WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Thursday, June 9, 2016

JE TUNAANGAMIA KWA KUKOSA MAONO SAHIHI?



June 9

Mithali 29:18

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa ili kufikia malengo yetu ya kufurahia utukufu wa Mungu lazima tuishi tukiwa na malengo au mwelekeo ulio sahihi; tukumbuke kuwa mtu bila malengo ni sawa na mtu kukosa mwelekeo wa kesho. Na Mtu bila kuwa na malengo daima atarudia maisha yake ya Jana. Tukumbuke kuwa maono au uwezo wa  kuona nini kiko mbele yetu ni daraja muhimu sana kati ya sasa na baadae. Bila uwezo huo tujue kuwa lazima tutaangamia,  tukumbuke kuwa maono yanatoa nafasi nzuri sana kwa maumivu yetu kupata sababu ya kufany jambo.  Wale wote ambao hawana maono ya maisha yao wanatumia muda wao mwingi kuongelea njia ambayo inawaletea ugumu wanapojaribu kujiondoa katika maumivu ya maisha.  Wengi wetu tunapitia maisha yetu bila kuelewa majaribu yaliyo mbele yetu. Tunatumia muda mwingi kutembea katika barabara ya manunguniko tukiamini kuwa kila jaribu ambalo liko mbele yetu ni tatizo na lazima tulikimbie.

Tafakari yetu leo hebu tuliangalie hili neno maona kwa maana pana zaidi; kwa tafsiri rahisi ni nini tunaona, na kwa namna gani au kwa njia ipi tunaona; maono ni kama darubini ambayo inatusaidia sisi kuelezea matukio ndani ya maisha yetu, namna ambayo tunawaona wenzetu na hata tunavyo weza mwelezea Mungu. Tatizo nki kuwa kama tuna mikwaruzo katika miwani yetu ni wazi kuwa tutamwona kila mtu kati yetu kuwa anamikwaruzo pia; lakini katika mazingira ya namna hii tatizo litakuwa kwetu kwa sababu maono yetu yatakuwa sio sahihi. Tuelewe kuwa kinachojitokeza ni kuwa  akili yetu inapokea picha kutoka kwenye macho yetu, mioyo yetu inatafsiri picha hizo. Kama mioyo yetu inapata uchungu, au inakuwa na wivu, au inaumia au inaadhirika kwa namna moja au nyingine  maono  ya moyo ndio yanaharibika. Tukisoma  Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. Na kweli inatokana na kuwa na maono sahihi na sio maono ya kujifanyizia.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa maono sahihi lazima yatoke kwa mungu,  kama kitabu cha mithali 15: 22-24 kinavyotukumbusha Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika. Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini! Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini. Kama nilivyosema hapo juu maono lazima yatoke kwa Mungu, wajibu wetu sisi kama binadamu ni katika kusaidia kukamilisha na kutimiliza ndoto ya maono hayo ili iweze timia. Ukamilifu wetu sisi binadamu lazima uwe katika kulielewa neno la Mungu kwa kusoma na kwa mafundisho yake. Kama Mithali 16:9 inavyosema Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake. Au ukisoma Zaburi ya 37:23-24 Hatua za mtu zaimarishwa na Bwana, Naye aipenda njia yake.  Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na kumtegemeza

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa ili tuweze kuifikia safari hii ya utukufu wa Mungu lazima maono na malengo yrtu juu ya Mungu yatimie. Tumepewa uwezo wa maono lakini tatizo letu hatujui jinsi ya kutumia maono haya katika kufanikisha na kufikia ushindi wa kweli. Akili yetu imeendelea kufungwa Mioyo yetu imeendela kujaa kutu na kiburi na kushindwa kuona maono yanayotufaa katika maisha yetu na kuishi kuwa na maono finyu ya kibinadamu nay a kidunia ambayo hayatusaidii kwani upeo wake ni mdogo na wa kidunia tu. Yatupasa kuamka sasa na kuwa na maono stahiki kwa utukufu wa Mungu na maisha yetu. Kwani pale ambapo hakuna maono watu wangu wanaangamia.

Hii ndio tafakari yetu ya leo- Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment