WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Monday, June 27, 2016

MNAFIKI KATIKA IMANI


June 27

Mathayo 6: 5-7

Tafakari ya leo inatukumbusha kuhusu utekelezaji wa majukumu yahusuyo imani ambayo yanampendeza Mungu. Je Mungu anapenda sadaka tunayoitolea kwake iwe ya aina gani? Je sisi tunapomwomba au kumtolea sadaka tunakuwa katika msingi wa namna gani ni ule unaopendeza Mungu au tunakuwa wanafiki mbele ya macho ya mataifa? Tukisoma bibilia tunaona kuwa Mungu anataka Moyo wa kweli, moyo thabiti ambao unajitoa kweli kwa Mungu. Mungu hataki mtu mwenye sura mbili ambazo zinatofautiana na ukweli wa Moyo wake; Mungu hajali kuhusu mwonekano wetu wa nje bali anataka mwonekano wetu wa ndani ambao unatakiwa kuwa umejaa ukweli na imani: Mungu anatazama unyenyekevu wa mioyo yetu; Mungu anatak kuona utakatifu wa mioyo yetu; na sio unafiki wa mioyo yetu. Mungu aliuona unafiki huu toka kuumbwa kwa dunia; tukifungua bibilia tunaona tatizo la unafiki liko toka katika kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo wa Yohana. Kwa msingi hii Hata Mwokozi wetu Yesu alionyesha kwa vitendo unafiki ambao ulukuwako katika Nyumba za ibada; Unafiki ambao ulikuwako miongoni mwa wanasheria; hata kati ya mitume wale 12 kulikuwako na unafiki pia.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa  tukimsoma nabiia Amos katika sura ya 5: 21-23 Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.  Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona. Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.  Lakini hukumu na itelemke kama maji, na haki kama maji makuu. Katika maneno mengine Mungu anatufundisha kuwa katika vitu vyote ambavyo nimewapa; katika vitu vyote anbavyo vimevumbuliwa; katika vitu vyote ambavyo nimeamsrisha sisi tumeshindwa kuvitekeleza ipasavyo na badala yake tumevigeuza na kuvudharau na kufanya mambo tujuavyo sisi; hata kuomba tuonavyo sisi inafaa; hivyo hata tunavyoomba tunaishia zaidi kujipamba kwa nje na sio kwa ndani; huu ndio unafiki ambao Yesu aliukataa.

Tunavyoendela na tafakari yetu hebu tuangalie Ole ambazo Mathayo alizitoa katika sura ya 23:13-24 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.  [Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]  Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnazunguka katika bahari na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehanum mara mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.  Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, Mtu atakayeapa kwa hekalu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amejifunga.  Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.  Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.  Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo kwa nje yaonekana kuwa mazuri, bali ndani yamejaa mifupa ya wafu, na uchafu wote. Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi.  Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnayajenga makaburi ya manabii, na kuyapamba maziara ya wenye haki, Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum? 

Tafakari yetu inatukumbusha kuwa  mnafiki hujifanya kuwa ni mwenye haki kwa mwonekano wa nje; lakini kwa mwonekano wa ndani sinyo alivyo; maisha yake yamejaa uwongo na mara nyingi ikiwa mwongo mwonekano wako wan je unakuwa na tofauti na mwonekano wa ndani; hivyo mtu wa namna hiyo anakuwa sio mwaminifu; sio mkweli; mpenda kujisifu hata kwa vitu ambavyo hawezi kutimiza; anataka kupata kibali kutoka kwa watu wanaomzunguka na kupendwa. Je wewe unatabia hiyo? Bwana wetu yesu Kristo alitutaanzarisha kuwa tukisoma Mathayo 6: 1-4 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;  sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. Hii ni taathari ambayo Bwana wetu Yesu aliitoa kwetu ili kuwa wakamilifu wa kweli;

Tafakri ya leo inatukumbusha kuwa lazima tujitambue kuwa sisi ni wenye dhambi na tumemkosea Mungu Ukisoma warumi 3:23 Ukisoma Mithali 20:9. Tunatakiwa kuelewa kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu Warumi 5:8 na lazima tuwe tayari kupokea matokeo ya dhambi zetu Warumi 6:23 na Yatupasa kuomba msamaha wa dhambi zetu Matendo ya Mitume 20:21/ 3:19. Tusipokuwa wanafiki ni rahisi kujenga imani yetu ya kweli juu ya Mungu. Huu ni wajibu wetu wa msingi na tunapaswa kuutekeleza bila shuruti;

Hii ndio tafakari yetu ya leo – Amina

Emmanuel Turuka


No comments:

Post a Comment