WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, June 14, 2016

MIMI NIMEBARIKIWA


June 14

Mathayo 7:11

Tafakari yetu leo tuangalie neema ya kubarikiwa. Mungu alimwambia Abrahamu kuwa  nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; Mweneyezi Mungu anatupa sisi Baraka ili nasi tuweze kuwabariki wengine; Kubarikiwa kwa namna yeyote ile sio maana yake tu kujisikia vizuri, kuwa na furaha na utulivu bali tunatakiwa nasi tuwabariki wengine pia; msingi huu wa Baraka tunayopata ambayo hutusaidia sisi kuwa na amani na furaha tunatakiwa tuwahamishie na wengine pia; Baraka lazima zitirike kwenda kwa wengine ambao nao wanahitaji kubarikiwa.

Tafakari yetu leo inatukumbusha injili ya Luka 18:29-30 Akawaambia, Hakika nawaambia, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi, au wana, kwa ajili ya ufalme wa Mungu, asiyepokea zaidi mara nyingi katika zamani hizi, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele. Tukumbuke kuwa tunapopata nafasi ya kuwabariki wengine nasi pia tunabarikiwa na Mungu kamwe hataacha kutubariki. Kwa mtu ambaye yuko tayari kuwa saidia wengine kamwe Mungu hata funga milango yake ya Baraka juu yake. Na Baraka za mungu zinakuja kama mvua na neema yake kama juu;

Tafakari yetu inatukumbsha kuwa tuna kila sababu za kufurahi kwani  tunapowakumbuka wengine katika shida zao kwa wema ule ule ambao Mungu ametujalia sisi: Mungu naye anachukua maujumu ya matatizo yetu nah ii baraka ya pekee nay a ajabu. Tunajua kuwa Mungu ni hodari katika kushugulikia shida zetu kwa wakati wake ambao ndio mwafaka kwetu. Tukumbuke kuwsa Baraka ambazo tutazitoa kwa wengine  zitaturudia sisi wenyewe zaidi ya vile tunavyowabariki wengine. Kadiri ambavyo sisi tunawasaidia watu wengine ndivyo hivyo hivyo Mungu atakavyo tubariki sisi. Tukisoma Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa. Hivyo ni wajibu wetu kuwabariki wengine ili tuweze nasi kubarikiwa kwa namna yeyote ile ambayo ni njema na inayokubalika mikononi mwa Mungu.

Tafakari yetu leo inatuonyesha kuwa Lengo la kwanza la Mungu ni kutubariki; nasio kutulaani; au kutuangamiza; na tufahamu kuwa Mungu pekee ndiye mwenye nguvu ya Kubariki  na kuongoza Dunia yote; Mungu anaweza fanya kitu chochote katika ulimwengu huu; ana nguvu na uwezo wa kubariki au kuangamiza kama Wafilipi 3:20 inavyosema Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; Mungu ni mwema na ahadi zake ni za ajabu sana; kama tunavyosoma Mathayo 7:11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? 

Tukumbuke kuwa Mungu ni rafiki sio adui na kamwe hawezi kuzuia Baraka yeye hutoa Baraka na sisi tunatakiwa kuzipokea na kuwasaidia wengine; Hii ndio tafakari yetu ya leo tunahimizwa kufanya mema zaidi na sio maovu.        Amina

Emmanuel Turuka








No comments:

Post a Comment