WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, June 22, 2016

UNAFIKIRI UMEJIFICHA?


June 22

Mwanzo 3:8


Yeramiha 23:24

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa  mara nyingi kuwa tunafikiri tunaweza kujificha mbele ya uso wa bwana lakini ukweli ni kuwa  mwanadamu hawezi kujificha mbele ya uso wa Mungu  bali tunaweza kufichwa ndani ya Utukufu wa Mungu. Bahati mbaya mawazo yetu yanatudanganya na kujiona kuwa tunaweza kujificha na kufanya chochote tutakacho bila kuonekana mbele ya Macho ya Mungu. Pengine hilo linawezekana kujificha mbele ya macho ya binadamu. Tumekuwa na tabia za kuacha njia zipasazo kufuatwa na  kwenda kinyume na utaratibu tuliokubali kuufuata tukiamini kuwa hakuna anayeweza kuona au kugundua. Lakini tukumbuke kuwa hakuna  kwa namna yeyote ile tunaweza kujificha mbele ya uso wake; tuwe kwenye ngiza; ndani ya chumba; tumejificha kwenye kichaka kwa ujumla hakuna jambo litakalo tendeka ambalo Mwenyezi Mungu asiweze ona. Chochote unachoangalia; kusoma; uanchoamua kuangalia; unachofikiria; mahali popote mabapo unakwenda Mungu anajua kwa nini uko mahali hapo na kwa sababu gani kamwe huwezi jificha mbele ya uso wake;

Tafakari yetu inatukumbusha jinsi Yeramiha 23:24 Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana. Yeramiha 49:10 Lakini nimemwacha Esau hana kitu, nimepafunua mahali pake pa siri, wala hataweza kujificha; kizazi chake kimeangamizwa, na ndugu zake, na jirani zake, naye mwenyewe hayuko. Ezekieli 28:3 Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha; ufunuo 6:15-17 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya ilima,  wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.  Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?

Tafakari yetu leo hebu tujikumbushe nini kiliwatokea Adamu na Hawa tukisoma Mwanzo 3:8-10 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.  Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Adamu na Hawa baada ya kutenda dhambi waliamua kujificha wakitambua kuwa Mungu hataweza waona na hivyo kuwa mbali kabisa na uso wa bwana; kumbe haikuwa hivyo ndivyo yalivyo maisha yetu; akili zetu zinajaa ukungu na kufikiri kuwa tunaweza kufanya dhambi yoyote na Haitaonekana mbele ya Mungu; Sababu kubwa ya kujificha ni kwa sababu tunakuwa tumefanya dhambi mbele ya Mungu;

Tafakari yetu bado inatukumbusha kuwa dhambi na tendo la kujificha hatuwezi kuvitenganisha na hilo ndilo anguko la mwanadamu; lakini pamoja nahii tabia ambayo inasababisha anguko la mwanadamu Mungu daima bado anataka kuturudisha katika njia iliyo bora kabisa; njia ya ukamilifu mkubwa tukisoma Luka 19: 1-5 anasema hivi, Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake.  Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watozaushuru, naye ni tajiri.  Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo.  Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.  Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Mungu yuko tayari kutushirikisha sisi katika ufalme wake, kama tutaacha tabia ya kujificha pamoja na dhambi zetu, tukiwa kama Zakayo tutapata wokovu wa kweli;

Tafakari yetu inatuonyesha kuwa Zakayo alijitambua kwa alikuwa Ni Mtu mwenye dhambi na ambaye alikuwa akichukiwa na watu kutokana na kazi yake. Hivyo baada ya kujificha yeye aliamua kumtafuta Yesu amwone ni  mtu wa aina gani. Alijua kuwa kwa habari juu ya Yesu alijua kuwa atakuwa amekutana na mtu mbaye ataweza msamehe dhambi zake na yeye kuanza kuishi maisha mapya ya wokovu. Hatutakiwi kujificha tunapokosea bali tumkimbilie mwokozi wetu Yesu kristo ili aweze kutusamehe na kutuondolea aibu ambayo inatupelekea sisi kujificha.

Tukumbuke kuwa hakuna yeyote ambaye anaweza kujificha kukimbia uwembo wa Mungu na uwepo wa Bwana wetu Yesu Kristo juu ya Matendo yetu; Tunatakiwa kubadilika kwa tuweze sasa kuwa wakamilifu kwa kuacha dhambi na kuishi maisha mema yanayompendeza mungu.

Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment