WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, June 1, 2016

MWALIMU BORA WA NYAKATI ZOTE NI NANI?




June 1

Yohana 13:13

Tafakari yetu leo tuangalie kwa nini Yesu amekuwa mwalimu bora kupita wote? Tuangalie hata mafundisho yake yalikuwa na nguvu sana sana; tuangalie pale alipotoa hotuba pale mlimani alipomaliza tukisoma kutoka Injili ya Mathayo 7:29 umati wote ulishangaa kwani alikuwa anaongea kama mtu mwenye mamalaka na sio kama wanasheria. Tunajua kuwa Yesu hakuingia darasani. Hakuwa na shahada yeyote kama ilivyo kwa wengi wetu kwani usomi wetu na upapanuaji wetu wa vitu kwa usahihi lazima uende shule kwanza; kwa vipengele hivi kwa kweli alikuwa mwalimu mzuri na bora kuliko mwalimu mwingine yeyote Yule kwa wakati wote; Yesu ni mfano wa kila kitu kizuri na kilichokamilika alikuwa hana makuu, mnyenyekevu, mpole na sio aliyekuwa anafundisha ubinafsi katika mafundisho yake;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Yesu amefundisha sana na mafundisho yake yalikuwa yakipata wasikilizaji wengi sana; ambao wengine walikuwa wakimfuata kila alipokuwa akienda kuhubiri na kufundisha; wengi walimwona kuwa mafundisho yake kama mwalimu bora yalikuwa yamejaa ufafanuzi ambao ulikuwa umejaa ukweli; alikuwa akikemea maovu na kuleta mabaadiliko katika jamii ili waweze kubadilika. Yesu alianza kufundisha akiwa na umri mdogo alipokuwa akiwajibu makuhani na walimu wa sheria maswali hekaluni tukisoma kutoka  Luka 2:46-47 au hata tukisoma Luka 4: 21- 36 ni mwendeleo wa mafundisho yake na aliishia kufundisha kabla ya kufa msalabani pale ambapo aliwafundisha kuhusu karamu ya mwisho.
Tafakari yetu inaumuhimu mkubwa sana kwetu sisi kujifunza kuwa Yesu alikuwa mwalimu bora kwa sababu watu wa kawaida waliweza kumwelewa vizuri sana; alikuwa hafundishi ili ajikweze na kwa kutumia njia ngumu ili watu sio wamwelewe bali wamsifie kuwa mafundisho yake huwezi yaelewa; alikuwa hafundishi kama walimu wa sheria na makuhani kwa kutumia lugha kuapa na kuogopesha watu wengine; bali alikuwa akifundisha kwa kutumia lugha ya kawaida kabisa;alikuwa akifundisha kwa kutoa mifano ya kawaida hata wakulima waliweza mwelewa; hata pale ambapo mfano wake haukueleweka bado alikuwa mpole na kutafuta njia rahisi ya kuwaeleza wasikilizaji wake; warumi 5:2

Tafakari yetu inaendelea kutoonyesha kuwa hata baada ya kufa na kufufuka alikaa na wafuasi wake kwa siku 40 akiwafundisha majukumu ambayo watufanya baada ya yeye kuondoka katika dunia hii Matendo ya Mitume 1:3; aliwafundisha kuwa itatakiwa waende dunia kote wakatangaze injili ya Yesu wakiwabatiza watu kwa jina la baba na la mwana na Roho Mtakatifu Mathayo 28: 19- 20: hivyo tunaona kuwa Yesu alikuwa mwalimu ambaye aliweza kuwafundisha watu wa elimu yeyote na wa mazingira yeyote bila shida yeyote. Na wote walikuwa wakifuatilia mafundisho yake waliweza kumwelewa na kuyafurahia bila shida yeyote ile.

Hii ni tafakri ya leo tunapotambua kwa kifupi uwezo na ubora wa Yesu kama Mwalimu bora sana; Amina

Emmanuel Turuka






No comments:

Post a Comment