WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Tuesday, June 7, 2016

KUGEUZA SHAVU LA UPANDE WA KULIA MAANA YAKE NI NINI?



June 7

Mathayo 5:39

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa  tunatakiwa kuelewa kwa nini Yesu aliwaambia wafuasi wake sentesi hii; pengine ni vyema kujua mazingira na umati ambao Yesu alikuwa akiuhubiria tukisoma Mathayo 5:38 alianza kwa kusema kuwa Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Yesu alikuwa ameziangalia sheria zilizokuwa zikitumika wakati huu kama tukisoma Kutoka 21:24 ilikuwa ikisisitiza kuwa jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu; adhabu hizi zilikuwa zikitolewa katika wakati huo ili kutenda haki katika mazingira yako kama kitabu cha Kumbukumbu la Torati 19: 20-21  Na watakaosalia watasikia na kuogopa, wasifanye tena uovu mfano wa huo katikati yako.  Wala jicho lako lisiwe na huruma; uzima kwa uzima, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa katika kipindi hicho sheria ambazo zilikuwa zikitumika zilikuwa zimetawaliwa na ulipizaji kisasi; kila mwenzako anachokufanyia na wewe mfanyie hivyo hivyo; lakini mafundisho ya Yesu Mlimani yalikuwa yakilenga kuondoa dhana hii ya kupipiza kisasa na kuanza kujenga dhana ya msamaha dhana ya upendo; dhana ya kuanza kuuliza maswali kwa nini ? je nikusaidie vipi; Yesu alianza kuleta dhana ya mazungumzo katikati ya tukio; yesu alikuwa anatufundisha kuwa tunatakiwa kuwa na subira tukisoma Warumi 12:17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Au tukisoma Mithali 24:29 Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa sisi kama wakristo tusijihami wakati wowote wa fujo, hujuma au vitisho; yesu hakusema kuwa hatuna sababu ya kujilinda lakini kama wakristo tunatakiwa kuonyesha upendo wetu tunavyokabiliana na matukio ya namna hii katika maisha yetu na tusisababishe sisi wenyewe kufanya vitu ambavyo vitaashiria hasira, chuki na fujo; yesu anasisitiza sisi kufanya retreat katika wakati wote ili kuepuka mapigano, fujo na kuchukua hatua ya kujilinda wenyewe na kuomba msaada wa nguvu za sheria kama Polisi. Mathayo 26:51-53 Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.  Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.  Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? Hivyo kazi ya malipizi tumwachie Mungu yeye anajua lini na wapi anaweza fanya malipizi.
Tafakari yetu leo inasimama katika kuepuka kulipiza kisasi; kugeuza shavu la kulia ni dalili ya unyenyekevu; ni dalili ya kukomaa kimaadili kama mkristo; hata kama unatukanwa huna haja ya kujibu matusi unatakiwa kuonyesha upendo wa ajabu ili hata Yule ambaye anakutukana au anataka kukufanyia fujo atabadilika na kuacha fujo; Yesu anatuonyesha kuwa fujo nyingi ni sababu ya kuvunjiana heshima, dhuluma. Ukiangalia magovi mengi husababishwa na majibishano, kutuvumiliana, dharau, hivi unyenyekevu huweza punguza matatizo haya yote; Hivyo kugeuza shavu la kulia ni kuonyesha unyenyekezu na kufufua dhana ya mazungumzo.

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa utu wetu unakuja kwa sababu tumeumbwa na Mungu; umuhimu wetu unakuja kwa sababu tumeitwa na Yesu ili tuibadilishe hii dunia; na Nguvu yetu inatokana na roho Mtakatifu ambaye ametujaza sisi nguvu ya kupokea matusi kutoka kwa wengine na kuyajibu kwa busara na upendo kama Yesu alivyokuwa akiwajibu wale wote waliokuwa wakimtukana.
Tafakari yetu inatuhimiza kuwa kugeuza shavu la kulia maana halisi tusiwajibu wale wanaotutukana kwa matusi bali kwa unyenyekevu na upole; wale wanaotuchukia kwa chuki bali tuwajibu kwa upendo. Tuige mfano wa Yesu yeye alikuwa kweli hazina ya Uvumilivu,unyenyekevu, upendo na msamaha.

Hii ndio Tafakari yetu ya leo Amina


Emmanuel Turuka

No comments:

Post a Comment