kukamilisha kitendo cha kupiga picha. Kabla ya kupiga picha tunatakiwa kurekebisha taswira kwa kujiuliza maswali yafuatayo; Je uhusiano wangu na Mungu Ukoje? Je uhusiano na familia yangu pia ukoje? Je uhusiano wangu Kazini ukoje? Je natimiza mwito wa Mungu kama alivyonielekeza kufanya? Je nina mheshimu Mungu pamoja na amri zake? Je nimeweza kufanya kazi yeyote ambayo imekuwa na matunda ya kiroho katika Jamii yangu na kwangu Mwenyewe?

Hii ndio Tafakari yetu ya leo ; kama tutajibu maswali hayo inavyopasa basi matumizi ya kamera ayetu ni ya kuigiwa mfano na Mwenyezi Mungu atakujalia maisha mazuri sana na hata baadae Mbinguni.


Amen

Emmanuel Turuka
(life is like Camera)

 




No comments:

Post a Comment