WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Wednesday, June 29, 2016

UNAZIJUA SILAHA ANAZOTUMIA SHETANI KUTUANGAMIZA?


June 29

2 Wakoritho 2:11


Tafakari ya leo tuangalia jinsi shetani anavyotumia silaha ambazo tunazo kutuangusha sisi wenyewe; shetani anapinu nyingi sana za kutuangamiza kabisa kama hatuko makini; tukisoma 2 Wakoritho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. Huu ni wajibu wetu kuzuia mbinu zote za shetani kwani tunamjua vizuri, na mikakati yake yote; silaha moja nzito sana ya shetani ni kuwa na majivuno silaha hiyo ni hatari sana katika maisha yetu kama wafuasi wa kristo; mara nyingi sisi kama binadamu hatuoni tofauti yeyote pale mambo yanapokwenda vizuri tukifurahia utajiri na amani mfano mzuri tukimwangalia Lucifer mkuu wa malaika ambaye alikuwa akiishi vizuri chini ya utawala Mungu; hatimaye tama na majidai yalimjia kupingana na Mungu. Timoteo 3:6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 

Tukisoma Ezekieli 28: 14-17 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto.  Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.  Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa hatuna sababu ya kuwa na majivuno kama 1 Wakoritho: 13:8 inavyosema Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; tunatakiwa kujiepusha na huluka ya majivuno yatokanayo na kufanya mambo mazuri kama Yesu alivyokuwa akiwafundisha wafuasi wake katika Luka 18:9-14 Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.  Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Hatutakiwa kujihesabia haki wenyewe hata kama tunafanya mema Mungu peke yake ndiye ajuae matendo yetu na anakipimo sahihi cha kutupima na kutupa thawabu tunayostahili.

Tafakari yetu inatusisitiza kuwa lazima tuendelee kuchukua taadhari  dhidi ya adui wa roho zetu. Tukisoma 1 Petro 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Ni ukweli ambao haupingiki kuwa unapopigana vita na unataarifa za kutosha juu ya adui yako, hukusaidia na kupunguza ugumu wa vita yako na uwezekano mkubwa sana wa ushindi; tukumbuke kuwa Mungu alikuwako tangu kuumbwa kwa dunia lakini shetani shetani hakuwako toka mwanzo wa dunia; Mungu kamwe haumbi kitu chochote kibaya; Mungu huumba vitu vyote katikaukamilifu mkuu; Adamu na Hawa waliumbwa katika ukamilifu na ubora uleule kama yeye alivyo; hata shetani alipoumbwa alikuwa katika ubora wa ukamilifu na alikuwa haitwi shetani; na alikuwa akijulikana kama Nyota ya asubuhi tukisoma

Tafakari yetu inatukumbusha anguko la Lusuferi ( Nyota ya Asubuhi) tukisoma kitabu cha Isaya 14:11-12 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika.  Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa. Kabla ya kuwa Shetani alikuwa mkuu wa malaika wote, alikuwa akiwaongoza malaika katika masifu mbele ya Mungu; alijaliwa nguvu nyingi na uwezo mkubwa kutoka kwa Mungu; Lakini alianguka katika dhambi alipotaka kufanana na Mungu na kugeuka kuwa shetani. Hivyo huyu adui bado ni mbaya katika maisha yetu ya kiroho kwa sababu ananguvu nyingi bado na Mungu hakuziondoa nguvu hizo. Kwa nini lakini Mungu hakuzichukua hizo nguvu za shetani ambazo zinatutesa leo; kwa sababu Mungu hachukui zawadi ambazo anakupa wewe hata pale unaposhindwa kutimiza yale ambayo yeye anataka wewe utimize mbele yako. Je wewe ukimpa mtu zawadi pale mnapotofautiana unaichukua ile zawadi tena; kwa ujumla jibu ni hapana;

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa tujiepushe na majivuno, mwonekano wetu, nafasi ambazo tunazo kimaisha,akili zetu, uwezo wetu kifedha kwani hivyo ni baadhi tu vitu ambavyo shetani anavitumia katika vita vya kutuangusha ili tusiweze kumtumikia Mungu vile itupasavyo sisi kuishi; tunatakiwa tutumie uwezo wa kiakili tuliojaliwa katika kumtumikia Mungu na sio shetani; tunatakiwa kuwa makini na kuendelea kuzitambua silaha ambazo shetani anazitumia juu yetu katika kutuangamiza; Amka leo na uwe mshindi wa maisha ya kiroho na maisha ya baadae.

Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina-


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment