WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Sunday, June 19, 2016

ASANTE BABA KWA UPENDO WAKO MKUU


June 19


Ezekieli: 22:30

Tafakari yetu ya leo inalenga katika kushukuru kwa baraka ya Baba kama Mzazi kiongozi; Mtazamo sahihi mbele ya Mungu:  Zaburi ya 111:10 kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, wote wafanyao hayo wana akili njema, sifa zake zakaa milele. Tukisoma Marko 12:30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwan nguvu zako zote. Yohana 14:15 mkinipenda, mtazanishika amri zangu. Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpigeni Shetani, naye atawakimbia. Mtazamo wetu lazima heshima, utii, upendo, uaminifu, unyenyekevu, utii, worshipful, na sala.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kuiangalia upya tena wajibu wa Baba katika familia hasa katika malezi na makuzi ya Taifa ambalo tugemeo letu ni vijana ambao lazima watokane na malezi Bora ya familia ambayo ndio msingi wa familia bora. Tukisoma kitabu cha Ezekieli 22:30 kinatukumbusha kuwa Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu. Mungu anaonyesha Kiongozi bora wa familia na jamii anayemtaka ambaye atasimama kati yake na nchi; je wewe leo kama baba wa familia uko tayari kuchukua haya majukumu?
Tafakari yetu inatuonyesha kuwa  baba hodari; Baba mwema; baba anayekubalika mbele ya Mungu, lazima awe tayari kuyabeba majukumu kama baba; anatekeleza wajibu wake kama baba; anafikiri kama baba; anatenda kama baba; aliyejaa upendo na msamaha;  akitekeleza haya yote anapata sifa ambazo Mungu ameziweka kwa Kiongozi wa familia; lakini bibilia inatukumbusha kuwa Baba hodari lazima awe ni mtu mzuri, na mtu mzuri ni Yule ambaye anafuata mafundisho na maandiko ya bibilia na kuweza kuwalea watoto katika misingi mizuri ya kiimani. Kama Mithali 3:5 inavyotukumbusha  kuwa jukumu kubwa la Baba liwe; Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zake zote tunawajibu kama Baba kukiri na kuomba mwongozo katika malezi ya watoto wetu, tukumbuke kuwa hakuna kisichowezekana mbele ya Mungu wajibu wetu ni kusimamia imani yetu.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa sisi kama baba wa familia tujue kuwa kwa imani tumekombolewa, na imani ili iweze kuwa dhabiti utiifu ni lazima; Kama baba tunatakiwa kuonyesha mfano mzuri ndani ya familia na kwa kufanya hivyo hata malezi ya vijana wetu yatakuwa rahisi sana Waefeso 2:8-9. Sisi kama wanaume (Baba) tuna tabia ambayo tunataka daima kuwa juu na kutoa maamuzi na wengine wote wayafuate hata bila kukaribisha  ushiriki wa mawazo mengine toka ndani ya familia. Tunatakiwa tujifunze kutoka kwa Mama zetu ambao kwa maumbile yao na busara zao ni rahisi sana kujikabidhi kwa kila wananchokifanya katika mikono ya Mungu. Yesu kwa kutambua ubabe wa sisi wanaume ndipo aliposema Mathayo 18:3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Watoto na wanawake wana tabia ya kuamini na kutegemeana.
Tafakari yetu leo inaendelea kutukumbusha kuwa kwa wanaume kama watatekeleza majukumu yao kwa utaratibu ambao unatakiwa Mungu atakeleza haya kwetu: tukisoma Isaya 40:30-31 Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka;  bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. Hiyo ni ahadi ya Mungu kwetu kama tunasima kwenye mstari sahihi; wakati waraka wa Paulo kwa Wafilipi 4:19 unatukumbusha kuwa ya Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu. Wagalatia 5:16-18 inatukumbusha kuwa Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.  Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. 


 Tafakari yetu inatukumbusha kuwa jukumu la baba ni kuleta matumaini ndani ya familia; Kuleta upendo; amani ; umoja; heshima; uwajibikaji wa kila mtu ndani ya familia; bibilia inatukumbusha kupitia Wakolosai 3:21 kuwa Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tama. Huu ni ujumbe mzuri sana ambao tunatakiwa kuuzingatia ili kuleta matumaini ndani ya familia yetu na umoja wa familia.  Ujumbe huu kutoka Wakolosai 3: 15-20 ni muhimu sana katika siku hii ya leo Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.  Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.  Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao. Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana. Ni ujumbe ambao umetoa mwongozo mzuri sana katika kusherekea siku hii ya leo ya Kumbukumbu ya Akina baba



Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment