WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, June 6, 2016

KUISHI KIUPWEKE NI UCHAGUZI WAKO;



June 6

ZABURI 102:6-7

Tafakari ya leo tunaangalia tatizo nzima la kuwa pekee kwa maneno mengine tatizo la upweke; swali la msingi ambalo tunatakiwa kujiuliza katika tafakari yetu je wewe ni mpweke? Tunafahamu kuwa kuna aina nyingi za upweke na Upweke kwa mtazamo mwingine ni tatizo moja kubwa sana katika jamii yetu; Lakini tukumbuke kuwa ukiwa na Yesu huwezi kuwa mpweke kwani  yeye atakupa faraja unayohitaji; tukisoma bibilia tunajifunza kuwa Yesu amekuwa rafiki mzuri wa wale wote ambao waliluwa wapweke  ndani ya jamii  tukisoma Yohana 5: 5-9 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.  Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?  Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu. Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende. Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo. 

Tafakari yetu inaonyesha kuwa kwa miaka 38 alikuwa mpweke hana rafiki wa kumsaidie ili aweze kupona lakini Yesu alipomwona alimsaidia ili aweze kupona. Hapa yesu ametuonyesha kuwa yeye ndiye rafiki Bora. Tunajua kuwa upweke huleta maumivu ndani ya mwili wetu na huweza kusababisha madhara makubwa sana. Upweke huleta woga; huleta huzuni; mara nyingi tunajaribu kutafuta faraja kutoka kwa wenzetu ndani ya jamii yetu lakini mara chache tunaweza pata faraja ya kweli; lakini faraja ya kweli ya upweke inapatika kutoka kwa Yesu tu; Yohana 11:11 akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. Yohana 11: 25-26 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;  naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Hivyo hata katika mauti yetu tunaye rafiki ambaye ni Yesu.

Tafakari yetu inatukumbusha kuhusu tatizo la upweke linalotokana na dhambi; Upweke ambao ni mbaya sna ni ule unaotokana na kuwa mbali na Mungu. Upweke ambao unaozungumzwa hapa sio ule wa kushindwa kwenda kanisani; unaweza kuwa unakwenda kanisani na kuhudhuria ibada zote na kuwa mtu maarufu katika kanisa lako; lakini tatizo kwa undani kabisa bado humjui Yesu na misingi yake ya Maisha ambayo anataka wewe uishi au kuyafuata; hebu tuyaangalie maisha ya Adam na Hawa walifanya uamuzi mbaya sana wa kumgeuka Mungu wakati Hawa alivyofanya uamuzi mbaya sana; makosa yao na dhambi yao tumerithiswa sisi na hatuwezi kuikwepa hukumu hiyo kama hatutaamua kumfanya Yesu kuwa rafiki yetu mwema na Kuishi kulingana na maagizo yake;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa Upweke dhambi inatufanya sisi tuendelee kuwa wapweke kwa maana inatutenga na Mungu; na hakuna kitu kibaya kwa mtu ambaye anatamka kwa kinywa chake kuwa anamjua yesu lakini ndani ya moyo na matendo yake anafanya matendo ambayo yanpingana na mafundisho ya Yesu; na wakati mwingine upweke wetu unatokana na jinsi ambavyo tunatamani kupata vyote; mguu moja ndani ya mambo ya kimungu na mguu mwingine katika mambo ya kidunia; lakini tukumbuke mambo ya kidunia ambayo yako kinyume na mafundisho ya Mungu hutuweka sisi katika wakati mgumu;

Tafakari yetu inatukumbusha kuhusu mama Msamalia kisimani ambaye alikuwa mpweke alikuwa na wanaume kadhaa; lakini hakuridhika; hakuwa na amani; hakuwa na furaha; yesu alipokwenda kisimani na kupata nafasi ya kuongea naye na kumsamehe dhambi zake alijisikia furaha kama tunavyosoma katika Yohana 4:29 Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? Hivyo katika maisha ya yesu ametujengea urafiki ulio bora na wa kudumu; Tatizo letu nado tunakuwa wagumu kutambua kuwa Yesu ni rafiki wa kweli ambaye ndiye pekee anayeweza kutuondolea Upweke katika maisha yetu; Tukitimiza mafundisho yake kamwe hatuwezi kuwa wapeke hivyo kuendelea kuwa au kukaa katika mazingira ya upweke ni jambo la kujitafutia wenyewe. 
Hii ndio tafakari yetu ya Leo-Amina

Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment