WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Friday, June 17, 2016

MIMI NIPO PAMOJA NAWE DAIMA


June 17

Isaya 41:10

Tafakari ya leo tujikumbushe ahadi ya Mungu ya kuwa yeye yupo pamoja nasi muda wote; usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Maagizo ni agizo nzuri kuwa hatutakiwi kuwa na mashaka: wasiwasi au hofu; la msingi msisitizo wake kwetu ni huu;  Nipo pamoja nawe; hivyo hatutakiwi kuogopa; Mimi ni Mungu wako, usifadhaike mimi ni Mungu wako; Mimi nitakuimarisha; Mimi nitakusaidia; Mimi nitakushika kwa mkono wangu wa kuume wenye haki.

Tafakari ya yetu inatuimarisha kuwa Munguyupo nasi; Mungu ni Mungu wangu: msingi wa kujiepusha na woga au hofu ni kusimama kwa kuzingatia misingi ya ahadi za Mungu; na moja ya nguzo ya msingi kabisa ni Kuamini kuwa Mungu ni Mungu wako na yuko tayari kukuimarisha na kukuongoza na kukuondoa na hofu zote; hasa pale tunapofikiria magumu na mahangaiko yote ya maisha bado tunatakiwa tuondoa hofu na mashaka kwa kumtegemea Mungu hivyo Tunakumbushwa kuwa Niko nanyi siku zote.  Hatutakiwi kumwogopa yeyote kwani Mungu ndio msingi wa kila kitu kwa sababu  Mungu ni mwenye nguvu. Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.  Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.  Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.  Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana.  Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako. Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! Hivyo sina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment